Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 26,520
- 40,215
Inawezekana kabisa CHADEMA wasiwe na nia mbaya juu ya kusudio lao la kuunda kikosi maalum cha ulinzi wa viongozi wake na chama kwa ujumla. Lakini ni budi kutoka nje ya box na kufikiri kwa mapana juu ya azimio hili pamoja na makandokando yake.
Tulisikia juzi kupitia BBC namna msemaji wa polisi alivyokosa stand kuhusu azimio hilo, na alivyokuwa anarudia rudia maneno badala ya kujibu hoja za msingi. Pia jana tumesikia kauli ya Kikwete huko huko BBC akiwalaani CHADEMA kwa kusudio hilo. Na si ajabu tutaendelea kusikia watu wengi wakitoa dukuduku lao kuhusu hii move ya CHADEMA.
Ninaamini kwamba CHADEMA wanajua wanalolifanya, lakini hatuna budi kufikiri kwa kina kuhusu hili.
Kwa kuzingatia pointi hizo hapo juu, ningependa sasa kumshauri Mbowe na Kamati Kuu CHADEMA kuangalia yafuatayo
Tunaweza kushabikia kwa wingi wetu kufurahia hii move lakini tukajastuka jahazi limezama mazima. Inawezekana kabisa kwamba waliotoa ushauri huu wa kiufundi wasiwe na nia njema na CHADEMA kwani wanaelewa fika kwamba pamoja na CCM kumiliki vikosi vyake vya ulinzi lakini makosa mawili hayarekebishi kosa.
CHADEMA muda mnao, naamini mtatafakari upya na kuja

- Ni kweli kwamba CCM wanamiliki kikosi chao Green Guard ambacho ni MILITARY trained youths kwa minajili ya ulinzi wa ndani wa chama, na kupitia matukio mbalimbali hata ushahidi wa viapo kuhusu uhusika wao kwenye matukio yanayohatarisha uhai na usalama wa wengine ilimradi maslahi ya chama yatimie.
- Siyo siri kwamba since Mwenyekiti wa Taifa wa CCM ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa vikosi vya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, haikuwa ajabu kwa yeye na chama chake kuhakikisha wanatumia nafasi hiyo kumiliki majeshi na mwenendo wa majeshi ya nchi kwa favour ya chama chake baada ya kugundua kuwa hawana jipya wala uhalali wa kuendelea kuongoza nchi. Haiyumkiniki kwamba wasaidizi wake ama yeye mwenyewe wamekuwa wakitoa maelekezo ya nini kifanyike na nani afanywe nini ili kulinda reputation ya CCM.
- Katiba ya Jamhuri ya Muungano wala sheria za nchi havijatoa kibali kwa chama chochote cha siasa kilichosajiliwa nchini kumiliki vikosi ama majeshi kwa kusudio lolote lile.
Kwa kuzingatia pointi hizo hapo juu, ningependa sasa kumshauri Mbowe na Kamati Kuu CHADEMA kuangalia yafuatayo
- Kwa kuwa CCM inamiliki kikosi chake cha ndani cha ulinzi, na kwa kuwa CCM inatumia vibaya dhamana yake ya uongozi wa nchi kwa kuyashurutisha majeshi na vikosi vya jamhuri kutimiza matakwa ya CCM [Viapo vya watumishi wa vikosi vya jamhuri [siri] vinaweza kudhihirisha hayo]. Ingelipasa CHADEMA kuliweka hilo bayana kwenye uso wa sheria ili kama sheria [mahakamani] itatafsiriwa kuifavor CCM basi ndipo waje na kusudio la kuunda kikosi chao pia.
- Inawezekana mbinu zote za kuimaliza CHADEMA zimegonga mwamba sasa kinachotumika ni ushawishi ili chama kifanye maamuzi yatakayopelekea kimalizike kisiasa. Kama ni ushauri mmepewa na mtu wa ndani fanyeni study ya faida na hasara zake pia mtafute upenyo kwenye sheria mbao mnaweza kutumia kuanzisha hicho kitengo bila kuonekana mnavunja sheria na katiba.