CHADEMA: Mwelekeo wa chama katika mwaka 2012

n00b

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
1,006
2,667
Wakuu nimepokea Tamko la Chadema kuhusu mwelekeo wa Chama mwaka 2012 pamoja na kumbukumbu ya mauaji yaliyotokea Arusha mwaka jana.
attachment.php

attachment.php
 

Attachments

  • TAARIFA ya CHADEMA KWA UMMA.doc
    1.4 MB · Views: 128
  • tamko1.png
    tamko1.png
    159.5 KB · Views: 406
  • tamko2.png
    tamko2.png
    134.1 KB · Views: 383
My Lord! Kilichonifurahisha hatimaye Slaa amesikia kilio cha watanzania na kuteua mkurugenzi mpya wa habari na uenezi.Hongera John Mnyika.Tunataka utoe habari kwa ukamilifu
 
hii Barua naona kama imechakachuliwa hivi.Naona maneno yanaungwaungwa mwenye habari iliyo na mtililiko mzuri atoa siyo huyu ,au Mnyika utupe habari kama ni za kweli
 
Nafurahia kwamba angalau kwenye Kurugenzi ya Habarri imeboreshwa na kuongezewa nguvu,Tunategemea timu ya watu watatu wakishirikiana na wenzeo Mnyika,Tumbo na Tumaini basi sasa tutahabarishwa mambo mengi ya kiutendaji ya chama

Naomba Chadema wasisahau swala la usatawi wa watoto na wanachi waliokatika mazingira hatarishi kwa mfano watoto wa mitaani, maalbino, watoto kutoka kwenye familia maskini sana wazee wanaonyongwa wanawake wanaonyanywaswa wanaume wanaochomwa mioto kufikiriwa wachawi na wale wanaohamishwa kwenye makazi yao ya asili kwa uonevu.

Swala lingine wanatakiwa kujikita pamoja na wanachi katika kukubaliana kitaifa wao itikadi yao ya kisiasa na kiuchumi ni ipi au wanasimamia nini ,ni la muhimu hili kuweza kutengeneza vijitabu vitavyoelezea hali halisi ya jambo hilo.

Swala la katiba litapaswa kupewe jicho la pekee kutumia njia za kisayansi na kiushwawishi ili lisipolwe na CCM na serikali kwa ajili ya manufaa yao wenyewe
 
Habari ya jioni wadau..mpaka sasa nashindwa kujua ni kwa nini tamko hili halijaonekana hapa.! Naomba mods au waandishi walilo nalo watuwekee hapa tupate ABC's. Leo JF imekuwa siyo ya kawaida kwa kushindwa kuweka tamko hili. Am waiting guys.
 
Mjadala wa Katiba mpya ambao ulilitawala mwaka jana kuanzia Januari hadi Desemba huenda ukaendelea kutawala siasa za mwaka huu kwani Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimeshatangaza kuwa hiyo ni moja ya ajenda zake kuu mwaka huu.
Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willbroad Slaa anasema nia ya chama hicho ni kuendelea kushinikiza mabadiliko makubwa yafanyike ili mwisho wa siku ipatikane katiba mpya iliyobora ambayo itakuwa na manufaa kwa watanzania wote kwa miaka mingi ijayo.

Dk. Slaa anasema chama hakiridhishwi na mwenendo wa siasa, kiuchumi na kijamii katika mwaka uliopita na kimedhamiria kuitisha mkutano wa kamati kuu ya chama Januari mwaka huu ambapo pamoja na mambo mengine utapokea taarifa maalum ya hali ya

siasa na kufanya maamuzi juu ya hatua za haraka za kusimamia uwajibikaji serikalini kwa maslahi ya umma .
Anasema mbali na Katiba kipaumbele kingine kikubwa ni kunusuru uchumi wa nchi na kupunguza ongezeko la kupanda kwa

gharama za maisha kwa wananchi na haswa mfumko wa bei na kuongeza uzalishaji na kushughulikia vyanzo vya migogoro katika maeneo mbalimbali badala ya kukabiliana na matokeo haswa migogoro ya ardhi.

Anasema sekretarieti ya chama haijaridhishwa na uwajibikaji katika serikali kwa umma ikiwa miaka minne imepita tangu kutolewa hadharani kwa Orodha ya Mafisadi (List of Shame) Septemba 15 mwaka 2007.

“Chama kilitarajia kwamba mwaka 2011 ulikuwa wa kukamilisha uchunguzi na uchukuaji wa hatua dhidi ya wahusika katika kashfa mbalimbali ili kurejesha utamaduni wa uwajibikaji. Badala yake serikali imeendelea kuahirisha kuchukua hatua kamili serikalini, Bungeni na hata ndani ya chama chenyewe,”.

