VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,007
Muwe mnaelewa. Mbunge au Diwani ahamie CCM. Harakaharaka uchaguzi mdogo uitishwe. Kuwe na makatazo tangu mwanzo kuhusu cha kuzungumza, wa kuzungumza na namna ya kupiga kura. Halafu mshinde nyinyi!?
Mikwara imiminwe. Wapigakura watishwe sirini na hadharani. Kanuni ziongezwe chumvi. Mkuu wa mkoa na wilaya wawe kwenye chumba cha kujumlisha kura katika jimbo au kata, mnashindaje hapo kwa mfano!? Labda muwe mabingwa wa mazingaombwe.
Kwa taarifa yenu, Mbunge au Diwani anahama na Jimbo au Kata yake kuja nayo CCM. Najua mnanuna lakini huo ndiyo ukweli. Kushiriki uchaguzi wenye kila aina ya uchafuzi ni kupoteza muda na rasilimali zenu. Kushinda haitawezekana!
Tume ya Taifa ya Uchaguzi inateuliwa na Mkuu wa Serikali. Wasimamizi wa uchaguzi kwenye Majimbo na Kata ni watumishi na wateuliwa wa Serikali. Rasilimali zitumikazo ni za Serikali. Serikali imeundwa na CCM. Mnashindaje!?
Piganieni kwanza Tume Huru ya Uchaguzi. Hakuna njia nyingine. Msiwe kama kenge, hadi damu itoke masikioni ndiyo asikie.Hata 2020, kushiriki katika uchaguzi kwa mfumo huu wa kiuchaguzi ni kupoteza muda. Hamtashinda hata mkiujaza uwanja!
Nabii Tito!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kakonko, Kigoma)