Lijualikali: CHADEMA iliiba kura za Urais baadhi ya Majimbo 2015

usinijibu hivyo

JF-Expert Member
Nov 7, 2017
248
327
*TULIIBA KURA KILOMBERO 2015*

Na Peter Lijualikali (Mbunge).
Ndugu Zangu naomba niendelee Kusema Ukweli na Kufichua Baadhi ya Mambo tuliofanya CHADEMA ili Wokovu Uendelee Kunibariki Kabla Sijaondoka Duniani.

Wilaya ya Kilombero ina Majimbo 2, Mlimba (CCM aligombea Godwin Kuambi Sasa Mkurugenzi wa Dodoma na CHADEMA alikuwa Suzan Kiwanga na Upande wa Kilombero CCM alikuwa Abubakar Asenga Sasa ni DAS na CHADEMA nilisimama Mimi).

Tathimini yetu haikuwa Nzuri baada ya CCM Kumsimamisha Magufuli Upepo Ulibadilika Wengi walijua angekuja Membe, kwa Ukweli Kilombero ina WanaCCM wengi hasa Wanawake, vijana ilionekana ni Washabiki zaidi Kuliko Kupiga Kura.

Hivyo ikatulazimisha kutembelea Upepo wa Mzee Lowasa wa Wakati Ule na kulazimisha Lazima Aje kufanya Kampeni Kutusaidia Wilaya ya Kilombero.

Mara ya kwanza Mzee EL alitangaza kuja na watu wakakusanyika Uwanja wa Hosp ya Kansa Mission Kwa Maelfu, Mzee hakutokea. Hiyo siku nilitamani Dunia ipasuke kwani watu walitawanyika huku wakitukama matusi na Kusema hawatoenda Kupiga Kura Tukio hill liligawa sana Kura Zetu.

Tukaendelea Kulazimisha CHADEMA Makao Makuu kuwa Mzee EL lazima aje Vinginevyo hali yetu itakuwa Mbaya sana baada ya Mzee Magufuli kupita October 18/2015 kuomba kura na Kujaza watu Wengi sana.

Tukajulishwa kuwa Mzee EL atakuja Siku 2 kabla ya Kupiga Kura. Kwa Maana Oct 23 atatua na Helcopta jimbo la Malinyi, Mlimba na Kilombero, Na Oct 24 Jmos atafunga Kampeni Zake Jangwani Dar ili J2 ya Oct 25 Watu wakapige Kura.

Baada ya Mzee Kutua Kosa ambalo lilipunguza Tena kura zetu ni akiwa Jukwaani Ifakara alikosea Baada ya Kumuombea Mgombea Wake wa Ubunge Kura alitamka *nichagueni Mimi na Mbunge wa CCM*"

Hali ilichafuka sana na mamia ya watu wakaamini yule Mzee anafanya kazi ya CCM.

Tulipofatilia baadae tukajua kumbe Tathimini ya Chama CHADEMA Makao Makuu ilionyesha Wabunge wa CCM walikubalika zaidi nakuwa sisi kwa kuwa tulikuwa Diwani wa Mjini Ifakara tangu Mwaka 2013 kabla ya Kugombea Ubunge, Kuna mambo tuli yakosea hivyo watu waliona hakuna jipya, hivyo Mgombea Urais EL akitaka apate kura nyingi ili aunde kwanza Serikali ikawa awataje Wabunge wa CCM Hadharani ili Mashabiki wao Wakiwapigia kura wapige na Za Urais, Asenga aliungwa Mkono sana na Wanawake na Kina mama.

Hilo jambo ambalo lilipangwa na Mkutano Ule ulirushwa LIVE na ITV walioangalia Watakumbuka nisemacho Mzee Lowassa aliharibu Jukwaani Mbele ya Maelfu.

Tulipokomaa tukaambiwa kuna Mkakati wa Chumba cha Kuhesabu kura na kuwa CHADEMA lazima ishinde.