“Katika kipindi cha mwaka 2011 pamejitokeza tena ufisadi mwingine katika ngazi mbalimbali na utamaduni umekuwa ni ule ule wa maazimio kupitishwa ikiwemo na Bunge bila utekelezaji wa haraka wa serikali na hatua stahiki za kinidhamu na kisheria kuchukuliwa kwa wahusikam,”.

Dk. Slaa anasema serikali ilikubali kuanzisha mchakato wa kufanya mabadiliko ya katiba kwa shinikizo kutoka kwa umma wa watanzaia hivyo ni wajibu wa Chadema kuendelea kushinikiza kuboreshwa kwa muswada wa kuundwa kwa Katiba mpya.

“Haikuwa dhamira ya serikali tangu mwanzo kuweka utaratibu bora wa kisheria wa kusimamia mchakato wa katiba mpya muswada huo uliwasilishwa kwa hati ya dharura, ukapingwa na kambi ya upinzani na wadau wengine, hatua iliyoisukuma serikali

kuiondoa hati ya dharura lakini ikaendeleza hodhi ile ile katika upitishwaji wa muswada tarehe 18 Novemba 2011 na hatimaye kusainiwa na Rais tarehe 29 Novemba 2011,” anasema Dk. Slaa.

Anasema Chadema haijaridhika na kauli ya Rais Kikwete “kuwa ndani ya robo ya kwanza ya mwaka ujao uundaji wa Tume ya Katiba utakuwa umekamilika” kwa kuwa kauli hiyo haisemi chochote kuhusu haja ya sheria ya mabadiliko ya katiba ya mwaka

2011 kufanyiwa marekebisho makubwa kwenye Mkutano wa Bunge unaotarajiwa kuanza tarehe 31 Januari 2012 kabla ya vyombo vinavyohusika na mchakato wa katiba havijaanza kuundwa na kufanya kazi.

“Tunahimiza chama nchi nzima kuendelea kutekeleza maazimio ya kamati kuu ya chama ya tarehe 20 Novemba 2011 kuhusu mchakato wa mabadiliko ya katiba na waraka namba 3 wa Katibu Mkuu wa chama kuhusu sheria ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2011.

Tunahimiza viongozi wote wa chama na wa kuchaguliwa kupitia CHADEMA kuendelea kushirikiana na wadau kutoa elimu kwa umma kupitia mikutano na njia nyinginezo juu ya mapungufu ya sheria husika na haja ya mabadiliko kufanyika kabla ya vyombo kwa mujibu wa sheria kuanza kazi yake,” anasema.

Kuhusu mwelekeo wa Uchumi, Dk. Slaa anasema chama kimesikitishwa na hali tete na mwelekeo mbovu wa uchumi wa nchi na kupanda kwa gharama ya maisha kwa wananchi kunakoendelea kusababishwa na pamoja na mambo mengine mfumuko wa bei na kushuka kwa thamani ya shilingi na kwamba hali hiyo sio tu ni tishio kwa maisha ya wananchi bali pia kwa usalama wa nchi kwa ujumla.

“ Rais Kikwete hakueleza hatua thabiti na za haraka za serikali katika kukabiliana na hali hii kwenye hotuba yake tarehe 31 Disemba 2011. Badala yake ameendeleza utaratibu ule ule wa hotuba zake za kuorodhesha visingizio vya nje vya uchumi wa dunia bila kuweka mkazo katika kueleza hatua za kuinua uchumi wa ndani pamoja na kulinda wananchi dhidi ya misukosuko ya nje,” anasema.

Anasema Chadema inaitahadharisha serikali juu ya mkakati unaoendelea wa kukabiliana na hali hii kwa kuongeza malipo kwa baadhi ya viongozi waandamizi kama wabunge kukabiliana na ugumu wa maisha huku yenyewe serikali ikiikabili hali hiyo kwa

kupandisha bei ya huduma za msingi zinazotolewa na taasisi zake huku ikimuacha mwananchi kwenye mazingira ya kipato kile kile wakati sekta ya umma ikiungana na sekta binafsi kupandisha bei za bidhaa na huduma.

Anasema hali hiyo ikiaachwa iendelee itakuza pengo la wenye nacho na wasionacho katika taifa na wakati huo huo itaongeza zaidi gharama za maisha kwa wananchi hususani wa kipato cha chini tofauti na ahadi ya Rais Kikwete na CCM ya kuleta maisha bora kwa kila mtanzania.

Aidha, anasema serikali ilipaswa kueleza ukweli wananchi kuhusu hali mbaya ya kifedha ambayo inalikabili taifa hivi sasa kwa kupungua kwa mapato ya ndani na ya nje ukilinganisha na bajeti iliyopitishwa na kufafanua mkakati wa kuongeza uzalishaji na kupunguza matumizi ya serikali.

“Tutawasilisha taarifa maalum kuhusu mapendekezo ya hatua za kuchukuliwa na chama pamoja na viongozi wa kuchaguliwa hususani wabunge ili kuweza kuzingatia masuala husika katika kazi za chama na za kuwakilisha wananchi” anasema.

