Mkuukufufua viwanda vilivyo kufa,migodi ndo njia ya kuongeza ajira so si chadema tu ndo itoe ajira hata wewe pia waweza anzisha ili uisaidie nchi yako na vijana wenzako kupata ajira
Kwa sasa hivi nchi inakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa ajira kwa vijana wetu wanaohitimu mafunzo yao mbalimbali, hakuna juhudi za dhati zinazochukuliwa kukabiliana na tatizo hilo; kama kawaida yetu ya kulalamika kila mmoja analalamika; lakini hakuna hatua za dhata kunusuru tatizo hilo!!
Ufisadi unaongezeka kila kukicha ukiacha matukio yaliyoripotiwa miaka iliyopita hv sasa kuna utoroshaji wa fedha kwenda nchi za nje!
Kama kawaida yetu linafanyiwa kazi na vyombo husika, watanzania tumebaki kulalamika huku tukiwa na hali ngumu za maisha, kiasi cha baadhi kukosa hata mlo mmoja wa siku!
Vijana na hawajui future yao, wengi wao ukiwauliza mipango yao katika miaka miwili ijayo hawajui wakujibu nini!
Wanaambiwa wakajiajiri huku wakiwa hawana mitaji, vifaa, wala hata elimu ya ujasiria mali bila kusahau ukosefu wa masoko! Watajiajiri vp! Jaribu kufuatilia watoto wa hao wanaowambia vijana wetu wakajiajiri uone kama wamejiajiri wao! Rasilimali za wananchi zinaliwa na wachache!
Ebu nyie mnaojiita nguvu ya umma tuambieni mtatatua vp haya mattizo yetu?
Manake siasa zimetuchosha! Hamna lolote tunalosaidika badala ya kuwa walalamishi tuuu! Pia tuzingatie kuwa na nyie mna matumbo kama hawa wengine waliopo sasa pia mna njaa kama wao! Nini kitawafanya msile kama hawa jamaa ile hali mna sifa zinazofanana za njaa na matumbo pia?
Naomba kuwasilisha
Binafsi nadhani msukumo unatakiwa utoke ndani ya mtu mwenyewe kama mtu hana nia hata ufanye vipi hawezi kuwa na nia na cjui kwann hili serikali halitaki kuliweka wazi kuwa sekta binafsi ndio injini ya gurudumu la maendeleo ya taifa letu kama ndio hivyo fursa zinapaswa kuwa wazi ili vijana hasa wanaomaliza vyuoni waweze kupata moyo wa kujiajiri kuliko kukaa kusubiri ajira za kuajiriwa.Fursa kwakweli kwa mtu anayeumiza kichwa kuzitafuta ziko nyingi sana sema kulalamika ndio imekuwa njia yetu ya kupoza machungu kwa wengi wetu,nilishawahi kuandika humu jamvini kuwa moyo wa kujituma na kujitolea unahitijika kwa mtu kama anataka kujiajiri maana sio lelemama yahitaji kujitoa kwa dhati na wakati mwingine bila kukata tamaa maana sio kila ufanyacho unaweza kufanikiwa kama mtu mmoja maarufu duniani Edson huyu alikuwa ni mvumbuzi wa 'bulb' tunazozitumia hii leo lakini katika tafiti zake za kutengeneza bulb alifail majaribio 1000 (1000 times) katika hali ya kawaida mtu unaweza kukata tamaa na msaidizi wake alishakata tamaa akamwambia kuwa anachokifanya hakiwezekani alichomjibu ni kuwa hajafail mara 1000 bali amejua njia 1000 ambazo haziwezekani.Hivyo kwa vijana wenzangu tuko na changamoto nyingi cha msingi ni kutokata tamaa
wao wanautofauti gani wakati ni watu wale wale tena watanzania wale wale makabila yale yale, mazingira tunayoishi ni yale yaleSidhani kama CDM wana njaa na ulafi wa kukwapua rasilimali za nchi hadi kufikia wanafunzi kukaa chini,mahospitali kukosa dawa etc kama wanavyofanya hao wengine,
Katiba kijana inahitaji usimamizi katika utekelezaji, kwanza katiba hiyo unayosema sio nzuri ndio maana kuna mchakato wa katiba mpya. Kwanza hawa wezi wanaofilisi nchi inahitajika waondolewe kwenye madaraka ili mambo mengine yapate kutekelezwa!! Kuna mambo mengi tuu yamekaa tenge, kama wewe sio mnafiki basi unajua nazungumzia nini, kama fedha zetu zilizofichwa nje ya nchi zinahitaji kurudishwa zisaidie maendeleo!!!hata katiba ya hawa jamaa wengine(ccm) ni nzuri mno lakini hakuna lolote lililofanyika kutokana na ubora wa katiba yao
Tena kusimamia katiba na sheria, wezi woote na wala rushwa kuwekwa lupango (jela) ndiyo sehemu yao, sio wezi wawe kwenye majukwaaa ya siasa na wenyeviti wa tume za bunge linalotunga sheria!!!Mkuu
Serikali/dola wao ndo watunga sera pamoja na sheria, kuzisimamia na kuhakikisha zinatekelezwa!
Ni kweli mtu mmoja mmoja anahusika lakini serikali ndo inatakiwa iwe inatoa miongozo na kuwachukulia hatua wale wote wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao kisheria!
isingekuwa ni hivyo tusingekuwa na serikali!
kila mtu angefanya atakavyo
Nia yako si kujua CHADEMA itawasaidiaje vijana wasiokuwa na ajira tu hata kuwasaidia wenye akili mbovu kama yako kwani kwani kama ungetaka kujua chadema itawasaidiaje usingemaliza kwa kashifa uko mwishoni mwa maelezo yako. Hivyo jibu la kwanza chadema itaanzia kwako kukuomba uachane na mawazo potovu ya wanachadema ambao wanapambana na udhalimu wa nchi hii uliowafanya Wtz wawe masikini kila uchao.
Katiba kijana inahitaji usimamizi katika utekelezaji, kwanza katiba hiyo unayosema sio nzuri ndio maana kuna mchakato wa katiba mpya. Kwanza hawa wezi wanaofilisi nchi inahitajika waondolewe kwenye madaraka ili mambo mengine yapate kutekelezwa!! Kuna mambo mengi tuu yamekaa tenge, kama wewe sio mnafiki basi unajua nazungumzia nini, kama fedha zetu zilizofichwa nje ya nchi zinahitaji kurudishwa zisaidie maendeleo!!!
Acha uvivu soma ilani ya cdm ya uchaguzi 2010/2015 ina majibu ya maswali yako, pia bajeti mbadala na taarifa ya mwelekeo wa uchumi kuna uainishaji wa jinsi ya kupunguza uhaba wa ajira, kuziba mianya ya ufisadi na kukuza uchumi ili kutoa matumaini mapya kwa vijana na wananchi kwa jumla.
wao wanautofauti gani wakati ni watu wale wale tena watanzania wale wale makabila yale yale, mazingira tunayoishi ni yale yale
kufufua viwanda vilivyo kufa,migodi ndo njia ya kuongeza ajira so si chadema tu ndo itoe ajira hata wewe pia waweza anzisha ili uisaidie nchi yako na vijana wenzako kupata ajira