CHADEMA mnatuchanganya

CHADEMA mnatuchanganya

Mbuzimtu

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2013
Posts
355
Reaction score
178
Ninawashangaa sana chadema kuona wanavyo lichanganya taifa hili.
Kwanza,
1. Wamekuwa na misimamo isiyo yumba mara zote wanapoamua kufanya mabo yao. Hii inasababisha hata uendeshaji wa serikali unakuwa mgumu. Mfano, Tangu wameanza kuwaelimisha wananchi mambo mbali mbali ya kisiasa na kisheria, watu wamekuwa wakihoji kila kitu. Tatizo ni chadema kiherehere chao kuwaelimisha wananchi na misimamo yao mikali

2. Chadema wameanzisha tabia ya kutoka bungeni mara zote wanapoona kuwa mambo yanayofanyika ni kinyume na sheria au ni kinyume na matakwa ya watanzania. Walianza 2010 wakati wa hotuba ya rais Kikwete na juzi tu wamesusa bunge la katiba. Mbaya zaid ni pale walipowambukiza na CUFna NCCR mageuzi. Hili nalo limezidi kuwa tatizo nchini na linakwamisha utekerezaji wa mipango ya chama tawala na serikali yake. Sio lazima kuwasikiliza wananchi kwenye mambo nyeti kama katiba kwani wanaweza kuharibu upatikanaji wa katiba inayotekerezeka.

3.Chadema wamejenga utamaduni wa kuhoji kila kitu cha serikali. Mfano, kila mara serikali inapoingia mikataba na makampuni au nch furani wao wanataka wananchi wajue. Huwa najiuliza ili iweje?. Sio lazima wananchi wajue kwani wanajua nini kuhusu mikataba?

Chadema badilikeni. Msitupereke putaputa wakati sisi tuko kizazi cha zamani
 
Sikukuu imekulewesha nini mkuu hakunaga chadema tena siku hizi mkuu
 
Chadema wamefanya mpaka kikwete akatawala na kuongoza vibaya. Mfano, kama siyo chadema mchakato wa katiba usingeanza. Sasahivi wameanza kumbana rais, yaani chadema wanaongoza nchi kiaina. siwapendi!
 
Ninawashangaa sana chadema kuona wanavyo lichanganya taifa hili.
Kwanza,
1. Wamekuwa na misimamo isiyo yumba mara zote wanapoamua kufanya mabo yao. Hii inasababisha hata uendeshaji wa serikali unakuwa mgumu. Mfano, Tangu wameanza kuwaelimisha wananchi mambo mbali mbali ya kisiasa na kisheria, watu wamekuwa wakihoji kila kitu. Tatizo ni chadema kiherehere chao kuwaelimisha wananchi na misimamo yao mikali

2. Chadema wameanzisha tabia ya kutoka bungeni mara zote wanapoona kuwa mambo yanayofanyika ni kinyume na sheria au ni kinyume na matakwa ya watanzania. Walianza 2010 wakati wa hotuba ya rais Kikwete na juzi tu wamesusa bunge la katiba. Mbaya zaid ni pale walipowambukiza na CUFna NCCR mageuzi. Hili nalo limezidi kuwa tatizo nchini na linakwamisha utekerezaji wa mipango ya chama tawala na serikali yake. Sio lazima kuwasikiliza wananchi kwenye mambo nyeti kama katiba kwani wanaweza kuharibu upatikanaji wa katiba inayotekerezeka.

3.Chadema wamejenga utamaduni wa kuhoji kila kitu cha serikali. Mfano, kila mara serikali inapoingia mikataba na makampuni au nch furani wao wanataka wananchi wajue. Huwa najiuliza ili iweje?. Sio lazima wananchi wajue kwani wanajua nini kuhusu mikataba?

