CHADEMA mmetuamsha! Tulikuwa tumelala

Kifuna

JF-Expert Member
Aug 7, 2008
434
96
Kitendo cha CHADEMA kutoka Bungeni mbele ya mkuu wa kaya akihutubia ni kitendo cha ujasili uliopindukia. Maana watanzania wengi hatujui nini hasa Demokrasia inavyotakiwa kuwa. Ni kweli JK ni Raisi Na ni kweli alitakiwa kuheshimiwa lakini Tume iliyuyompa nafasi hiyo haijiheshimu hata kidogo kwa kusoma matokeo tofauti na yale yaliyoletwa toka Majimboni.

Tuliwasikia mala ya kwanza CHADEMA walilalamika kabla matokeo hawajamaliza kuyasoma lakini wazee wale walipuuza. kwa kitendo kile cha kutoka bila kujali umati uliokuwa ukisikiliza hotuba ile nimekipenda sana. Labda sasa tutaanza kuwa na nidhamu kwenye chaguzi zetu.

Kosa ninaloliona lilifanyika mle Bungeni ni kitendo cha wanasisiemu kuwazomea wenzao waliokuwa wanatekeleza Demokrasia yao. maana Bungeni huruhusiwi kusema mpaka Spika akuruhusu lakini unaruhusiwa kutoka Na taratibu zote za Bunge zinaendelea. Nasema tena CHADEMA mmetuamsha maana tulikuwa tumelala. Naomba kutoa hoja!!
 
zomba

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
17,008
3,666

Tafadhali nakuomba, kwanza kabla ya yote, jifundishe kuandika kiswahili kizuri:

"ujasili" = ujasiri
"mala" = mara

Usituharibie ladha ya lugha yetu tamu.
 
KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,428
8,191
Tafadhali nakuomba, kwanza kabla ya yote, jifundishe kuandika kiswahili kizuri:

"ujasili" = ujasiri
"mala" = mara

Usituharibie ladha ya lugha yetu tamu.
Nawewe usitukwaze asubuhi na viswahili vyako kama unataka kuwa msanifu wa lugha nenda BAKITA hapa siyo mahali pake!!unaleta chai hapa!!
 
Kifuna

JF-Expert Member
Aug 7, 2008
434
96
Ok, mi nilikuwa sijalala

Asante kwa kuwa ulikuwa hujalala, lakini kumbuka mwaka 1995 Lwatonga alishinda pia! Ila alikuwa hajui aanzie wapi. Sasa CHADEMA wameonyesha njia. Kuanzia hapo tusonge mbele wote tunajua nguvu ya umma...Pipoooooooooozi!!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom