Mzalendo_Mwandamizi
JF-Expert Member
- Dec 12, 2007
- 1,116
- 4,773
Kabla ya Julai 2015, nilikuwa miongoni mwa Watanzania waliokuwa wakiiunga mkono Chadema. Sio kama mwanachama bali nilikuwa naafikiana nao katika harakati zao za kisiasa hususan vita dhidi ya ufisadi.
Lakini ghafla wakampokea Lowassa, mwanasiasa ambaye Chadema hao hao walimwandama kwa takriban miaka tisa mfululizo (tangu mwaka 2006 hadi 2015) wakimuita fisadi.
Na wala sikutafakari mara mbili, nikaamua kuacha kuiunga mkono Chadema. Bahati nzuri Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt Slaa ambaye pia alikuwa mgombea urais mwaka 2010, nae aliamua kuachana na chama hicho. Niliandika haya kumpongeza
Sidhani kama Chadema wanahitaji kupewa pole kwa sababu kila aliyejaribu kuwatahadharisha kuhusu Lowassa aliishia kutukanwa.
Uamuzi wa Lowassa kurejea CCM si jambo la kushangaza kwa sababu (a) alihama CCM kwa ajili tu ya kusaka urais huko Chadema (b) kwa kugombea urais kupitia Chadema, Lowassa aliweza kukihenyesha chama hicho kilichomuita fisadi huko nyuma, lakini kikalazimika kuzunguka nchi nzima kumsafisha Waziri Mkuu huyo wa zamani.
Kwa kifupi, Chadema mmevuna mlichopanda. Hatma ya chama hiki sasa itategemea sana jinsi kitakavyoweza kuhimili kipigo hiki kikubwa kabisa kwao. As it stands, kuna uwezekano mkubwa kabisa kwa chama hicho kutoambulia japo jimbo moja katika uchaguzi mkuu ujao, sio kwa kushindwa bali sio siri kuwa kuna wabunge kadhaa wa chama hicho wapo njiani kwenda CCM.
Na liwalo na liwe, wabunge wawili wasiotarajiwa kabisa kuwa ipo siku wataikimbia Chadema ni Kubenea na Bulaya wapo njiani kwenda CCM.
Tujikumbushe #FutureTweet hii ya Januari 9 mwaka jana
Sent using Jamii Forums mobile app

Vyama Vingi