CHADEMA mtumieni Jenerali Ulimwengu

Jenerali Ulimwengu ana kadi ya CCM ni mwanaCCM asilia ingawa ni mkosoaji mzuri wa sera za chama chake.

Kununua mapandikizi kwa maneno matamu ya mdomoni kunaweza kuingiza mamluki chadema.

Kama anaona CCM hakufai pamoja na sera zake anang'ang'ania nini huko?

Nani kakwambia CCM haifai kisera au kiitikadi? CCM ina itikadi nzuri na sera nzuri tu ila utekelezaji ni taabu kwa sababu ya maslahi binafsi kushika usukani kwenye kuendesha CCM. ndiyo maana watu kama Ulimwengu wapo wanakosoa ndani kwa ndani huku wakiwa na moyo kwamba CCM haina mbadala na mapambano yao ya kuielimisha CCM na kuuelimisha umma yataifanya CCM ifuate tena misingi yake.. Kazi ya ulimwengu haitaji kuwa kiongozi au mshauri wa chama chochote yeye kama mwanandishi na mwanaharakati anasema anachokiona na jamii inajifunza na kuamua mustakabali wa nchi..kadi yake ya kijani haikuhusu.
 
Hivi ule waraka wa Kikwete aliokua anauandika kwenye Raia Mwema bado unaendelea? Kwakua nilikua nausoma lakini sijui niliishia wapi kwakua ulikua ni waraka mrefu mno!
 
Mdondoaji na wengine,
Kuwa mshauri wa chama sio mpaka uwe na kadi, tujadili hoja iliyopo, habari za aliniambia kuwa anataka kujiunga CDM hazina mashiko hapa jamvini. Strike the point!
 
Mkuu Ndinani,
Habari za kupeana mawazo ya kuhusu namna kuendesha chama makini huwez uzifanya kwenye klabu za pombe ama kwenye vilinge vya soga( kahawa ). Mantiki ya uzi wangu ni kuwashauri CHADEMA wamuombe mzee Jenerali Ulimwengu awe mmoja wa washauri wa chama FORMAL not INFORMAL. Hata mimi huwa naonana na Mnyika kwenye canteen tunapokunywa chai na huwa ninamshauri mambo ya chama chao, lakini maudhui yake yatakuwa less concerned ukilinganisha na ushauri ambao ningetoa iwapo ningetambuliwa katika mfumo wa chama chao.
Jenerali Ulimwengu si mtu wa aina hiyo, ana uzito wa kipekee sana katika taifa letu Tanzania. Kwamba alikuwa knye system akaboronga si kweli, ninachofahamu ni kwamba the man was so strong kuwaambia ukweli majambazi na wanaotafuna Tanzania yetu bila huruma kwa kalamu yake na maneno yake amabayo yamemfanya awe mhanga hadi leo.
Ndiyo maana ninawashauri wakuu wa CHADEMA kulifikiria hili suala ikiwezakana wamuajiri kabsa kwa kazi hiyo kama walivyomuita Profesa Baregu, Jenerali deserves also!

Kwanza kama na yeye ana ona umuhimu wa kuchangia ktk mabadiliko ya hii nchi basi aingie CDM, awe mwanachama then atapata hiyo hadhi ya kuwa mshauri wa CDM formally...otherwise uanachama wa kubembelezwa na ahadi za kupeana kazi hauna mashiko wala mantiki yoyote. Sidhani kama Prof Baregu na Prof Safari walishawishiwa kujiunga CDM, naamini walijiunga kwa matashi yao wenyewe...
Pamoja sana!!!!
 
Jenerali Ulimwengu ana kadi ya CCM ni mwanaCCM asilia ingawa ni mkosoaji mzuri wa sera za chama chake.

Kununua mapandikizi kwa maneno matamu ya mdomoni kunaweza kuingiza mamluki chadema.

Kama anaona CCM hakufai pamoja na sera zake anang'ang'ania nini huko?

Kumbuka sio wote wenye Kadi ya CCM wana mapenzi ya dhati na CCM ila mfumo na mazingira yanalazimu wawe nazo ili maisha ya kila siku yasiwe na bugudha, umeshawahi jiuliza CDM wanapata wapi taarifa za ndani za CCM? umeshawahi jiuliza CDM wanatoa wapi nyaraka za serikali na za CCM ili hali zilikuwa za siri sama?

Haya yoote yanathibitisha kuwa watu wamechoka na mfumo wa CCM ila hawawezi kuondoka au kujitoa kirahisi kama udhaniavyo ndio maana wanagawa nyaraka na habari muhimu kwa CDM ili wafanikishe mchakato wa kuiweka CCM Pembeni
 
Tuacheni Ushabiki wana JF swala la kuomba busara haijalishi kama ni wa chama gani kwan alichosema 'Akelu' ni kuchota Hekima na Busara zake tu Jenerali huo Ugamba wake umetoka wapi mbona mahela ya SABODO tunapokea nae ni Mwana Gamba Pure nadhan umefika wakati cdm kupokea ushauri kutoka kwa watu wenye hekima bila kujali wanatoka upande upi wa chama
 
Back
Top Bottom