Baada ya Ule mkutano Mvurugano Ulikuwa Mkubwa sana sana.Mashabiki wetu walichukia sana Kwanini Mzee yule EL awataje Wabunge wa CCM?

Siku zilikuwa Zimeisha, tukajulishwa kuwa Mzee alipotua Alimuacha Mwanae na Wadau Muhimu kupanga Mkakati Kwa kukutana na Mkurugenzi, OCD Na DC wa wakati Ule. Na Walikutana nao Kwa kuwa Ilisemekana Wote hao Walisaidiwa na Mzee EL kupata vyeo vyao hivyo wasingeweza Kumpinga, tukajulishwa Kuwa Waliwezeshwa vya kutosha ili kuhakikisha Jimbo la Mlimba na Kilombero yanaenda CHADEMA.

Katika Ukumbi wa Kuhesabu kura Kosa ambalo Asenga na Kunambi walifanya ni Kuanza kuzisimamia Kura za Mgombea wao wa Urais Magufuli wakiwa na kijana mmoja aliitwa Rama Sasa nae ni Mkurugenzi wa Halmashauri kama nakumbuka Vizuri ni Karatu.

Kwa Waliokuwepo ndani ya Ukumbi wa Halmashauri Ifakara Wakati Kura zinawasili watakumbuka Kazi iliokuwa inafanywa na Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi kubadili karatasi za Majumuisho ya Kura haraka na kuwapa Wasaini Upya.

Wakati huo Wagombea Ubunge Kunambi na Asenga Wao wanaangaika na Na Makaratasi ya Kura za Rais wao.

Walipozipata Karatasi za Kata zote Tuna zijumlisha Mezani kumbuka wakati huo wale vijana wanaendelea na zile za Ubunge Kutuongezea Kura Mimi na Suzani Kiwanga na Kuzisaini zile za Majumuisho.

Tumejumlisha Kura za Wagombea Urais, Magufuli akapata kura Nyingi kuliko Mzee Lowasa. Presha ilitupanda sana

Magufuli Kura 49,478
Lowassa Kura 49166

Isinge wezekana hata Mara moja kwa Upepo Ule wa Lowassa, Mgombea Ubunge wa CHADEMA Kupata Kura nyingi zaidi ya Lowassa, ambae kutokana na Upepo wake alikuja Kuniombea Kura na Ukweli alikuwa na Watu Wengi sana.

Kwa kuwa Vijana hao Walisimamia kwa Macho na Masikio kura za JPM ilikuwa Ngumu kufanya Mchezo wowote Ule nao Waliamini Endapo JPM atapata Kura Nyingi basi na wao watakuwa Wameshinda kwa kuwa Ndio waliozunguka Vijijini Kumuombea Kura.

Kama watafikiri Vizuri watagundua Katika Kura za Urais kule ndani hatukubishana hata kidogo Kwa kuwa waliyakomalia sana Yale makaratasi ya Urais wakati huo sisi tunaangalia Majimbo tu.

Tulipoanza kujumlisha kura za Majimbo mle ndani Mimi niliagiza Redbull yangu nikawa na kunywa Taratibu.

Nakuwaacha wajumlishe wao na Wakala wangu pacha wa Rejia Mtema. Nikiwazoom tu Kwa pembeni.

Jambo ambalo lilianza Kuharibu ni kuonekana Waliongeza kura nyingi Zaidi kwa Wabunge wa CHADEMA Kuliko ata idadi ya Wapiga Kura wa baadhi ya kata na Vituo.

Vijana wa CCM wakaanza kama kushtuka mle ndani.

Kuwa kabla hatujamaliza Kujumlisha tuhesabu Kura za Masanduku, Tulianza kusikia baridi.

Kwa kuwa walimuamini Mkurugenzi yule Dada Azimina, aliwaambia tumalize kujumlisha Kwanza Karatasi za Majumuisho toka kwenye kata then tutaenda kwenye Mabox.

