CHADEMA mnafahamu mnachokidai | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA mnafahamu mnachokidai

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by rodrick alexander, Jul 24, 2012.

 1. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #1
  Jul 24, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,109
  Likes Received: 1,499
  Trophy Points: 280
  [FONT=&amp]chadema mnafahamu mnachokidai[/FONT]

  N[FONT=&amp]nimekuwa nikifatilia kwa makini siasa za tanzania na hasa vyama viwili chadema na ccm.nimekuwa nikikifatilia ccm kama tawala na chadema kama chama mbadala wengi tumezungumzia mapungufu ya chama tawala ambayo yanaonekana waziwazi na mpaka sasa wamekuwa na kigugumizi kuyarekebisha lakini hatuwezi kuwazungumzia chama tawala bila kuangalia na chama ambacho kinaweza kuwa mbadala wake.[/FONT] [FONT=&amp]moja ya mambo yanayowakera wananchi wengi na hasa walipa kodi ni ukubwa wa serikali kiasi cha kufikiri nafasi nyingine zimewekwa ili kulipa fadhila.

  ukubwa huo umezidi kuwapa mzigo wananchi wa kawaida yaani walipa kodi.bahati nzuri chadema wameliona na wamelipigia sana kelele iwe kwenye majukwa ya siasa na hata bungeni kwenye hotuba zao na hata kwenye ilani yao ya uchaguzi wamezungumzia haja ya kupunguzwa ukubwa wa serikali.[/FONT]

  [FONT=&amp]jambo jingine ambalo limezua mjadala na hasa kuwa kero ni suala la muungano.wapo wanaopendekeza muundo wa muungano uwe serikali moja,wengine tatu wengine tubaki na muundo tulionao na wengine wameenda mbali zaidi kufikiria kwa sasa hivi hakuna haja ya muungano bora uvunjike.kwa bahati nzuri chadema nao wameweka msimamo wao ni kutaka tuwe na serikali tatu yaani serikali ya tanganyika ,zanzibar na serikali ya muungano.[/FONT]

  [FONT=&amp]bahati nzuri haya maswala yalisha jadiliwa kipindi cha nyuma juu ya muundo wa muungano.wakati tunaungana zanzibar iliachiwa kwa makusudi iwe na serikali yake ili isipoteze uasili wake na pia ilionekana itakuwa ni mzigo mzito kwa wananchi wa tanganyika kuhudumia serikali ya tanganyika na muungano tofauti na zanzibar ambayo ukubwa wake ni sawa na mkoa au baadhi ya wilaya za bara watanganyika watakamuliwa zaidi kugharamia serikali yao na serikali ya muungano.[/FONT] [FONT=&amp]

  swali langu kwa chadema wakati wanapigia kelele juu ya ukubwa wa serikali hawaoni kuwa na serikali tatu ni kuwabebesha mzigo wananchi wa tanganyika kwani watabeba gharama zaidi kuwahudumia{serikali ya tanganyika} rais wa tanganyika mawaziri wake pia kuwahudumia {serikali ya muungano}rais wa muungano na mawazir wake na bado wastaafu kwani juzijuzi tu tumejulishwa viongozi wastaafu wametengewa bilioni 9 kwa ajili ya matibabu.[/FONT]
   
 2. H

  Honolulu JF-Expert Member

  #2
  Jul 24, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 5,654
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  [​IMG]

  Hivi ndivyo CCM iliovyowafanya watanzania!
  Watahakikisha watanzania hamkai!
  Mnabaki mmesimama! Mkikaa mtaelewana!
  Lazima mbaki mmesimama ili mgombane vizuri!
  Ccm watahakikisha hata mijadala yenu inahusu umbeya na udini!
  Wakati mnahangaika na umbeya na udini
  wateule wachache wanaishi maisha ya paradiso kwa raslimali zenu!

  Na hili ndilo ninaloliona hapa kwa hawa wanaojiita Great Thinkers. Ukifuatikia mijadala mingi hapa utakuta ni kuhusu issue za watu binafsi zilizojaa umbeya mtupu. Ni lini tutaweka hapa mijadala motomoto yenye maslahi ya taifa?
   
 3. r

  richone Senior Member

  #3
  Jul 24, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 146
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  tuambie tupiganie nini
   
 4. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #4
  Jul 24, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Ina maana huajaielewa hiyo thread? mbona iko wazi? Hongera sana mleta tthread, kweli umewashika pabaya vilaza.
   
 5. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #5
  Jul 24, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Hakutakuwa na gharama yoyote katika serikali tatu endapo CDM itaingia madarakani kwa vile uongozi wanapeana kindugu. Mbowe atakuwa Rais wa Tanganyika, Slaa atakuwa Rais wa Zanzibar, Ndesamburo atakuwa Rais wa Tanzania Josephine Mshumbuzi atakuwa waziri mkuu, Lucy Owenya atakuwa makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar , Lissu na dada yake watakuwa wanasheria wa Serikali zote tatu.
   
 6. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #6
  Jul 24, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Nadhani ni wakati muafaka kwa CHADEMA kutazama upya mtizamo wao kuhusu muundo/aina ya muungano utakaotufaa. Binafsi sikubaliani na aina yeyote ya muungano zaidi ya ule wa serikali moja. Kama haiwezekani ni bora tusiwe na muungano kabisa.

  Imeshaonekana wazi kwamba iwe ni serikali mbili au tatu, zote zina matatizo na hazituletei mshikamano tena, achilia mbali kuhatarisha amani. Nadhani umefika wakati wa kuamua moja.

  Tuungane tuwe kitu kimoja (yaani serikali moja, au tuachane, kila mmoja ajitegemee. Tumekuwa na kero kwenye muungano kwa about 50yrs na tumejaribu kuzitatua kwa muda wote huo.

  Tukubali tu kwamba tumejaribu, tumeshindwa na hatuwezi tena kusonga mbele!
   
Loading...