Chadema badilikeni. Msitupereke putaputa wakati sisi tuko kizazi cha zamani

@Mbuzimtu

Haya mkuu. Tumekusoma kwa hii aina yako ya presentation...tusonge mbele pamoja daima kwa ajili ya wananchi na nchi yetu sote.
 
Tabia hii wasijekuambukiza watoto tu, huku nyumbani hakutatosha aisee, sababu ukilewa tu unasikia watoto wanaanza kuhoji kuhusu utimizaji wa wajibu wako.
 
Mkuu, tayari watoto washaharibiwa. leo watoto wanajua ukweli na maigizo.
Jambo ambalo lilinikera ni siku moja Lissu akitoa hotuba Bungeni, Mwanangu akasema Duddy, Lissu deserve to be the President of Tanzania not.............
Nikajiuliza kwa kweli taifa limeingiliwa, Mpaka watoto wanajua pointi ni ipi na pumba ziko wapi!. Hii ni hatari sana. Serikali iko makini kufanya ionavyo kuwa inafaa, sisi wananchi kazi yetu ni kusikiliza na kuwachagua viongozi wakati ukifika. Tuungane kuwaonya chadema wasihoji kila kitu.
 
Unachokisema kina mantiki kubwa sana, na tayari nimeona Clouds TV nao wameliona hili na kuanza kukanya wananchi, Aina ya siasa zinazofanywa na CHADEMA zinapaswa kupingwa na kila mwananchi anayelitakia mema Taifa letu, wakiachiwa namna hii Taifa linaweza kuingia kwenye machafuko wakati ndio Taifa la kupigiwa mfano duniani kote kwa amani,utulivu,utiifu na kuenzi viongozi wake, vitu vinavyovutia wawekezaji na misaada kutoka nje ya nchi.

Haiwezekani watu wote tukashiriki kwenye uongozi wa Taifa,kama ulivyosema,tukiishatimiza wajibu wetu wa kupiga kura tunapaswa kukiachia chama tawala kutimiza wajibu wake wa kulinda taifa,kuleta maendeleo na kuimarisha amani,utulivu na udugu miongoni mwetu.

wananchi tusikubali kuvurugwa,
 
Hahahah hahaha hahaha Mbuzimtu tafadhali, mtendee haki mtoto wako. Malizia kile alichokisema. La sivyo mkabidhi hicho kitendea kazi unachokitumia kuandikia maana kitakuwa kinamstahili yeye kuliko baba anayesita kumalizia sentensi nzuri ya ujasiri iliyotolewa na mwana.

What a light touch...
 
Last edited by a moderator:
Ninawashangaa sana chadema kuona wanavyo lichanganya taifa hili.
Kwanza,
1. Wamekuwa na misimamo isiyo yumba mara zote wanapoamua kufanya mabo yao. Hii inasababisha hata uendeshaji wa serikali unakuwa mgumu. Mfano, Tangu wameanza kuwaelimisha wananchi mambo mbali mbali ya kisiasa na kisheria, watu wamekuwa wakihoji kila kitu. Tatizo ni chadema kiherehere chao kuwaelimisha wananchi na misimamo yao mikali

2. Chadema wameanzisha tabia ya kutoka bungeni mara zote wanapoona kuwa mambo yanayofanyika ni kinyume na sheria au ni kinyume na matakwa ya watanzania. Walianza 2010 wakati wa hotuba ya rais Kikwete na juzi tu wamesusa bunge la katiba. Mbaya zaid ni pale walipowambukiza na CUFna NCCR mageuzi. Hili nalo limezidi kuwa tatizo nchini na linakwamisha utekerezaji wa mipango ya chama tawala na serikali yake. Sio lazima kuwasikiliza wananchi kwenye mambo nyeti kama katiba kwani wanaweza kuharibu upatikanaji wa katiba inayotekerezeka.

3.Chadema wamejenga utamaduni wa kuhoji kila kitu cha serikali. Mfano, kila mara serikali inapoingia mikataba na makampuni au nch furani wao wanataka wananchi wajue. Huwa najiuliza ili iweje?. Sio lazima wananchi wajue kwani wanajua nini kuhusu mikataba?

