CHADEMA mkae mtulie...

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Mkae mtulie kwa upendo na heshima. Muongee kwa staha na kwa kujenga hoja.Mheshimiane nyinyi kwa nyinyi.Tumieni Katiba yenu kumaliza hoja yoyote itakayoletwa mezani. Msikubali kupambanishwa na watamani madaraka kama wafanyavyo wenzenu wa 'jembe na nyundo'.

Mwenyekiti Mbowe na timu yako ya uongozi wa kitaifa,shughulikia matatizo ya chamani mwako kikatiba.Wananchi wa Tanzania wameshawaelewa hoja zenu.Wanasubiri 2015 wawape nchi muiendeshe.Bungeni,onesheni kuwa mnaweza.Majukwaani,jengeni hoja za kiukombozi. Magazetini,andikweni kwa wema.Runingani,tangazweni mnavyojisambaza kwa hoja mujarabu na umati wa Watanzania walio na matumaini nanyi.

Mwaka 2015,simamisheni mgombea ambaye hata uchakachuzi hautampora ushindi wake. Iwe wa Urais,ubunge au udiwani.Watanzania wanawangoja.Msiwaangushe. Mkae mtulie na hatari zote zisiwafikie.

Nangoja ukombozi...
 
Makundi mbalimbali yakijibu maswali kwamba "NI KITU GANI WANGEPENDA KIWEPO KWENYE KATIBA MPYA"?

Majibu yalikuwa hivi:

DEREVA:Traffic wasiwepo barabarani

MWANAFUNZI: Somo la hesabu lifutwe mashuleni

MFANYABIASHARA: TRA ibinafsishwe

WANACHUO: Bodi ya mikopo imilikiwe na Dowans

WAKAZI WA MBAGALA/GONGO LA MBOTO: Ghala la mabomu lijengwe ikulu

WANA NDOA: Vyeti vya ndoa viwe na 'expiry date'!

wewe jamaa unashangaza kweli jana wewe umetoa post ya uchochezi kwamba Zitto hawezi kuwa raisi wa Tanzania sasa nashangaa leo unasema CHADEMA watulie wakati wewe ndiye unawachonganisha
 
Wakitekeleza hayo chama kinakufa. Hawa ni watu wa majungu, kebehi, matusi na hata umaarufu wao unatokana na hayo , hakika kinyume na hapo hawana cha kuwaelelza wananachi, ni kama wasanii wa bongo na filamu na miziki ya mapenzi, wanafanya hivyo kwa vile wamegundua ndo yenye soko. CDM wanaamini kuwa matuki, kebehi , siasa za chuki ndo watanzania wanapenda kusikia na ndivyo wanavyopata umaarufu.
 
Makundi mbalimbali yakijibu maswali kwamba"NI KITU GANI WANGEPENDA KIWEPO KWENYE KATIBA MPYA"?

Majibu yalikuwa hivi:

DEREVA:Traffic wasiwepo barabarani

MWANAFUNZI: Somo la hesabu lifutwe mashuleni

MFANYABIASHARA:TRA ibinafsishwe

WANACHUO: Bodi ya mikopo imilikiwe na Dowans

WAKAZI WA MBAGALA/GONGO LA MBOTO: Ghala la mabomu lijengwe ikulu

WANA NDOA: Vyeti vya ndoa viwe na 'expiry date'!

Wanasiasa : wananchi wasifanye kazi bali wapewe pesa za matumizi na serikali kila siku.
 
wewe jamaa unashangaza kweli jana wewe umetoa post ya uchochezi kwamba Zitto hawezi kuwa raisi wa Tanzania sasa nashangaa leo unasema CHADEMA watulie wakati wewe ndiye unawachonganisha

kumbe na wewe umemgundua. Huyo lazima atakuwa anti-ZITTO tu , aibu yake. Tulivu ya CDM ni mpaka ZITTO awe Rais vinginevyo, ukabila, udini na uamajimbo utawatafuna tu.
 
Mkae mtulie kwa upendo na heshima. Muongee kwa staha na kwa kujenga hoja.Mheshimiane nyinyi kwa nyinyi.Tumieni Katiba yenu kumaliza hoja yoyote itakayoletwa mezani. Msikubali kupambanishwa na watamani madaraka kama wafanyavyo wenzenu wa 'jembe na nyundo'.

Mwenyekiti Mbowe na timu yako ya uongozi wa kitaifa,shughulikia matatizo ya chamani mwako kikatiba.Wananchi wa Tanzania wameshawaelewa hoja zenu.Wanasubiri 2015 wawape nchi muiendeshe.Bungeni,onesheni kuwa mnaweza.Majukwaani,jengeni hoja za kiukombozi. Magazetini,andikweni kwa wema.Runingani,tangazweni mnavyojisambaza kwa hoja mujarabu na umati wa Watanzania walio na matumaini nanyi.

Mwaka 2015,simamisheni mgombea ambaye hata uchakachuzi hautampora ushindi wake. Iwe wa Urais,ubunge au udiwani.Watanzania wanawangoja.Msiwaangushe. Mkae mtulie na hatari zote zisiwafikie.

Nangoja ukombozi...

CDM bia ZITTO haiwezekani.
 
Makundi mbalimbali yakijibu maswali kwamba "NI KITU GANI WANGEPENDA KIWEPO KWENYE KATIBA MPYA"?

Majibu yalikuwa hivi:

DEREVA:Traffic wasiwepo barabarani

MWANAFUNZI: Somo la hesabu lifutwe mashuleni

MFANYABIASHARA: TRA ibinafsishwe

WANACHUO: Bodi ya mikopo imilikiwe na Dowans

WAKAZI WA MBAGALA/GONGO LA MBOTO: Ghala la mabomu lijengwe ikulu

WANA NDOA: Vyeti vya ndoa viwe na 'expiry date'!

Like x2
 
Akina Mama walioolewa: Akina baba waonyeshe Salary slip zao mwisho wa mwezi!
 
Wanasiasa : wananchi wasifanye kazi bali wapewe pesa za matumizi na serikali kila siku.
Mkuu nimeipenda hiyo.... watanzania tuwe tunalewa kila wakati ili kiingereza kipande hasa kwa wanachuo.... ha ha ha mkuu tunajaribu kuonyesha jinsi baadhi ya watanganyika na wazanzibari wanavyoona kama katiba Mpya ndio suluhu ya matatizo yao... kila mtu oh... katiba mpya! WHAT IS KATIBA MPYA?
 
kwani chadema kuna fujo?
 
Back
Top Bottom