CHADEMA mmemuona Regia Mtema na Morogoro yake? Hii ya kilombero mpaka ifakara je? Wabunge mmeona?

FDR.Jr

JF-Expert Member
Jun 17, 2008
1,359
353
CDM mmemuona regia e. Mtema na Morogoro yake? Hii ya Kilombero mpaka Ifakara je? Wabunge mmeona?

Kwa mara ya mwisho kuwasiliana na regia ilikuwa ktk salamu zake za mwaka mpya, nilimpongeza na kumkosoa na ninamshukuru alinielewa na kunipa tumaini kuwa nilichomkosoa kimo ktk kalenda yake ya 2012......,

Nilifarijika sana hasa pale aliposisitiza na aliponibainisha kwa lugha ya nyumbani, aliahidi pia atani pm .........; naugua kwa kifo chako na licha ya u ccm wangu nilitamani niwe hapo viwanja sitini-benki muda huu ila mungu amenipa faraja kwa yaliyotokea leo pale dada yangu ulipougusa mkoa wa morogoro-mikumi-ruaha-kilombero-mang'ula-kiberege-sagamaganga-kaporo-kibaoni na dakika 40 zilizopita umeingia ifakara viwanja sitini -benki ktk uwanja wa familia ya mtemanyenja aka mtema.

Mlongu wangu umeiandika historia na umeacha fundisho kwa wote waliokusindikiza leo kuingia huko nyumbani. Wan jf. Nawataka wabunge wote walioenda leo ifakara na kesho wakishamlaza nyumbani regia wajiulize kama wataipata heshima hii aliyoipata Regia tangu amefariki na sasa mko Ifakara nyumbani kwao?

Bint wa 1980 ameunyamazisha mkoa wetu, ameziliza wilaya na ninawapoandikia hii taarifa muulizeni pedeshee mteketa amekumbwa na nini ifakara, ccm, cdm, cuf na wengineo tujifunze kuingia mioyoni mwa wananchi wetu kwa namna njema na yenye mashiko.

Imeandikwa "jililieni.........." neno hili hutimia kwa utu wema wetu na siyo vinginevyo. Rudini bungeni mpiganie alichoamini regia wabunge ulanga -kilombero pokeeni kijiti chake, acheni zecomedy iliyofanywa malinyi siku ambayo regia alipopata ajali juu ya mashamba ya mpunga, dkt mponda, maige na dkt hovisa kupingana mbele ya wahanga wa sakata hilo.

Mmeidhalilisha serikali. Suzan kiwanga chapa kazi msaidie mteketa tupate mageuzi kilimo na miundo mbinu.

Lala kwa amani dada yangu Regia Mtema.
 
Jitahidi kupanga habari yako kwa paragraph na muonekano mzuri.....otherwise ni habari njema yenye matumaini.
 
wakati mwili ukiingia ifakara jana...watu walikuwa wakiimba nyimbo za kejeli na vijembe kwa mteketa.......huyu jamaa hapendwi lakini pia wakazi wa ifakara wanadai ndo mchawi
 
wakati mwili ukiingia ifakara jana...watu walikuwa wakiimba nyimbo za kejeli na vijembe kwa mteketa.......huyu jamaa hapendwi lakini pia wakazi wa ifakara wanadai ndo mchawi


Mteketa ni nani?? tupe CV yake!!

naskia tu jina lake kwa ngwasumaaaAaa
 
Jamani huyu jamaa alikuwa anaandika huku analia ndo maana kaandika kwa fujo..
 
mleta mada nadhani ana hisia kali sna...hasa jana mwili ulipofika ifakara...watu wengi walijitokeza kuupokea mwili wa marehemu....walikuwa wengi sana..(kuna picha nimeweka humu)....

Kujitokeza kwa watu wale na wengi wao walikuwa wakiimba nyimbo na kutoa maneno si mazuri kwa mbunge wa jimbo hilo bwana mteketa kuwa ndiye yuko nyuma ya kifo cha Regia na sasa amechokoza nyuki...wengine wakaenda mbali sana wakisema leo wasimuone kwenye mazishi...

Hali hii ilipeleka kumfanya mwenyekiti wa chadema taida (mbowe) kusimama na kuwasihi vijana watulize munkari...maana walikuwa wengi na hii ilipeleka kuchelewa kuufikisha mwili hosp.


chek picha hii hali ilivyokuwa



 
Changamoto kwetu 2liobaki, 2fanye mambo ya msingi. Jamii itukumbuke kama Regia. We mic u mama
 
Back
Top Bottom