CHADEMA Mwanza; Mbunge na Meya Hapatoshi!

CHADEMA Mwanza; Mbunge na Meya Hapatoshi!

MAFILILI

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2011
Posts
2,377
Reaction score
1,200
[h=2] Meya ampongeza Mgeja kwa kuiponda Chadema [/h] umanne, Aprili 30, 2013 06:30 Na Mwandishi Wetu, Mwanza


MEYA wa Manispaa ya Ilemela, Henry Matata, ameibuka na kumpongeza Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, kwa kuponda Baraza la Mawaziri litakaloundwa na Serikali ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Aidha, baadhi ya wanachama na wafuasi wa chama hicho wameonyesha kukerwa na uteuzi huo na wameeleza hiyo ni dharau kwa watu wengine na inaonyesha nje ya wabunge hao hakuna mtu wa kushika wadhifa huo kama ambavyo Mbunge wa Nyagamana, Ezekia Wenje, anatavyotaka umma uamini hivyo.

Akizungumza na MTANZANIA jana kuhusu baraza hilo, Matata, alisema huo ni ubakaji wa demokrasia ndani ya chama.

Alisema Wenje hana uwezo wa kutangaza baraza la mawaziri, bali mwenye dhamana hiyo ni rais pekee anayeweza kufanya hivyo.

“Mimi ni mwanachama wa Chadema, kuwa Meya nimepelekwa na katibu wa wilaya kwa barua iliyonitambulisha kuwa ni mgombea wa chama. Siwezi kusema siko Chadema ukiachana na mambo ya Mahakama. Namshangaa Wenje, katangaza baraza la mawaziri wa Mwanza au wa Tanzania. Anawezaje kutangaza baraza la mawaziri wakati mwenye dhamana hiyo ni rais. Anawavika kilemba cha ukoka wabunge hao,
” alisema Matata.

Alisema watu wenye busara wanamwona mbunge huyo hana akili kwa madai kuwa Chadema inaweza kushika dola, endapo tu itaachana na mtindo wa kufukuza wanachama wake kwa kisingizio cha usaliti na fitina zinazofanywa na baadhi ya watu kwa chuki binafsi.

Alisema fitina zao za kuwachukia wanachama kuwa wasaliti na kuvurugana, itawawia vigumu kushika dola kama anavyodhani Wenje kwamba hawawezi kushika dola hadi washikamane na akatoa pongezi kwa Mgeja kuwa anaona mbali kutokana na ujasiri wake wa kuponda baraza hilo.

“Huwezi kupata dola kama hamna mshikamano, Chadema wanapaswa kujenga hoja ili wananchi wenye busara wawaelewe, si kwa maandamano, vurugu ama kufitiniana na kuvurugana. Lazima viongozi wawe na busara ya kushawishi wananchi na hao wachache walionao wasiwafukuze ili washinde na kupata dola,” alisema Matata.

Mwanachama mwingnie wa Chadema aliyejitambulisha kwa jina moja la Lucy, alisema kitendo cha Wenje kutaja majina ya wabunge wa kuunda baraza la mawaziri ni kupora uhuru wa wanachama na kubaka demokrasia na madaraka.

“Tunalalamika CCM wanabebana na kulindana, wanapeana vyeo kumbe hata sisi viongozi wetu wanataka tuamini wabunge waliotajwa ndiyo wanafaa kuwa mawaziri, nje ya hao hakuna mwanachama anayefaa kuwa rais ama waziri. Huko ni kubaka na kuminya demokrasia,” alisema Lucy.

Mwingine alijitambulisha kwa jina moja la Lutaigulwa, alisema kuna udikteta ndani ya Chadema na ndiyo maana Wenje kwa udikteta huo alimua kupanga safu hata kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015.

Alisema kupangwa kwa safu hiyo ya mawaziri, kumeonyesha dhamira ya wazi na ya dhati kuwa viongozi nia yao ni madaraka na si kuwatetea Watanzania.

Baraza hilo la Wenje limewachefua na kuwagawa Chadema na kusababisha baadhi ya wafuasi na wanachama wake kumpongeza Mgeja kuwa ni jasiri, baada ya kuliponda hadharani kuwa halina mashiko na viongozi wake wanabaka na kuminya demokrasia.

Mgeja alisema Dk. Slaa kutajwa kwake kuwa mgombea urais, ni kuminya demokrasia na uhuru wa wanachama.
 
Huyo ni Meya wa Mahakama,Matata alivuliwa uanachama kwa shutuma za kuhongwa pesa na CCM ili ahujumu chama na alipoitwa kwenye vikao halali vya Chama ili ajitete alijibu kuwa yeye hajawahi kukataa pesa maishani mwake,kwa vile alikua bega kwa bega na Diwani wa Igoma Adams Chagulani wote wawili walivuliwa uanachama katika vikao halali vya chama,walichofanya ni kukimbilia mahakamani kufungua kesi.

