kwani Rais alie mfukuza kazi alikua Mkristo, jadili hoja ilio muhusisha, kwani Kikwete akiwa waziri hazina aligundua nini, umesahau maafisa kumi n mbili makamishna alifukuzwa nao......mfumo wa kulindana ndio umeua nchi hii.Wewe acha kuzungumzia marehemu,
Kuweka record yako vizuri Kighoma Malima ni muadilifu wala hakuwa fisadi...mafisadi unawajua vizuri kina mkapa, yona, mramba, chenge, RA, edward lowassa, ...
ama unataka kubadilisha hii thread kwenye mkondo uliopo kwenye mkondo mwingine kabisaaa..maana wanaomtuhumu kighoma wamejazwa na chuki za "Kidini" hasa wakristo nothing more..call a spade a spade...hakuna kiongozi muadilifu kama kighoma
Chadema hakujatulia, Mbowe ashambuliwa
Imeandikwa na Theopista Nsanzugwanko; Tarehe: 27th November 2009 @ 23:58
ALIYEKUWA kiongozi wa mambo ya Bunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Juju Danda, amejiondoa katika Chama hicho.
Danda amesema jijini Dar es Salaam kuwa, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) anapaswa kukagua hesabu ya Chadema na kwamba, hati zikiwa safi yupo tayari kufungwa jela.
Amedai kuwa, taratibu za manunuzi hazifuatwi katika chama hicho, na kwamba, manunuzi yote ya chama yanafanywa na Antony Komu ambaye ni mtu wa karibu na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.
Danda amedai kuwa, Mbowe ameifanya Chadema kama kampuni yake binafsi.
Nikiwa mmoja wa walipa kodi wa nchi hii, nina wajibu wa kuhakikisha fedha zinazotolewa kama ruzuku kwa vyama vya siasa zinatumika kwa mujibu wa sheria hivyo basi naomba mkaguzi mkuu wa fedha za Serikali aikague Chadema na ikipata hati safi mkondo wa sheria uchukue hatua dhidi yake amesema Danda.
Kwa mujibu wa Danda, Mbowe tu anafahamu zilipo fedha za ruzuku, makusanyo yanayopatikana kupitia ujumbe wa simu, na fedha zinazotoka kwa wahisani.
Amesema, wananchi wengi wanakichangia chama hicho lakini Mbowe amekuwa akibadili michango hiyo kuwa yake binafsi na kudai kukikopesha Chama.
Ametoa mfano kwa kudai kuwa, kuna mfanyabiashara jijini Dar es Salaam aliyechangia milioni 43 kwa ajili ya uchaguzi wa ubunge Tarime mwaka 2008 lakini Mbowe alidai kukikopesha chama.
Chadema wamekuwa wakilia na wimbo wa ufisadi kila siku lakini,shilingi milioni 35 alizochota Mbowe katika ruzuku ya Desemba mwaka jana ni sawa na asilimia 52 ya ruzuku ya chama kwa mwezi, wakati Sh.bilioni 133 za EPA ni sawa na asilimia 23 tu ya matumizi ya serikali kwa mwezi amedai Danda.
Danda amesema,yeye na aliyekuwa afisa habari wa chadema, walifukuzwa kwa kuwa walitofautiana kimtazamo na 'mmiliki huyo' hasa baada ya kuonesha hisia zao za kumuunga mkono Zitto Kabwe alipotaka kugombea uenyekiti wa chama hicho.
Amedai kuwa, baada ya kufukuzwa alitakiwa kuomba msamaha ili arudishwe kwenye chama lakini alikataa.
Danda amedai kuwa, hajafikiria atahamia chama gani lakini akishaamua ataondoka na wanachama wengi toka Chadema.
Alisema ndani ya Chadema kuna makundi mawili, kundi la Mbowe lenye maisha mazuri na magari ya kifahari na lile la Zitto lenye wanachama wanaomuunga mkono mwanasiasa huyo.
Nimeaga nimerudi tena kidogo tu nitoe jibu la sentensi moja: NAAMINI WAZEE WALIMSHAURI ZITTO AJITOE NA ZITTO AKAKUBALI KWA SABABU CHADEMA NI ZAIDI YA MBOWE NA ZITTO. Alamsiki, siku nyingine Kituko.
JJ
ukianza na Wangwe,Kafulila hakuna hata mmoja ambae alifukuzwa nnje ya utaratibu uliopo ndani ya katiba ya CHADEMA, sema shida yako umelelewa kwenye mfumo wa kubembelezana na kuamini kua bila mtu fulani hakuna maisha.
Hakuna alie juu ya Chama, maana Chama ni taasisi, ndio maana alikuwepo Mtei Mtei , akaja Bob, sasa Mbowe.....maisha yanakwenda.
