CHADEMA (Moshi) kurudisha Mali za Halmashauri toka Mikono ya CCM?

mzambia

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
885
60
MBUNGE wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo (Chadema) amesema wiki hii itakuwa ya kihistoria wakati Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, litakapopitisha azimio la kurejesha mali za umma, zilizoporwa na CCM.
Alitaja mali hizo kuwa ni pamoja na kiwanja chenye hati namba 056038/94 chenye ofisi za CCM Moshi Mjini na eneo la hekari 2.7 lenye hati namba 15686 la Umoja wa Vijana wa Chama Chama Mapinduzi (UVCCM) mkoani Kilimanjaro.Ndesamburo aliwaambia waandishi wa habari jana mjini Moshi kuwa, wamefanya upekuzi wa kisheria katika ofisi ya msajili wa hati katika kanda ya kaskazini na kuthibitisha kuwa viwanja hivyo bado vipo kwa jina la halmashauri.

Mbunge huyo alisema Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo lenye madiwani 24 wa Chadema na watano wa CCM, litapitisha uamuzi huo Alhamisi wiki hii.Alisema maamuzi hayo ni magumu lakini yana maslahi ya umma.Ndesamburo alisema uamuzi wa halmashauri kuipa CCM mali hizo za umma, ulifanywa na madiwani wa chama hicho tawala, huku wakifahamu kuwa zilikuwa ni za wananchi wote bila kujali itikadi za vyama vyao.

"Haiingii akilini watu wachache wanakaa na kuamua kuipa CCM mali zinazomilikiwa na wananchi wote,"alisisitiza Ndesamburo.Mbunge huyo alifafanua kuwa mali ya umma haiuzwi kupitia utaratibu wa madiwani kupiga kura na badala yake kwa kutangaza zabuni ili Watanzania wote washiriki katika kununua.

Ndesamburo alisema badala yake, madiwani wa CCM kwa kutumia wingi wao, waliamua kuwa wao ndio walalamikaji na mahakimu na hatimaye kujipatia mali hizo, jambo ambalo halikubaliki

Mbunge huyo alisema Watu wote wanaokaa au kutumia mali zilizopo katika viwanja hivyo, watalazimika kuingia mikataba upya na halmashauri na hata kama CCM watakubali kugeuka kuwa wapangaji hiyo ni ruksa.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, Bernadette Kinabo alipoulizwa, kuhusu azimio hilo, alisema hoja hiyo ni mfu na kwamba mali hizo zinamilikiwa kihalali na CCM."Hili jambo halina uhusiano na sheria ya manunuzi ya umma wala zabuni kwa sababu linahusu ardhi lilipelekwa kamati ya mipango miji na baadaye likapata baraka za madiwani wa wakati huo kwa hiyo ni halali kisheria,"alisema Kinabo.

Kinabo alisema kama suala ni sheria ya manunuzi ya umma au ya zabuni kukiukwa, inakuwaje madiwani hao wanalipeleka katika Baraza lao ambalo lina nguvu ya kisheria kama lile lililopitisha maamuzi hayo.

Viongozi wa CCM akiwemo Mwenyekiti wa Manispaa ya Moshi, Godfrey Mwangamilo, wamekaririwa wakisema viwanja hivyo na mali zilizomo ndani yake ni za CCM na taasisi ya zake.
 
Fanyeni lililo sahihi,hata kama serikali (ccm) itatishia kuvunja halmashauri ni vyema mkawaonesha wana nchi kwamba mmewatetea hadi mwisho,...
 
Nina hamu kuona viwanja vya CCM Kirumba na kile cha Ali Hassani Mwinyi pale Tabora vinarudi kwa TFF kwa vile niliweka jasho langu kubeba matofari tukiwa tunajitolea kama raia wa kawaida halafu leo tunaambiwa eti ni viwanja hivyo ni mali ya CCM.
 
baada ya huko twende tukarudishe ccm kirumba kwani ulijengwa kwa pesa za walipa kodi na sio michango ya wanaccm pekee.........
 
kunavitu vingi ccm imejilimbikizia mf shure za wazazi tumejenga kwanguvu yawa tz wamezibali kuwamali za uwz ccm mapato na matumizi havieleweki
 
Nina hamu kuona viwanja vya CCM Kirumba na kile cha Ali Hassani Mwinyi pale Tabora vinarudi kwa TFF kwa vile niliweka jasho langu kubeba matofari tukiwa tunajitolea kama raia wa kawaida halafu leo tunaambiwa eti ni viwanja hivyo ni mali ya CCM.

hahaha mkuu umenikumbsha mbali sana ..kumbe ulibeba matofali kama mimi kwenye uwanja wa ululukule lindi miaka hiyo
 
Nakumbuka enzi hizo nikiwa mtoto mdogo mgambo na polisi walikuwa wakikamata meza,viti, hata mifugo kama kuku kwa wananchi wanaoshindwa kuchanga kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu kama hii nyumba na viwanja kwa mfano hizi za vijana, lakini gafla baada mfumo wa vyama vingi kurudishwa mali zote zikawa za ccm bila kujali waliozichangia hawakuwa wanachama/ au kuwa na itikadi au la!
 
Vipi Viongozi wote wastaafu wa CCM kupewa Viwanja vya Kujenga Maeneo Ambayo yalikuwa yanamilikiwa na Wananchi?
Majengo kama CCM Lumumba CCM ilipewa bila kulipia Kodi kwa NHC
 
hoja ya nguvu japo subject haijakaa sawa, badala ya chadema ungesema "nguvu ya umma".

Hivi hawa ccm eti viwanja vyote vya wazi ni vyao, kama kumilikishwa vimilikishwe vyama vyote vya siasa kwa usawa au wapangishwe kupitia NHC.
 
Back
Top Bottom