Chadema Moshi mjini (MH.Ndesamburo)

Mr Mayunga

JF-Expert Member
Jun 11, 2011
313
40
Mheshimiwa tunaomba utusaidie sana,ajira ni tatizo kubwa hapa moshi mjini kwa mawazo haya tatizo lingeweza kupungua.Tufufuliwe viwanda vilivyokufa hapa Moshi,kama kile cha Magogo,Magunia N.k.Nasema viwanda kwasababu ni sekta ambayo inaouwezo wakuajiri watu wengi mno.
 
Si ni mbunge wako? Mwendee nyumbani kwake usitujazie server kwa post zisizo na tija.
Besides, tatizo la ajira ni la kitaifa ulipaswa umwambie Mkw€re sio Ndesa Pesa
 
ungepost jukwaa la ajira nahisi ingesadia sana, hata hivyo sijajua kama Ndesambulo ni member wa JF
 
Mheshimiwa tunaomba utusaidie sana,ajira ni tatizo kubwa hapa moshi mjini kwa mawazo haya tatizo lingeweza kupungua.Tufufuliwe viwanda vilivyokufa hapa Moshi,kama kile cha Magogo,Magunia N.k.Nasema viwanda kwasababu ni sekta ambayo inaouwezo wakuajiri watu wengi mno.
Kwani viwanda ulivyovitaja hapa vilikuwa vinamilikiwa na Ndesa Pesa?
 
Mheshimiwa tunaomba utusaidie sana,ajira ni tatizo kubwa hapa moshi mjini kwa mawazo haya tatizo lingeweza kupungua.Tufufuliwe viwanda vilivyokufa hapa Moshi,kama kile cha Magogo,Magunia N.k.Nasema viwanda kwasababu ni sekta ambayo inaouwezo wakuajiri watu wengi mno.

Hiyo ni issue ya kitaifa,mlaumu Rais wako kilaza
 
Halafu umefungua thread kuhusu Mbowe atengeneze ajira HAI sasa umekuja na hii unataka ni dogo!
 
Mzee Ndesa ametoa mchango mkubwa sana kwenye ajira. Kama sio biashara zake za utalii watu wengi wasingekuwa na ajira. Na mara nyingi ametaka kutoa michango mikubwa zaidi lakini serikali imekuwa inamzuuia kufanya hivyo. Kwa mfano soko la kiborloni lilikufa pale alipotaka kulijenga liwe la kisasa, lakini mkuregenzi akasema eneo hilo ni la viwanda! Wafanyabiashara wakaondolewa na kupelekwa Memorial leo hii Kiborloni hakuna cha soko wala Kiwanda. Ni vizuri tujue chanzo cha matatizo yetu ni serikali ya ccm.
 
c/o Angel msoffe: mzee ndesa alishaomba kibali tn bungeni apewe ruhusa ya kufufua kiwanda cha magunia kwa pesa yk serikali ikamkatalia, ila MOSHI SI HABA MZEE KAJITAHIDI SANA.
 
Halafu umefungua thread kuhusu Mbowe atengeneze ajira HAI sasa umekuja na hii unataka ni dogo!
Hahahahaaaa unamuita dogo waweza kuta mzee masawe......!!!!
Halafu wachaga ni wajanja ye anasubiri ajira ya Ndesa au JK??? Atangoja milele
 
Ndesa aliomba kiwanda cha general tire wakamnyima kiwanda mpaka leo hii lonakaribia kua ghala la kuhifadhia bidhaa feki kutoka china.ndesa pesa ni kati ya wafanyabiashara wazalendo sema serikali muflisi ya sisiemu huwa haitaki wazawa kuwa wamiliki wa raslimali za nchi yao,wao wadosi tu na waarabu.ndesa iko pesa alafu ni kichwa pia.
 
c/o Angel msoffe: mzee ndesa alishaomba kibali tn bungeni apewe ruhusa ya kufufua kiwanda cha magunia kwa pesa yk serikali ikamkatalia, ila MOSHI SI HABA MZEE KAJITAHIDI SANA.

Sehemu kubwa ya wachaga ni wafanyabiashara ukitaka uisaidie hii jamii ni kuwawezesha kimikopo
 
Mheshimiwa tunaomba utusaidie sana,ajira ni tatizo kubwa hapa moshi mjini kwa mawazo haya tatizo lingeweza kupungua.Tufufuliwe viwanda vilivyokufa hapa Moshi,kama kile cha Magogo,Magunia N.k.Nasema viwanda kwasababu ni sekta ambayo inaouwezo wakuajiri watu wengi mno.

Hii ni kazi ya Serikali ya Kuu na siyo kazi ya Mbunge!
 
Sasa mbona Lema alisema wakati wa kampeni akichaguliwa kuwa mbunge wa Arusha mjini, atajenga Machinga Complex mbili pamoja na Barabara za juu
 
Ndesamburo kama mbunge alishatimiza wajibu wake siku nyingi;alishaomba serikali iwape watu binafsi viwanda vya Machine tools,magunia n.k wavifufue ili viweze kutoa fursa mbali mbali kwa watu wahayo maeneo na Tanzania kwa ujumla lakini serikali yetu imeamua kutia pamba masikioni.Ball is in our court now,kutumia kura zetu vizuri kwa manufaa ya wote na vizazi vijavyo
 
Sasa mbona Lema alisema wakati wa kampeni akichaguliwa kuwa mbunge wa Arusha mjini, atajenga Machinga Complex mbili pamoja na Barabara za juu
Lema amekuwa mbunge kwa kipindi cha mwaka mmoja mpaka sasa kama ni ahadi ni vizuri tukaanza na alizotoa JK miaka sita iliyopita (tangu 2005)
 
Mayunga bwana! Hukubahatika kwenye zile ajira milioni moja za Jk? Mbona Mzee ndesa hakutangaza ajira? Chukua jembe ukapalilie mikahawa na migomba kule kibosho inalipa kwa siku ni 5000/= mara 30 ni 150,000/= sawa na kima cha chini cha mshahara.
 
Back
Top Bottom