Walifanya Kosa kubwa bila kujua yule Dada alikuwa Mwana Mkakati wetu wa Lowassa.

Kwa mvutano Ule wa Uchaguzi Mimi Lijualikali nisingeweza hata kidogo Kupata kura nyingi Kuliko Lowassa.

Lijualikali kura 52,158
Lowassa kura 49,166.
Magufuli kura :49,478
Asenga kura:49,490

Kura za Mgombea Urais wa CCM ziliendana sana na Kura za Mgombea wa Ubunge tofauti ilikuwa ndogo sana.

Na huo ni Ushahidi kuwa kila MwanaCCM aliempigia kura Rais wa CCM alipiga pia kwa Mbunge wa CCM na Diwani.

Yani Mimi nilimzidi Lowassa Kwa Kura (52,158-49,166= 2992)
Hizo 2992 ni kura nyingi sana kumzidi Lowassa Mwaka 2015.

Mzee Lowassa alikuwa na Upepo Mkubwa Mara 3 yangu alijaza watu Kuliko niliojaza katika Mikutano yangu .ISINGE WEZEKANA HATA KIDOGO.

Kunambi na Asenga Wakaanza kuzingua kushtukia Mchezo wakishinikiza Twende kwenye Mabox ya kura.

Mara Mkurugenzi akatoka na kukimbia nje ya Ukumbi wa Kuhesabu kura, ili kuepuka zoezi la kuanza Kuhesabu Mabox, akateleza na kuanguka askari wakamrudisha ndani akasema amepokea Meseji Nyumba yake Mabanda yamechomwa Moto na kuna watoto wake. (ilikuwa sehemu ya Mpango).

Mara DC wa wakati huo akawapigia Simu vijana wake (Asenga na Kunambi) na kuwaita ikulu ndogo Wakale ili warudi Kuhesabu kura za Mabox (Makazi ya DC si mbali na Ukumbi wa Kuhesabu kura ni kama Mita mia 3 hivi).

Vijana bila kujua kuwa DC yule alikuwa Mtu Kindaki ndakiwa Lowassa kama ambavyo Lowassa alikuwa na MADC Wengi wakimuunga Mkono wakati Ule ikionyesha wazi alipokuwa Waziri Mkuu alipanga Safu zao pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri.

Vijana wakatoka kwenda Kula ikiwa ni saa tatu Usiku Muda huo Wakisambaza habari kuwa JPM kashinda kura na kura za Wabunge tunarudi Kuhesabu moja moja.

Wakati huo nje ya Ukumbi tumejaza vijana wa CHADEMA kwa mamia, Ikabidi tuvujishe kuwa CCM inachelewesha Matokeo wanataka kuiba Kura.

Vijana wa CHADEMA wakawa wanasogea karibu wapite utepe wa Polisi.

Hakuna askari aliefanya kitu maana yule Mzee OCD Alikuwa ni Mpenzi Mkubwa wa EL.
Vijana wetu kama kawaida jazba ikaanza kuwapanda. Wakiimba kurusha mawe wengine wakaanza kuchoma Moto jengo la Baraza la Ardhi Wilaya.

Tukakubaliana tutoke wabaki Polisi ili saa moja Asubuhi turudi Kuhesabu kura kwa kuwa Asenga na Kunambi waliyakataa matokeo ya Ubunge .Tukakubali na wao vijana wakaenda nyumbani kwa DC nafikiri walilala pale.

Mkakati wa Mwisho wetu ukawa Mkurugenzi Asubuhi atangaze Yale matokeo kabla ya Saa moja Asubuhi tuliopanga kurudia Kuhesabu kura.

Akaandaliwa Muandishi wa ITV Vizuri,

Swali Mkubwa likawa
Upande wa CCM nani anathibitisha Matokeo na Wagombea wameyakataa?

