CHADEMA, mmeagana na nyonga katika kumpokea Nyalandu na wengine wa aina yake?

Sasa. Kama nyalandu ni fisadi na alikuwa CCM.
Ina kuwaje CCM. Ina Kaa na mafisadi?

Kiukweli kumuita mtu fisadi wa Kati ameondoka kwenye chama chenu. Sio sawa. Msingoje mpaka aondoke ndo mseme.

Uenda wameamua kujisafisha. Wangeendelea KUA CCM. Wangeendelea kuwa mafisadi.
Kinyonga ubadilika kutoka na mazingira.

Ni Nani msafi ndani ya CCM?
Kama boss anapiga. Kwanini na Mimi nisipige?
 
mkuu...nini mzee wa kanisa? kuna wengine wanapewa na uchungaji kabisa!
Aisee hiyo kali,labda wanaanzisha makanisa yaosasa ukijipa uchungaji hakuna maswali tena,lakini ukimkuta mwenye dhabahu lake!sidhani. Otherwise kawe kakusanyiko kawasanii.
 
Chama ni watu tutaendelea kupokea wanachama wapya tena vigogo wengi kutoka ccm. Hatuwezi kusajili mbuzi tunasajili watu.CCM mtuelewe hivyo
Kila mmoja mchafu anayeingia, wasafi 20 wanatoka ndukiiiii...sasa hizi ni akili au tope?
 
Kuna wakati mwingine mnajinasibu kama wanasheria wasomi lakini mnayoyaandika sijui kama walimu wenu wanapata mda wa kuyasoma na kuona product walizotupa duniani. Hata waliotunga sheria ya mtandao wanajua kabisa unachokiamini wewe ndio jinai yenyewe na hii wala haikuzuii kuingia hatiani.

Kama ulivyo wewe mkweli na kusimamia unacho kiamini ndio Mwenzio Nyalandu ameshindwa kustand heat in the kitchen, dont bother wengine watasema nini CCM haiwezi kemea mafisadi, wezi, wafoji vyeti, watekaji, wavunjaji sheria, na wananchi wanaona dhahiri shairi na watachukua hatua stahiki. Hata kama wewe hukubaliani na huna chama wenzio watajengaje chama kama hawatoandikisha wanachama wapya pamoja na walio CCM.

Mwanzo mwanzoni nitamke wazi (narudia mara kwa mara) kuwa mimi Petro Eusebius Mselewa si mwanachama wa chama chochote cha siasa hapa Tanzania na kwingineko. Najua kuwa ninachokiandika humu huwa kinamkwaza huyu na kumfurahisha yule kutokana na maudhui yake. Lakini, naamini kuwa daima huzungumza ukweli na kile ninachokiamini. Ndiyo maana sioni haja hata ya kuficha utambulisho wangu. Hivyo, nimeshakuwa sugu katika kukosolewa na kusifiwa.

Pili, naamini kuwa kuwa siasa ni abrakadabra. Siasa imejaa uongo, maigizo, utapeli na ulaghai wa hali ya juu. Leo huyu anapondwa; kesho huyohuyo anasifiwa. Mara baada ya Lowassa kutangaza kuhamia CHADEMA, nilikuwa wa kwanza bila woga,aibu au chuki kusema hivi:Sikubaliani na hoja ya Lowassa Kujiengua CCM na Kujiunga CHADEMA/UKAWA

Pamoja na ukweli kuwa wanasiasa hubadilika zaidi ya upepo katika kuponda na kusifia, huwa ngumu kugeuza ukosoaji kuwa sifa. CHADEMA ilijijenga katika misingi ya kuukosoa na kuupinga ufisadi. Ilipendwa katika misingi hiyo na kuvuna wanachama kwa maelfu hasa wasomi na vijana. Ilikuwa ikirusha makombora kwa kila iliyemuona ni 'fisadi' ndani au nje ya CCM. Waathirika wakubwa wa makombora hayo ya CHADEMA walikuwa Orodha ya Mafisadi na hata Nyalandu.

Orodha ya Mafisadi (iliyomjumuisha Lowassa) na hata aliyekuwa Mbunge Nyalandu ilisemwa na CHADEMA kuwa ni mafisadi waliobobea na wasiofaa si tu kwenye uongozi bali pia kwenye siasa na maisha ya kitanzania. Ya Lowassa yakatokea na sasa yanafuata ya Nyalandu. Kazi ya CCM itakuwa nyepesi sana kama ilivyokuwa kwa Lowassa. Ni kusema tu kuwa kwasasa mafisadi wanahamia CHADEMA.

Ndiyo maana nawauliza CHADEMA: mmeagana na nyonga katika kumpokea Nyalandu na wengine wa aina yake? Yaani, kuna maandalizi ya kutosha kuonyesha usafi wa Nyalandu na wanachama wengine watarajiwa wa aina yake ili kuondoa dhana ya wanaCCM kuwa sasa mafisadi wanajiunga na CHADEMA?

Ndiyo maana tangu kutolewa kwa tangazo la Nyalandu la jana, nimekuwa nikichezwa na machale kuwa huenda kuna mchezo wa kisiasa unachezwa. Ni wa kuwatinga CHADEMA katika kujibu tuhuma dhidi ya waliowahi kuwatuhumu ili hali CCM ikichanja mbuga katika kujiimarisha na kujiandaa kwa uchaguzi mkuu ujao. Hakika, CHADEMA itakuwa na la kueleza kila uchao kumhusu Lowassa na Nyalandu. Au wakiri walikosea walipokuwa wakiwasemea vibaya.

