MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 10,205
- 22,249
Nawaamuru wafuasi wa CHADEMA msome kwa makini sana huu uzi na muufanyie kazi.
Hivi karibuni kama mmefuatilia mwenendo wa kisiasa hapa nchini inaonyesha CHADEMA (Chama cha Mbowe) hakina matatizo mengi sana na wala watu wengi hawana ubaya nacho. Na pia inaonekana CHADEMA hawana visasi na watu wanaotuhumiwa kuwaumiza miaka iliyopita. Nilishangaa kwenye tamko la Makonda kuhusu wanaomfuatilia kumuangamiza hakukuwepo na CHADEMA, viongozi wa upinzani au hata makada wa chama hiki cha Mbowe. Tuhuma za Makonda zote zimeelekezwa kwa watu wake wa chama chake kiasi kwamba akawa anakumbusha mazuri aliyowahi kuyafanya. Hata huko bungeni mbunge kibajaji amemlalamikia Zito kuhusu kauli zake dhidi ya hayati JPM pia kuwasuta wabunge wenzie wa CCM kwamba walikuwa wakimsifia wote JPM na wasijifanye kumkana.
Mimi nawashauri CHADEMA kutumia huu upepo vizuri kujijenga kisiasa kwa wananchi na kuachana na siasa zote zisizo na tija. Siasa za kipuuzi za kina Mdude ni za kuepukwa. Pia ingawa chama kipo taabani basi waendelee kumuamini Mbowe kama mwenyekiti. Mbowe ana busara na pia ana mtaji wa huruma za wananchi kwa aliyotendewa kwa miaka mingi. Alisimama imara na chama chake kilichoasisiwa na baba mkwe wake. Kingine ni chama kujitahidi kuwa na msemaji mmoja na kuachana na hii tabia mbaya ya kila mwanachadema kutoa tamko kiholela. Hicho chama kila mtu ni mwenezi wa chama. Pia chama kitengeneze hali ya kuwa na msimamo mmoja linapojitokeza jambo linalotaka wao kuonyesha msimamo wao. Kwa mfano sasa hivi kuhusu Ukraine na Urusi tunaona makada maarufu wakijitahidi kusema wanavyojua wao. Kada Yeriko anapambana kuripoti kutoka Moscow. Je CHADEMA inaunga mkono Urusi? Hadi sasa hivi hakuna kada maarufu wa CCM aliyesema chochote kuhusu hiyo vita maana ni suala zito la kidiplomasia. Siku mkipata dola mkamchagua Yeriko kuwa kiongozi italeta picha gani kwa Ukraine?
Nina mengi ya kuwashauri ila naishia hapa.