Chadema badilikeni. Msitupereke putaputa wakati sisi tuko kizazi cha zamani

maneno hayo kawaambie wasiotaka muelimika
 
Jk mwenyewe anaitambua vema cdm na mziki wake.

Hata kama anaitambua, lakini sio namna hii.

Chadema imekuwa kikwazo kwenye maeneo mengi sana, Imewavuruga wananchi kiasi cha kufikia kuzomea viongozi wao, tena mpaka viongozi wa kitafa.

Juzi niko barazani nadowea uji wa futari, wazee wasiokuwa na elimu, ambao hawajawahi kuwa na nafasi yoyote ile ya uongozi wa katika taifa letu nao wanahoji kwa nini hati ya Muungano haikupelekwa umoja wa Mataifa kama ni kweli uliridhiwa na serikali ya zanzibari.

Hawa watu wakiachiwa wataipasua hii nchi vipande vipande.

Viongozi wa ccm waliopo sasa ni wastaarabu,wapole,wang'avu.ni wasafi wa mioyo na smart wanaojua kupangalia mambo yao kuanzia kwenye uvaaji mpaka ujengaji wa hoja na wengi ni wasomi wa hali juu, kulinganisha na chadema wanaong'ang'aniza moja jumlisha moja iwe tatu badala ya mbili
 
Unachokisema kina mantiki kubwa sana, na tayari nimeona Clouds TV nao wameliona hili na kuanza kukanya wananchi, Aina ya siasa zinazofanywa na CHADEMA zinapaswa kupingwa na kila mwananchi anayelitakia mema Taifa letu, wakiachiwa namna hii Taifa linaweza kuingia kwenye machafuko wakati ndio Taifa la kupigiwa mfano duniani kote kwa amani,utulivu,utiifu na kuenzi viongozi wake, vitu vinavyovutia wawekezaji na misaada kutoka nje ya nchi.

Haiwezekani watu wote tukashiriki kwenye uongozi wa Taifa,kama ulivyosema,tukiishatimiza wajibu wetu wa kupiga kura tunapaswa kukiachia chama tawala kutimiza wajibu wake wa kulinda taifa,kuleta maendeleo na kuimarisha amani,utulivu na udugu miongoni mwetu.

wananchi tusikubali kuvurugwa,

Jitahidi kuandika huku ukitumia akili yako vizuri na ebu tafakari juu ya hizi picha hapa chini.

arusha1.jpg
Damu hii pale Soweto Arusha waliimwaga CDM?
View attachment 174062
Mwenyekiti huyu wa CDM pale Usariver alichinjwa na CDM?
darasa.jpg
Ubovu wa shule hii ni sababu ya CDM?

Kiwia a5.jpg
Wabunge hawa wa pale Mwanza walipigwa na wanaCHADEMA?
 
Hata kama anaitambua, lakini sio namna hii.

Chadema imekuwa kikwazo kwenye maeneo mengi sana, Imewavuruga wananchi kiasi cha kufikia kuzomea viongozi wao, tena mpaka viongozi wa kitafa.

Juzi niko barazani nadowea uji wa futari, wazee wasiokuwa na elimu, ambao hawajawahi kuwa na nafasi yoyote ile ya uongozi wa katika taifa letu nao wanahoji kwa nini hati ya Muungano haikupelekwa umoja wa Mataifa kama ni kweli uliridhiwa na serikali ya zanzibari.

Hawa watu wakiachiwa wataipasua hii nchi vipande vipande.