Lakini, kwanini CCM na Serikali yake haikuwashughulikia akina Lowassa na Nyalandu tangu wakiwa CCM na hata sasa wametoka kama ni kweli kuwa wana ufisadi wanaohamia nao CHADEMA? Swali hilo nalo hunipa kizunguzungu na kuimarisha imani yangu kuwa siasa ni uongo,ulaghai, utapeli na propaganda.
 
makanisa (kwa mfano) yanawachukulia malaya, walevi, nk kama watenda dhambi.

lakini wanapofanya maamuzi ya kuachana na dhambi makanisa yale yale yaliyokuwa yanawaita kuwa ni wadhambi yanawapokea, yanawabatiza, yanawapa kipaimara na hatimaye wanakuwa sehemu ya waumini wengine.

kama makanisa matakatifu tu yanafanya hivyo, seuze vyama vya siasa?
Swadakta !
 
Ni haki yake ya kimsingi kuhama na kuhamia chama anachokitaka. Ila kama ni mkweli basi atoe mchango wake katika chama anachotaka kuhamia akiwa mwanachama wa kawaida...asitafute uongozi wa juu. Hii itawapa nafasi wanachama wengine, na viongozi pia, kujua mwenendo wake na kama ni muumini wa kweli wa sera za chama hicho....nafikiria tu kwa sauti
 
Nyalandu si kama wewe kwa sababu Nyalandu kaona mbali sana wewe endelea kuota!!!!!
Ni kweli sio Kama Mimi kwamaa ni msomi zaidi yangu!
Na pia alishiriki matukio ya kijangili kipindi akiwa waziri huku mkisingizia ccm huyo jamaa ni msanii kuliko mnavyodhani.
 
Tanzania hatuitaji malaika ila watu tu wakuitoa CCM madarakani haya mengine yatakuja tu.....CCM wamejisahau sana.
 
siasa ni uongo,ulaghai, utapeli na propaganda.
Hii siyo sahihi, siasa ni sayansi.

Baadhi ya watu wanaendesha siasa za majitaka ili tu kufikia malengo yao ya kushika madaraka hawa wapo tayari hata kuua kila atayeonekana ni kikwazo kwao kufikia adhma yao hiyo.
Hizo siasa za majitaka zina sifa ulizoeleza, ni kama kisu huyu anatumia vizuri yule anaua kwa kutumia kisu utasema kisu ni kibaya au ni mtu na namna anavyokitumia hichi kisu?
 
CCM Ebu mtajeni mwanachama mmoja tu mnaye weza kujivunia kuwa huyu ni msafi.Acheni watu watimize mapenzi yao acheni tabia ya kuuona hiyo ccm kama mbingu kuwa waliomo ni watakatifu ila unapojitoa umegeuka shetani.
 
Chadema wanazidi kuongeza ugumu wa kuitoa ccm madarakani...Tope la Lowasa linawatesa mpaka kesho bado wanajiongezea la Nyalandu...!

Ccm haifai lakini Chadema wanazidi kupoteana....
Tope la Lowassa in which sense?
 
Jibu swali Mkuu,unafiki wangu uko wapi?
Kuna wakati unashindwa kutofuatisha msomi na mjinga! Ndugu Mselewa, katika suala hili la Lowasa uchambuzi wako kama msomi (wakili msomi?) ungejitanabaisha kuwa wa kisomi, ni bahati mbaya umebaki kuwa blah blah! Hii ilikuwa fursa kwako kuji brand kama wakili/mwanasheria msomi. Nasikitika umepoteza fursa hii..
 
Huwa sielewi watu wanazichukiliaje siasa, hivi Chadema kabla ya Lowassa ilikuwa na nguvu kuliko hii ya sasa! Tafadhari jamani tusiwe wanafiki, Chadema ya sasa inakubalika popote hata ndani kabisa ya Ccm, ina nguvu hata bila ya kampeni za siasa, Chadema hii ya sasa umekuwa kimbilio la wanasiasa wazito kwa sababu tayari imeshaaminika, mie nadhani wakati huu ndo muda muafaka wa kumpokea mwanasiasa yeyote anayekuja, mahakama za mafisadi zipo, kama walifisadi wacha mahakama ziamue, lakini niwakumbusheni, hao mnaowaita mafisadi ndo hao kila siku wanarejeshwa bungeni na wananchi wao! Tafakari
 
Kuitwa kwao mafisadi na chama walichokihama ni kma njia ya kujisafisha km kijana akiachwa na demu,lzm utajihami kwa kusema kwanza huyu Demu alikuwa Malaya Sugu

Kuhusu siasa kuwa ni uongo ni sahihi100%

Kwa kuwa basi iko hivyo,acheni mchezo uendelee,japo kuhama kwake kumeongeza nguvu ya CDM pia isisahaulike kuwa anaweza kuwa kibaraka,hivyo mwekeni kado anatapikishwe kwanza,kisha aingie uwanjani kucheza mchezo huo wa uongo na ulaghai kma watu wengine!
 
Back
Top Bottom