Pili hata sishangai kwa kauli yake maana hata alipokuja Mangula Mwanza Matata alipanda Jukwaani na kusema CCM oyeeee na akasema atahakikisha anashilikiana na CCM kuwa inalejesha majimbo yote ya Nyamagana na Ilemela ili yarudi CCM sasa guts za kusema huyu ni CDM inatoka wapi?
 
Hakuna Mtanzania mwenye akili timamu atakayekubali taifa hili la Tanzania lipate aibu kwenye jamii ya kimataifa kwa kuwaruhusu CHADEMA waingie madarakani.
 
Kinana wa mwanza huyu anashida sana,acha aruke ruke tu damu ikikata atatulia
 
Yote kwa yote; Wenje kabaka demokrasia kwa kutangaza baraza la mawaziri pamoja na kumtangaza Dr. Slaa kuwa mgombea wa Urais 2015; kwa vile mtu wa Chadema umeweka kibanzi jichoni!
 
kaa kimya kuuficha upumbavu na ujuha wako hupati usingizi kisa CHADEMA embu hangaika na familia yako kwanza coz mwanao wa kwanza kaishia la sita wa pili ndo huyo ana zero mwingine kashidwa mtihani wa kadato pili lol!

Halafu wewe unapiga domo hapa kutetea mijitu isiyo kufaa kwa lolote.unakazi we mtoto wewe mwenyewe shule hakuna na kama unayo umeunga vyeti kibao ndo mana hata kufikiri huwezi du!!

Jitu kubwaa mawazo kidogo. Embu kaongeze elimu kidogo basi walau upate hadhi ya hata kuchangia hoja za wasomi. Ujumbe wa SUMU na MAFILILI Sababu ndo wanafanana character's.
 
Mwanzo umeanza vizuri kama hivi»Meya ampongeza Mgeja kwa kuiponda Chadema

umanne, Aprili 30, 2013 06:30 Na Mwandishi Wetu, Mwanza

Lakini mwisho hukutaka kuainisha kuwa habari hii imeandikwa na gazeti la UHURU peke yake na mwandishi wenu huyo ni mwigulu
 
Kuishiwa propaganda ni hatari sana. Hivi CCM wamekuwa bogus namna hii? Sipati picha...au huu ni utani?....akili kama mende
 
Hakuna Mtanzania mwenye akili timamu atakayekubali taifa hili la Tanzania lipate aibu kwenye jamii ya kimataifa kwa kuwaruhusu CHADEMA waingie madarakani.

lipate aibu mara ngapi wewe kubwa jinga, nyambafu mmeshatutia aibu sana wazungu na waafrika wenzetu nchi zingine wanatuona hamnazo rasilimali kibao bt nchi na wananchi wake ni masikini tunazidiwa na rwanda,mikataba ya kifisadi,mmeua elimu yetu wakati nyie wanenu wanasoma nje kwa kutumia kodi zetu,hospitali huduma hovyo,hakuna maji safi wala machafu,ajira ndo usiseme,watz hata mlo mmoja shida,vipi ulaji wa mapanki mwanza,kuua na kutesa watu hivi zombi huyaoni haya deni la taifa hili ni janga kubwa,nchi masikini sana duniani tz 50yrs ya uhuru mjing..ajing.a wewe unasema cdm watatutia aibu wakati nyie mmesha tuvua nguo kwa wakwe cdm wanataka kutufunika mnadai eti wanatutia aibu plz wait Arusha kuna uchaguzi,vp ya kilosa uchaguzi wa vitongoji viwili juzi kati umeskia mlivyogaragazwa pamoja kinanda na nepi kwenda huko lakini hola.
 
Hakuna Mtanzania mwenye akili timamu atakayekubali taifa hili la Tanzania lipate aibu kwenye jamii ya kimataifa kwa kuwaruhusu CHADEMA waingie madarakani.

Hakuna Mtanzania yeyote yule mwenye akiri timamu atakayekubali taifa hili lipate aibu kwenye jamii ya kimataifa kwa kuwaruhusu CCM waingie madarakani 2015.
 
MATATA NI MTU MWENYE UELEWA WA HALI YA CHINI MNO HATA KUMJADILI HUMU NI KUMPA HADHI ASIYO STAHILI HATA KIDOGO.Baada ya kulijua hilo CHADEMA Waliamua kuachana naye.
 
MATATA ni CDM mpeni ushirikiano,unesheni ushirikiano wanaCHADEMA.
 
Hivi Mafilili kumbe uko low namna hiyo ? ukiandika upuuzi mwingine kama huu Ntakudharau kuliko ulivyowahi kudharauliwa tangu Uzaliwe ! Hivi Matata naye ni wa Kujadiliwa humu ! Huyo si alihongwa hela ya Bia 5 tu akasaliti wananchi , hana hadhi ya kuingizwa Jf huyo Meya wa barafu , jua likiwaka tu atayeyuka .
 
Waacheni wafu wazikane wao kwa wao. CHADEMA chimbianeni makabuli bhana, maana hakuna mwingine wa kuwafanyia kazi hiyo hapa Tanzania.
 
Back
Top Bottom