Usiku tukaenda Kumuona Mzee Kambangwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya huyu alikuwa MwanaCCM Wa Lowassa alikuwa anasema wazi *kumzuia Lowassa ni sawa na Kuzuia Mpango wa Mungu*

Akapewa Mzigo wake ikaandikwa barua kuwa amemteua alikuwa Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi ya CCM wakati Ule Mzee NGELANGELA
Ili asaini Matokeo kuwa CCM imeridhia.

Mzee akawekewa Mpango sawa akaenda Kusaini Matokeo kwa Niaba ya CCM Usiku huo huo.

Ndipo alfajiri mbele ya Kamera Ya ITV Mkurugenzi akatangaza Ushindi kwetu kwa Kura:
Lijualikali: 52,158
Asenga: 44,492
Suzani Kiwanga:40,068
Kunambi:34,883

Vurugu zikaanza vijana wa CCM hawakubali vijana wa CDM wanashangilia kiasi askari walitoka Morogoro Mjini kuja kuongeza Nguvu Ifakara.

DC akapewa kazi ya Kuwasihi Vijana watulie kama hawajaridhika waende Mahakamani.yalioendelea Mahakamani Tutawaambia Wakati Mwingine.

Naona Baadae CCM ilistukia Mchezo Mkurugenzi, DC na yule OCD waliovuliwa Vyeo.

Ndugu zangu Lowassa alijipanga kwa kila namna kuchukua Dola 2015.Wasaliti wa CCM walitumika sana.Watu walikuwa CCM Mdomoni tu na Moyoni walimuunga Mkono Lowassa wakiamini alionewa kukatwa CCM.

Mtu anaeweza kuitikisa CCM ni yule Mwenyenguvu CCM akitoka nje ya CCM kama alivyokuwa EL.Vinginevyo CCM ikishikamana kama ilivyosasa Itaongoza Nchii hii miaka Mingi ijayo.

Nawaomba Radhi wote niliowakosea na imani yangu Vijana waliokosa Ule Ubunge zamu yao itakuja

Mungu awabariki sana.
#Mandela

Kama ni kweli hii basi tutajua Mengi sana ata ya vifo vya watu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo jamaa ameamua kuwa mropokaji sasa, akishawataja waliomsaidia kuiba hizo kura kwa majina, waende mahakamani, aache porojo za kitoto na kuwadanganya watu.

Wapo waliokesha nae kuhakikisha ushindi wake hauchakachuliwi, then yeye leo anasema hakupata ushindi wa halali!.

Halafu anasema leo baada ya kupokea marupurupu yote na mshahara kama mbunge, tena kwa miaka yote, hii level ya ujinga anayoonesha ni ya kiwango cha juu mno!.

Huyu anastahili kesi ya Uhujumu Uchumi.

Karma will do.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo jamaa ameamua kuwa mropokaji sasa, awataje waliomsaidia kuiba hizo kura kwa majina, aache porojo za kitoto na kuwadanganya watu.

Wapo waliokesha nae kuhakikisha ushindi wake hauchakachuliwi, halafu yeye leo anasema aliibiwa kura!

Karma will do.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona kawataja! Wewe fuatilia DED, DC, OCD na Mwenyekiti wa CCM wakati huo basi.
 
Ukiona mgeni wako ana toa siri za alipo toka jua akitoka na kwako ata zitoa tu siri zako apeleke kwingine

Dark Side
Hiyo mikasa Nyerere aliiweza ndio maana hakukuwa na ujinga wa hivi. Ogopa sana mtu anayesnitch. Ingekuwa USA hawa wangekuwa wanapigwa pipe sana. Hata hapo chini tu kwa madiba, masnitch wanakula bomba watangulie mbinguni. Hata katika siasa mtu snitch sio Mzuri kabisa hata kwa ustawi wa taifa na taasisi kama CCM

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom