KipimaPembe
JF-Expert Member
- Aug 5, 2007
- 1,285
- 699
Jasusi,
..binafsi ningependa Chadema wawe na viongozi wengi zaidi wa juu wanaoshughulika na siasa FULL TIME.
..wakati wengine wanakwazwa na Uchaga wa Mbowe, mimi nakwazwa na the fact kwamba huenda atakuwa na majukumu mengi mengine kama biashara zake na ubunge.
..kitu kingine ningependa Chadema wawe na kitengo cha RESEARCH kuwasaidia wabunge wao ktk kujenga hoja bungeni. hoja wanazojenga zisitegemee uchacharikaji wa mbunge husika bila kuongezewa uzito with research uliyofanywa na staffers.
..suala lingine ni VISIBILITY kama alivyolielekeza Zakumi. kama serikali inapitisha bajeti inayopunja fedha ktk miradi ya maendeleo ya mkoa kama Rukwa, basi Chadema wanapaswa kwenda kuzungumza na wananchi wa mkoa huo kuwaelezea kilichojiri bungeni.
..kuna wakati CCM ilituma mawaziri kwenda "kuwaeleza" wananchi kuhusu bajeti. ingependeza na Chadema nao wawe na utaratibu wa kwenda kuwaeleza wananchi mapungufu ya bajeti kila baada ya kipindi cha bunge.
..Chadema pia wawe efficient zaidi ktk kutoa habari zao. wakati wa uchaguzi CCM wali-dominate mno magazeti, radio stations, blogs, and tv. kunatakiwa kuwepo na mkakati wa ku-challenge CCM dominance ktk vyombo vya habari.
Just a thought, kama Dr. Slaa asingegombea Urais, success ya Chadema ingekuwa kama ilivyo? If Chadema wangeng'ang'ania kuwa wao ni Bunge na kutoweka mtu mwenye wasifu kama Dr. Slaa, je matokeo yake yangekuwa sawa na ya leo?
Hata kama ni Ngeli na Ngali, lakini lazima tujiulize, ni vipi Dr. Slaa amekisaidia Chadema hususan wakati wa Uchaguzi au hata mchango wake tangu aingie Chadema kwa Chadema kupata mvuto na msukumo ulioko sasa hivi.
Simvunjii Freeman Mbowe heshima wala kudharau mchango wake binafsi katika kuongoza. Naomba nifafanue suala la mvuto. Freeman ameshafanya kazi kwa muda na ameifikisha Chadema hapo ilipo na kwa kushirikiana na viongozi wengine. Sasa gari liabidi liingie kwenye overdrive na ndio maana natamka kuwa ni bora kwa kuongeza kasi na nguvu, Mbowe ambaye ni more of a technocrat, aachie ngazi kama Mwenyekiti na awekeze nguvu zake bungeni na kwenye utungaji wa sheria na kumwachia Dr. Slaa ambaye si technocrat pekee bali ni pure politician mwenye uwezo wa kufanya yote mawili awe msimamizi wa kukiongoza chama kisiasa na kukijenga.
Rev. Kishoka,
Unachosema ni sahihi, lakini kuna historia watu wanaogopa isije jirudia kwao. Ni ile iliyomkuta Mapalala.
Kwa sababu Freeman amewezesha chama kuendelea kuwa stable katika mawimbi mazito, sio mbaya akindele kuongoza kikatiba ingawa kiutendaji anaweza kudelegate kazi nyingi kwa Slaa na wengine.
Katika politics za kiAfrika hakuna vyama vinavyoendeshwa ki-stable. Ni personality za watu ndio zinazokipa chama u-stable. Kama Freeman anaweza kuongoza chama, mpeni uenyekiti wa chama kisicho na personality na tuone matokeo yake. Mpeni TLP na awaleteeni viti 20 vya ubunge.