Tumaini kama kiongozi mfano JK ANAYOVYOSHINDWA kuwawajibisha wasaidizi wake, kwako huo ni mfano wa demokrasia, amakweli kiwi cha macho huletwa na malezi mabaya ya tangu udogo.
[/COLOR]
Ha ha haa! Kuna ngoma inaitwa mduara.
mimi najiepusha kuzungumzia CUF, kwasababu zangu binafsi, ila swala la UDINI linawatafuna sana, watajuana na CCM, ila siioni falsafa maridhawa ndani ya ya chama hiko, ndo maana niko CHADEMA. kwanza CUF sio tishio kwetu, ni kama TLP tu, sisi tuwaza kupambana na CCM ALIE Madarakani, anaetuletea unasikini....nyinyi mnapambana na asie na mamlaka....ama dola, ama kweli.Ungeniuliza ni kiongozi gani wa chama cha siasa una-appreaciate uongozi wake so far ningesema..ni "Ibrahimu Lipumba" wa CUF
mimi najiepusha kuzungumzia CUF, kwasababu zangu binafsi, ila swala la UDINI linawatafuna sana, watajuana na CCM, ila siioni falsafa maridhawa ndani ya ya chama hiko, ndo maana niko CHADEMA. kwanza CUF sio tishio kwetu, ni kama TLP tu, sisi tuwaza kupambana na CCM ALIE Madarakani, anaetuletea unasikini....nyinyi mnapambana na asie na mamlaka....ama dola, ama kweli.
kwangu issue sio kua Muislamu , mpagani , mpare , mpemba au Mmasai, cha muhimu ni namna gani unaweza kuongoza na kuleta mambo mema kwa nnchi yako....
Kesho tutakuwa na Kongamano la Vijana, halafu kuanzia tarehe 30 Novemba, 2009 mpaka tarehe 3 Disemba 2009 tutakuwa kwenye mfululizo wa vikao vya juu vya chama tukiutathmini mwaka 2009 na kupanga mwelekeo wa chama kwenda mwaka 2010.
ni wapi nimezungumzia udini, wewe na CUF wako mtajuana kama vikao vya kuhamasishana mnafanyia misikitini ama laah, ila nijuacho mimi moja ya malengo ya CHADEMA nikushika dola, kwa maendeleo ya Taifa, lengo letu sikupambana na vyama visivyo na dola.......Sababu zako binafsi ni "UDINI" kama kawaida unajificha sehemu tambarare
CUF siyo tishio..kwako..lol unafurahisha baraza au?...CUF ni wa pili kwenye uchaguzi wa serikali za mitaani uliopita...tlp sijui ni ya ngapi wapi na wapi?
Ibrahimu hajalaumiwa na wanachama for nepotism, kuonea wanachama wa CUF na ubadirifu wa fedha...lakini huyo jamaa yako mbowe na slaa kila siku wanachama wanalalamika je wakipewa dola..
Namna gani gani unaweza kuongoza na kuleta mambo kwa nchi yako ha ha ha ..hayo ni matokeo ya uadilifu wako binafsi na uadilifu wa taasisi yako..kusimamia hayo..tumeshuhudia CCM na Chadema kwenye swala la kusimamia uadilifu....wanaboa...long way to go for chadema as an institution.
Ngoja awaudhi wenye chama ndio atajua unachooongea..dogo bado anabebwa kwa nepi...
ni wapi nimezungumzia udini, wewe na CUF wako mtajuana kama vikao vya kuhamasishana mnafanyia misikitini ama laah, ila nijuacho mimi moja ya malengo ya CHADEMA nikushika dola, kwa maendeleo ya Taifa, lengo letu sikupambana na vyama visivyo na dola.......
CCM wenyewe wanajua nani ni adui yao kwanza, maana wanapambana kwa nguvu zao zote.
Tumaini
Asante kwa mchango wako, ugonjwa upi huo? Kelele zipi hasa unatushauri tuzingatie kama sauti maridhawa za kuchochea mabadiliko ndani ya CHADEMA na taifa letu kwa ujumla? Naomba uziweke kwenye mpangilio ili tuzielewe maana tuliwahi kufundishwa tukiwa watoto kuwa kelele ni sauti zisizo katika mpangilio maalum?
Iddi njema kwa watanzania wote hususan waislamu.
