CHADEMA, msipite tu!

CHADEMA, msipite tu!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,007
Ni jambo jema la kisiasa kupita maeneo mbalimbali ya nchi kueneza chama na kusema chama husika kina nini kipya kwa watanzania. Kuonesha jinsi gani CHADEMA ni mbadala wa CCM-kama chama tawala ili ifikapo chaguzi za 2014 na 2015 CHADEMA ikabidhiwe uongozi wa nchi.

Kulikuwa na Operesheni Sangara hasa katika mikoa ya Kanda ya Ziwa (Mwanza,Shinyanga,Mara na Kagera). Kimsingi,Operesheni hii iliwaamsha wengi na kuimarisha chama katika sehemu husika. Ukweli wa hili ulithibitika hapo 2010 ambapo CHADEMA ilipata viti vingi vya Ubunge katika Kanda hiyo ukilinganisha na Kanda nyingine za nchi hii.

Baadaye,ikaja Operesheni ya: Vua Gamba,Vaa Gwanda. Hii ilitembea karibu Tanzania nzima. Na bado inaendelea. Ni Operesheni iliyosheheni ushawishi na kuhamisha wanachama wa vyama pinzani kwa CHADEMA na kuhamia humo (CHADEMA). Kuna mafanikio katika hili pia. Na sasa kuna Operesheni za Kikanda. Kanda zinazinduliwa na kuanza kazi. Ni jambo jema. Ni ubunifu uliotukuka na wenye kupigiwa mfano.Kisiasa,kukosolewa kwa jambo lolote ni sifa kuu ya siasa. Operesheni itakosolewa lakini pia itapongezwa.Cha muhimu ni kusonga nayo mbele kwa malengo yaliyowekwa.

Hata chama chetu cha CCM kinafanya siasa bunifu. CHADEMA,kama chama kikuu cha upinzani nchini, kinaimarika na kueneaTanzania. Ingawa mimi ni m-CCM,napenda siasa safi na za ushindani. Siku yaja ambapo watanzania watachagua wagombea kwa sera,uwezo na malengo yao.Si kwa kuangalia chama atokacho,rangi za bendera za chama,viongozi wake wala historia ya chama husika. Watachagua maendeleo. Na vyama vitasimamisha wanamaendeleo.Tanzania itapiga hatua kubwa kimaendeleo. Siku yaja upesi!

Lakini,CHADEMA msiishie kupita tu kila mkoa,wilaya,tarafa,kata,kitongoji/kijiji,mtaa,nyumba nahata kitanda kwa kitanda. Mnakopita,acheni alama ya uwepo wenu. Jengeni Ofisi.Ofisi,pamoja na kuwa kielelezo cha uwepo wenu hapo,itahamasisha wanachama,kukusanya wanachama wapya na kadhalika.Ofisi ndiyo kila kitu. Ujenzi wa matawi tu hautoshi. Mnaweza kuanza na ngazi za kimkoa,kiwilaya na kitarafa.Taratibu ndiyo mwendo.

Sijui kwanini leo ninawashauri na kuwasisitiza jambo hili ambalo chama changu hupatia ushindi wa kihoja kupitia humo.Hatahivyo, ni siasa kuimarisha siasa.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam.
 
Tunashukuru sana kwa ushauri safi, viongozi wetu ni makini sana na watapokea ushauri wako, nakusihi hata wewe achana ccm vaa gwanda maana huku ndiko kuna matumaini ya Tanzania tuitakayo.
 
Pamoja na hoja nzito naomba ujinasue na fikra kuwa Chadema ni chama cha upinzani. Chadema ni chama cha siasa kinachoelekea kuUnda serikali kwa ridhaa ya wapiga kura kwenye mazingira halali ya upigaji kura. Kwa sasa ni chama mbadala chenye upande mbadala Bungeni.

Neno chama cha upinzani ni turufu ya wajinga inayopandikizwa kwa wananchi kwa mtaji wa UJINGA. Tusubiri chama tawala cha sasa kitakapo kuwa hakipo madarakani msamiati utabadirika.
 
Katika hili VUTA-NIKUVUTE nakupongeza, kiukweli kumshauri mwenzako kuhusu mema hata kama mna itikadi tofauti ni hekima kubwa sana. UBARIKIWE NDUGU YANGU, nchi hii haitajengwa kkwa siasa za chuki na uhasama wa kuua raia wasio na hatia.
 
Point! Ila sina uhakika kama ni lazima kuiga mfumo wa ccm ili uwe chama bora.
Ni matumain yangu viongoz wa CDM watajibu ktk huu ushauri wako.

Sent from my BlackBerry 9780using JamiiForums
 
endeleeni kujipa moyo na kuishi kwa matumaini, ccm bado ipo sana kuongoza na kutawala nchi hii, ukweli mchungu.
 
njaa ya vuta nikuvute itamfikisha pabaya, hii ya kulialia na kuangukia miguu ya mabwana zake itamtafuna kwa muda mrefu sana
 
Ushauri wako ni nzuri HATAHIVYO Chadema hawana lengo la kudumu, wameshindwa kuweka ofisi Imara wilaya za Ilala na Temeke, itakuwa vigumu kuweka ofisi Tandahimba!!!!
 
Back
Top Bottom