“Tunatarajia kwamba serikali ya CCM itazingatia mwito huu na kuwasilisha mpango maalum katika mkutano wa Bunge unaonza tarehe 31 Januari 2011 na kama sehemu ya utekelezaji wa mpango huo utafanya mapitio ya bajeti za Wizara zote za Serikali kwa kuzingatia maoni yaliyotolewa na Kambi ya Upinzani Bungeni.

Pia, tunatarajia serikali kama ilivyofanya kwa suala la Katiba Mpya itazingatia hoja toka kwenye ilani ya CHADEMA ya mwaka 2010 kuhusu hatua ambazo serikali inapaswa kuchukua katika kuinua uchumi wa nchi na kupunguza gharama za maisha kwa wananchi kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuongeza uzalishaji,” anasema Dk. Slaa.

Kuhusu mwelekeo wa Jamii, anasema Chadema imezingatia kwamba pamoja na ahadi za kila mwaka za serikali bado mwelekeo wa kuboresha huduma za msingi za kijamii hususani elimu, afya, maji na nyinginezo miaka 50 baada ya uhuru haulingani na umri wa taifa na rasilimali ambazo nchi inazo.

Aidha, anasema Chadema inatambua kwamba kuna ongezeko la migogoro ya kijamii katika taifa ambayo serikali badala ya kushughulikia vyanzo vya migogoro hiyo inashughulikia matokeo na hivyo kuendeleza migogoro zaidi.
Anasema Chadema inaitaka CCM, serikali na vyombo vya dola kubadilika kwenye mwaka 2012 ili kuepusha nchi kuingia katika

malumbano na migogoro ya kijamii na badala yake watimize ahadi kuhusu huduma za jamii kama ambavyo waliahidi katika ilani yao ya uchaguzi.

“Hatujaridhika na hatua za serikali katika kushughulikia migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji, serikali na umma, na wananchi na wawekezaji katika maeneo mbalimbali yenye rasilimali za kilimo, misitu, madini na nyinginezo,” anasema.

Anasema chama kinatoa rai kwa umma watanzania na wanachama kutambua kwamba katika kusimamia vipaumbele vya kisiasa, kiuchumi na kijamii vya taifa na chama; CHADEMA kimejipanga kutimiza wajibu wa chama mbadala na chama kikuu cha upinzani nchini katika mwaka 2012 kwenye vyombo vya uwakilishi ambavyo tuna wajumbe wa kuchaguliwa na katika ngazi mbalimbali za chama.

Anasema pamoja na kutumia mikutano ya maamuzi ya kiserikali na kichama chama kitaendelea kutumia pia njia nyingine zote za kidemokrasia ili kuunganisha umma katika kuwezesha uwajibikaji na kuchochea maendeleo.

Anasema wananchi watarajie CHADEMA kuendelea na ziara kuanzia mapema mwaka huu katika mikoa mbalimbali mijini na vijijini tukiweka kipaumbele kwa maeneo ambayo chama hakikufika kwa ukamilifu katika mwaka 2011 kwa mujibu wa ratiba

itayotangazwa na kamati kuu ya chama. Aidha na kwamba kitaendelea na maandalizi kwa ajili ya ushiriki mzito wa chama katika chaguzi mbalimbali za marudio zilizojitokeza na zitakazoendelea kujitokeza katika ngazi mbalimbali.

Dk. Slaa anasema pamoja na kuunganisha umma kuhamasisha demokrasia na maendeleo kwa maslahi ya taifa, mwaka 2012 ni mwaka wa kuanza kwa uchaguzi mkuu wa ndani ya chama kuanzia ngazi ya msingi, matawi na kuendelea mpaka uchaguzi wa

ngazi ya taifa utakapofanyika mwaka 2013 kwa ajili ya kujenga oganizesheni thabiti ya chama nchi nzima.
“Tunahimiza wanachama na wapenzi wa chama nchi nzima kuwasiliana na ngazi zao za chama kwa ajili ya kupata maelezo

kuhusu waraka namba moja na namba mbili wa Katibu Mkuu wa mwaka 2011 kuhusu uchaguzi wa ndani ya chama ili kuweza kushiriki katika kutimiza wajibu huu muhimu kwa chama na kwa taifa,”anasema.




CHANZO: NIPASHE
 
Nampongeza Ndesamburo wa chadema kwa kutambua umuhimu wa mahakama ya kadhi kwa waislam wa Tanzania
 
mtiririko mzuri, mabadiliko mazuri pia ya kiutendaji,,,,,tunategemea mazuri na makubwa kutoka CHADEMA. chama chenye matumaini ya watanzania tulio wengi,,,,,,,,,,,,,,
get going CHADEMA......
we are backing you up......!!!!!!!!:poa:poa:poa:poa:poa:poa:poa
 
Back
Top Bottom