JJ
Awaudhi wenye chama kwa kukubali kununuliwa na RA ili awe anawapigia ndogondogo -- kumtetea kujananja katika ufisadi wake na kujaribu kuibomoa Chadema. Na kila mara huwa ni Mbowe dikteta, Mbowe anatafuna ruzuku -- hivi hakuna hoja nyingine? Hoja hii inachosha sana -- imeshatumika huko nyuma na wengi tu viongozi waliotimuliwa kutoka vyama vingine vya siasa kama NCCR, TLP, CUF etc.Halafu naunga mkono akina kafulia na huyu dandi ni sisimizi tu -- na nawahakikishia RA hatawajali tena, kwani hawawezi kumsaidia wakiwa katika chama ambacho kimepoteza kabisa mwelekeo -- yaani NCCR. Mbatia aliaibika Tarime kutokana na kukubali kuwa wakala wa CCM kujaribu kuizuia Chadema.mbatia aliweza kufanikiwa Pemba miaka kadha iliyopita alipoisaidia CCM kuchukua viti kule alikopiga kambi -- huku hao hao CCM wakimnyang'sanya kiti katika jimbo Kigoma. Akina Dandi wawe tayari kufanya hiyo kazi ya UWAKALA -- kwa RA na CCM!!!
Siyo vibaya kijipa moyo...endeleeCHADEMA, HALI NI SHWARI...........
Kesho tutakuwa na Kongamano la Vijana, halafu kuanzia tarehe 30 Novemba, 2009 mpaka tarehe 3 Disemba 2009 tutakuwa kwenye mfululizo wa vikao vya juu vya chama tukiutathmini mwaka 2009 na kupanga mwelekeo wa chama kwenda mwaka 2010.
Vijana wote wapenda mabadiliko haya shime tuungane, maana adui yetu CCM ametangaza vita tayari kuelekea uchaguzi mkuu, tukutane kesho.
kumbe kuna mafungamano , sasa naanza kuelewa haya mambo.....Umenena ndugu yangu -- ingawa huyo dandi bado hajaenda NCCR. Labda ataenda CUF -- lakini kule pia RA ana mkono. . Kumbe alikuwa kihiyo wa kutupa! Mwingine ramadhani Mzee alitimuliwa CUF na akataja hayo hayo ya kutafuna ruzuku. . Siku hizi "sisimizi" (nami nakubali ni sisimizi) akiondoka Chadema, basi linakuwa jambo kubwa kweli kweli -- magazeti ya RA yanaliendeleza mpaka vichwa vya habari vinasikitisha na kutia doa katika fani ya uandishi. lakini sababu ya hii inajulikana -- ufisadi tu.
Wapendwa wanaJF wenzangu:
Nimekuwa mchangiaji wa nadra sana wa JF kutokana na sababu ambazo nilishawahi kueleza hapa siku za nyuma, mojawapo ukiwa ni ushauri wa baadhi yenu ambao niliuheshimu.
Nimekuwa msomaji wa majadiliano yanayoendelea kuhusu mustakabali wa taifa letu, na katika baadhi ya mijadala imetajwa CHADEMA na jina langu limekuwa likijitokeza tokeza. Aidha baadhi yenu mniandikia ujumbe nije hapa kufafanua baadhi ya mambo yanayohusu CHADEMA hususani yale yanayonihusisha kwa namna moja au nyingine.
Niliwahi kuandika hapa kwa kirefu naichukuliaje JF, lakini moja ya mtazamo wangu kuhusu JFni kuwa hivi ni chombo cha habari, pia ni kama kijiwe cha kijamii cha mijadala, lakini pia ni kama mkutano wa majadiliano katika mji(town hall meeting), naitazama pia JF kama mkutano wa hadhara ambao kila mmoja yuko huru kuhutubia!.
Katika muktadha huo, kama ambavyo nashiriki mijadala katika matukio yenye sura ya hayo hapo juu, najihisi nina wajibu kwangu binafsi na kwenu kuja kushiriki mijadala mara kadhaa.
Kwa kuanzia nawaletea taarifa hii rasmi, ambayo nimeitoa leo kwa niaba ya ya CHADEMA. Taarifa hii inajibu baadhi ya maswali ambayo yamekuwa yakiulizwa hasa kuhusu yanayoendelea ndani ya chama katika siku za karibuni.
Tamko hilo mnaweza kulipata kwa kubonyeza hapa: http://www.chadema.or.tz/habari/habari.php?id=103
Kesho tutakuwa na Kongamano la Vijana, halafu kuanzia tarehe 30 Novemba, 2009 mpaka tarehe 3 Disemba 2009 tutakuwa kwenye mfululizo wa vikao vya juu vya chama tukiutathmini mwaka 2009 na kupanga mwelekeo wa chama kwenda mwaka 2010.
Hivyo, naomba muendelee na mjadala na kama kuna maswali yatakayoulizwa nitakuja kuyajibu moja baada ya jingine baada ya tarehe hizo.
Salamu zangu za baraka ya Iddi kwa waislamu, ni siku nzuri ya kutafakari aya kwenye kurani tukufu mathalani Al Heed 57:25, Al-Nisa 4:35, Al-Maidah 5:8
Alisema ndani ya Chadema kuna makundi mawili, kundi la Mbowe lenye maisha mazuri na magari ya kifahari na lile la Zitto lenye wanachama wanaomuunga mkono mwanasiasa huyo.