Kiongozi,
Kama hizo personalities ziko in-line with Mbowe, huoni kuwa tutakuwa tunaziweka kwenye test tukupresume kuwa zitakuwa in-line na Slaa. ninachoamini ni kwamba stability, hata kama basis yake siyo deep rooted, ikisimama kwa muda mrefu inakuwa tradition na ikisimama kwa muda mrefu zaidi inakuwa order. Hivyo basi, ni vyema Mbowe akaendelea kuwa mwenyekiti mpaka stability iliyopo ikawa ni tradition ya chama.
kama freeman asingekubali kuwa mwenyekiti wa chadema na angeendelea kuwa mbunge wa hai, nae angepata kuwalipua watu bungeni je umaharufu wake kisiasa ungekuwaje? je freeman angeendelea kuwa mbunge wa hai 2005 chadema kingefika hapa kilipo? hamna mtu ambaye anajua haya majibu.....Just a thought, kama Dr. Slaa asingegombea Urais, success ya Chadema ingekuwa kama ilivyo? If Chadema wangeng'ang'ania kuwa wao ni Bunge na kutoweka mtu mwenye wasifu kama Dr. Slaa, je matokeo yake yangekuwa sawa na ya leo?
Hata kama ni Ngeli na Ngali, lakini lazima tujiulize, ni vipi Dr. Slaa amekisaidia Chadema hususan wakati wa Uchaguzi au hata mchango wake tangu aingie Chadema kwa Chadema kupata mvuto na msukumo ulioko sasa hivi.
.
kama freeman asingekubali kuwa mwenyekiti wa chadema na angeendelea kuwa mbunge wa hai, nae angepata kuwalipua watu bungeni je umaharufu wake kisiasa ungekuwaje? je freeman angeendelea kuwa mbunge wa hai 2005 chadema kingefika hapa kilipo? hamna mtu ambaye anajua haya majibu.....
je slaa angegombea urais 2005 na freeman angeendelea kuwa mbunge wa hai, je chadema kingekuwa wapi na wao wawili wangekuwaje? no body knows
je malecela angeshinda urais, chama cha ccm kingekuwa better than sasa hivi? no body knows
je ronaldo asingecheza mechi ya juzi madrid wangeshinda? no body knows
kabla ya slaa kuchaguliwa kugombea urais watu wengi walikuwa wanasema slaa aendelee kuwa mbunge maana yake bado wanamuhitaji bungeni, walikuwa wanataka wabunge wachadema waongezeke na chama kijikite katika kuchukua nchi 2015.
chadema is a team na wote wanafanya kazi kama team chadema, na chadema ina katiba yake na jinsi ya kuteuwa viongozi. Na huwa wanateua mwenyekiti one year before the general election, na hii ni ample time kwa mtu atayechaguliwa kuweza kukipanga chama vizuri. Uenyekiti wa freeman sio wa milele una kikomo chake, Time ikifika wataangalia position zote na kuona nani afae kuwa mwenyekiti, katibu mkuu na position nyingine zote ndani ya chama.
lakini unavyotaka wewe watu watolewe kwenye uongozi sasa hivi bila kufata mpangilio ni sawa sawa na kuwatupia lawama baadhi ya watu wakati wapiga kura wenyewe bado mentality zao hazijabadilika.
chadema is a team, they win together they lose together.
Divisive politics must end, they do more to undermine chadema than the intended individuals
enoguh said
Semilong,
Upende usipende popularity ya Dr. Slaa ni moto chini. Tangu alipokuwa Bungeni na akiongea na hata kwenda MwembeYanga na kwingineko, anavutia watu na kama nzi kufuata harufu watu wanakwenda left and right.
Free, kakiokoa sana chama kwa kwanza kutumia fedha zake mwenyewe na huo ni utegemezi ambao inabidi uachwe. Narudia tena, kama Musa alivyowavusha Wakaguru kuvuka Sinai, sasa Dr. Slaa ni Joshua wa Wakaguru kuwafikisha watu Kaanani.
Chadema kina hitaji kiwe na safu kuu ya viongozi ambao ni full time viongozi na si part time. CCM wanaweza kufanya mambo part time kwa kuwa tayari wameshajijenga na wana mfumo mbovu wa mabavu na ndio maana hata maoni ya watu wanayapuuza na kukaa kama kamati maalumu kuvunjilia mbali mawoni ya wanachama na hata wananchi.
