Mshangai
JF-Expert Member
- Feb 16, 2008
- 468
- 1,086
- Thread starter
- #61
Mkuu Kalamu1 sio kuwa sijakuelewa unamaanisha nini. Ni hivi hata mie naamini katika Utanzania lakini tambua kuwa bado ni mwanachama wa CCM na kama tungesimamisha mtu makini na mwenye kujali utu na kusikiliza ushauri pengine hata hii mada nisingeandika.Nilichepuka kidogo, nikarudi, nikakuta bado upo, na michepuko yangu inaendelea, sijatulia.
Ni hivi: tofauti ninayoiona kati yako na mimi ni hii moja tu, ambayo kwa bahati mbaya hujanitambua niko wapi, kutokana na mstari huo ulioweka hapo.
Siambatani na chama kama ulivyoambatana na CCM wewe. Mwambata wangu pekee na wa kudumu ni Tanzania pekee. Hiyo ndio tofauti yangu na wewe.
Niliwahi kuambatana sana na CCM wakati fulani pamoja na kwamba sikuwa mwanachama. Sasa hivi natamani wapinzani, bila kujali Lissu yupo au hayupo, watusaidie kutuondolea hili zimwi ambalo linajigeuza kiasi kwamba linataka hata kuzuia njia ya kuliondoa. Hii itakuwa balaa kubwa kwetu.
Wapinzani wakiingia, miaka mitano wakivuruga, watakuwa hawajajiimarisha hadi waweze kutuzuia kuwaondoa tukiamua kufanya hivyo.
Hiyo ni tofauti kubwa sana na kuiacha hii CCM ya mtu mmoja kuendelea kujiimarisha kutunyonga.
Kama chama, nakubali CCM tulifanya makosa mengi huko nyuma lakini tulikuwa twaweza kukaa na kujadili wenyewe na hata wakati mwingine Rais aliwaita think tank wa upinzani kubadilishana mawazo.
Hakupata MTU kushambuliwa kimwili au kupotezwa. Lakini why Lissu? Kwa vile ndiye pekee anayeonekana anaweza leta mabadiliko, kuheshimu katiba, kutokuwa na visasi au chuki. Wengine ni yaleyale tuu na twaweza kurudi nyuma kwa kasi zaidi