HISIA KALI
JF-Expert Member
- Oct 26, 2010
- 694
- 109
mbunge mwigulu nchemba akiwa mjini sumbawanga alisema kuwa sera za chama cha demokrasia na maendeleo ni za kukubaliana na ushoga na hata kauli mbiu yao ya sasa ya movement for change ni mabadiliko toka hali ya sasa ya jinsi ya kiume kuoa ya kike na kukubaliana na ushoga.
Hivi kauli za namna hii ni za mtu kabisa ambaye ni kiongozi au ni za muuza mitumba aliyevuta bagi? Ametoa kauli hii akiwepo katibu mwenezi nape nnauye na viongozi wengine wa ccm na hakuna aliyekanusha.
Kauli ,za namna hii zinzashiria nini nje ya muuonekano wa ccm?
kama kasema hivyo basi itakuwa ni miongoni wa kauli zinazotolewa na viongozi wa siasa wanadhani kuwa wananchi wa tanzania hawana akili ya kutosha kuchambua mambo. Hivi kweli hata kama chadema ina urafiki wa kisiasa na chama kinachotawala uingereza basi ina maana chadema inaendesha sera za chama hicho hapa tanzania.
Kwanza sera ya ushoga sio sera ya chama cha kinachotawala uingereza bali ni sera ya nchi ya uingereza kuwa ujumla na pia sera hii ipo kwenye nchi nyingine nyingi tu za ulaya na marekani ambazo serikali ya tanzania inashirikiana nazo kwenye mambo mbali mbali ikiwemo kupata misaada ya kifedha.
Ni jambo la kawaida kwa mtu hasiyekunywa pombe kuwa na marafiki wanaokunywa pombe. Hili halimfanyi na yeye kunywa pombe.
Hata hapa Tanzania sasa hivi kuwa mashoga (ndio maana kuna mjadala wa kuhalalisha ushoga au la) na wana marafiki wa kawaida ambao sio mashoga.