Moja ya mapendekezo yangu ya siku nyingi ni kwa Chadema kuondokana na mfumop wa kiuendeshaji na kiuongozi kama wa CCM, haya ya Halmashauri kuu, kamati kuu na upuuzi mwingine na kama ulimsikia Kikwete wakati wa kampeni, alidai kuwa wapinzani ni nakala na wao CCM ni irijino.
Chadema wakiweza kujiimarisha kwa kuwafikia wananchi kwa wingi kupitia full time Wanasiasa na kuboresha mfumo wao na kuondokana na ile structure ya ki-CCM, watafungua wigo mkubwa sana wa watu hata ndani ya CCM kuondoka na kwenda kweny chama chenye Demokrasia ya kweli.
Labda nitoe mfano wa Howard Dean ambaye aliwahi kugombea tiketi ya Democrats kugombea Urais wa Marekani. Alipopigwa ngwala, na John Kerry, akahamia na kuwa mwenyekiti wa Chama na kazi yake ikawa ni kuhamasisha Democrats na kuwavuta independents wakipigie kura na kukubali sera na itikadi za Democrats.
Hii ndio role ya sasa inayomfaa Dr. Slaa na Mbowe Zitto, Mnyika, Lissu na wengine ambao ni wabunge, focus yao iwe kuisambaratisha CCM Bungeni na huku nje kisiasa, Dr. Slaa awapeleke mputa mputa kina Msekwa na Makamba.
Lakini tukimtaka Mbowe afanye vyote, Mbunge, kiongozi wa upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa Chama on top of that bado ni Mfanyabiashara, there is no way he will be able to mutlitask efficiently and achieve sound results kila kona. Kuna sehemu atashindwa na kuzidiwa na demand ya kila upande itasababisha ashindwe kufanya vizuri. Si mnasema kiswahili mpenda vyote au mtaka vyote humponyoka?
So ninaposema mvuto, ni kuangali ani namna gani Dr. Slaa (ambaye kadhulumiwa kura milioni 3) ambavyo ameweza kuhamasisha Watanzania bila kujali Chama na watu kuanza kuona kuna tumaini jipya.
Same approach should be used to expand and reinforce the network and strength of Chadema na hilo lianze mapema na si late stage. Slaa apigane na Kikwete, Mbowe amkomalie Makinda na Pinda.
Slaa aende kwa Wazee wa Mikasi (Shein na Hamad) akakiuze Chadema kwa ngovu zote na kuhamasisha mvuto mpya kule wa kuonyesha chama cha umoja na si utengano kama CUF au kutenganisha watu kama CCM.
Kazi hii Freeman hawezi kuifanya bila kutolea kafara kimoja cha majukumu yake.
Aidha kuwa na mwenyekiti mpya na mwingine, kutaondoa zile desturi na tamaduni za migongano ambazo tumeziona zikiviandama vyama vingi vya kisiasa Tanzania na hata Afrika ambapo Nyerere alifanya kosa alipoamua kuunganisha Kofia mbili na kuzivisha kwenye kichwa kimoja katika ule mfumo wa kikomunisti au kijamaa ambapo Chama ni nguvu na si Serikali.
Nikiwa nimekaa chini kutafakari ni kwa nini katika nafasi 23 za Chadema za wabunge wa kuteuliwa hawakuteua wawakilishi kule Lindi, Mtwara, Ruvuma, Pemba, Tanga, Dodoma, Pwani, Tabora na kuongeza kule Iringa, Mbeya, Arusha, Rukwa na Mara, leo tunasikia kauli za chapati maji, kudai walinukuliwa isivyo kuhusu kutomtambua Kikwete kama Rais.
Hivyo swali langu kwenu wana Chadema, bado mnapingana nami kuwa hamuhitaji uongozi mpya ikiwa tayari kuna pande tatu zinavutana; Zitto, Freeman Mbowe na Dr. Slaa kwenye hili jambo moja la kuyakubali matokeo ya urais?
So take a minute again and think of what I was trying to relate to indirectly and assess the last 120 hours of life of Chadema!