Zitto ana kauli za utata sana sijui kwa nini, yeye sidhani kama ni msemaji wa chama, na hata kama ni msemaji wa chama hakutakiwa azungumzie vile. Anyway kwa mazingira yaliyotokea nawapongeza wabunge wa chadema ambao wameonyesha kwa vitendo kuwa hawakubaliani na matokeo ya urais kama ambavyo mimi sikubaliani na matokeo hayo.
Dawa ni kukomaa mpaka kieleweke, na kudai katiba mpya ndiyo suluhu ya haya yote, vinginevyo wataendelea kudhulumu hivihivi!
Ninaamini CHADEMA hakuna mgawanyiko, ila mafisadi wanataka kupenyeza hisia zao zipate nafasi ndani ya chadema, na hawatapata nafasi hata kidogo. CHADEMA ni chama makini ambacho hakiwezi yumbishwa na chochote.