Gosbertgoodluck
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 2,856
- 401
Kumekuwepo na porojo mbalimbali kupitia kwenye vyombo uchwara vya habari kwamba chadema imegawanyika kutokana na kitendo chake cha kususia hotuba ya jk bungeni hivi karibuni. Porojo hizo ni mbinu ya kuvuruga 'move' nzuri iliyobuniwa na kutekelezwa na chadema ili kuleta mabadiliko makubwa kwenye uwanja wa siasa hapa nchini. Ninachowaomba viongozi wa chadema msikubali na msijaribu kukata tamaa. Hatua mliyochukua bungeni imeungwa mkono sana na wazalendo wa nchi hii. Endapo mngeandaa maandamano ya kuunga mkono ususiaji wenu wa hotuba ya jk, mngeamini hiki ninachosema. Wananchi wengi mitaani wanawasifu sana kwa ushujaa wenu huo. Tafadhali endelezeni mapambano. Wanaowapinga ni vibaraka wa mafisadi wanaonufaika na mianya ya ubovu wa katiba yetu na tume ya uchaguzi. Wananchi wengi ambao ndiyo wanyonge wapo nyuma yenu.