Viongozi wa ccm waliopo sasa ni wastaarabu,wapole,wang'avu.ni wasafi wa mioyo na smart wanaojua kupangalia mambo yao kuanzia kwenye uvaaji mpaka ujengaji wa hoja na wengi ni wasomi wa hali juu, kulinganisha na chadema wanaong'ang'aniza moja jumlisha moja iwe tatu badala ya mbili

yani inavyo onyesha wewe jamaa unaweza kukuta kundi la watu wakiongea habari nyeti zinazo kuhusu'. harafu wewe kwa haraka zako ukaaza tu kuunga mkono hoja bila kujua kama ulikua unasemwa mwenyewe.
 
Hata kama anaitambua, lakini sio namna hii.

Chadema imekuwa kikwazo kwenye maeneo mengi sana, Imewavuruga wananchi kiasi cha kufikia kuzomea viongozi wao, tena mpaka viongozi wa kitafa.

Juzi niko barazani nadowea uji wa futari, wazee wasiokuwa na elimu, ambao hawajawahi kuwa na nafasi yoyote ile ya uongozi wa katika taifa letu nao wanahoji kwa nini hati ya Muungano haikupelekwa umoja wa Mataifa kama ni kweli uliridhiwa na serikali ya zanzibari.

Hawa watu wakiachiwa wataipasua hii nchi vipande vipande.

Viongozi wa ccm waliopo sasa ni wastaarabu,wapole,wang'avu.ni wasafi wa mioyo na smart wanaojua kupangalia mambo yao kuanzia kwenye uvaaji mpaka ujengaji wa hoja na wengi ni wasomi wa hali juu, kulinganisha na chadema wanaong'ang'aniza moja jumlisha moja iwe tatu badala ya mbili

Ujue wasingekuwa chadema sisi tungekuwa tushabadilisha mpaka jina la nchi yetu. Misaada mingi inaletwa na wafadhili wengine wanataka kununua mpaka nchi nzima sisi tuwe wazungu. kikwazo chadema wanaihoji sana serikali. Nadhani chadema isingekuwepo, inawezekana sisi sote tungeshauzwa!.Chadema badilikeni!. Mnawafanya viongozi wanashindwa kufanya wayatakayo.
 
Hahahah hahaha hahaha Mbuzimtu tafadhali, mtendee haki mtoto wako. Malizia kile alichokisema. La sivyo mkabidhi hicho kitendea kazi unachokitumia kuandikia maana kitakuwa kinamstahili yeye kuliko baba anayesita kumalizia sentensi nzuri ya ujasiri iliyotolewa na mwana.

What a light touch...

Makene, Mwanangu siyo mzuri!. Anamswali mengi kweli. Hadanganyiki!. Sasa wewe unashindwa kuelewa hapo tena!. Au ndo kina sisi ambao chadema imeshindwa kutuharibu fahamu zetu
 
Hata kama anaitambua, lakini sio namna hii.

Chadema imekuwa kikwazo kwenye maeneo mengi sana, Imewavuruga wananchi kiasi cha kufikia kuzomea viongozi wao, tena mpaka viongozi wa kitafa.

Juzi niko barazani nadowea uji wa futari, wazee wasiokuwa na elimu, ambao hawajawahi kuwa na nafasi yoyote ile ya uongozi wa katika taifa letu nao wanahoji kwa nini hati ya Muungano haikupelekwa umoja wa Mataifa kama ni kweli uliridhiwa na serikali ya zanzibari.

Hawa watu wakiachiwa wataipasua hii nchi vipande vipande.

Viongozi wa ccm waliopo sasa ni wastaarabu,wapole,wang'avu.ni wasafi wa mioyo na smart wanaojua kupangalia mambo yao kuanzia kwenye uvaaji mpaka ujengaji wa hoja na wengi ni wasomi wa hali juu, kulinganisha na chadema wanaong'ang'aniza moja jumlisha moja iwe tatu badala ya mbili
Duh we jamaa utakuwa mtupu kabisa kichwani yaani null set haya nenda lumumba ukachukue buku saba zako we mjinga
 
Seriously mkuu! Nilitarajia point ya maana! Lakini sorry weak supporting arguments!
 
Back
Top Bottom