CHADEMA...mbona mnameza matapishi??

CHADEMA...mbona mnameza matapishi??

Lakini sidhani kama ni busara kuja humu kwa ajili ya kutetea vyama....we need to be free thinkers
 
Kwa taarifa yako hakuna kikao chochote kiwe cha ndani au cha hadhara ambacho CHADEMA wamewahi kutangaza kumkubali JK. Kimsingi wanachama tunashangaa kwa nini kila mara chama kinatoa msimamo huu na kinatekeleza mwingine?? Je kuna haja yeyote ya kuendelea kuamini misimamao ya viongozi wa chama?? Pia Chadema ni ya wanachama na si viongozi tu so kama walivyotutangazia kuwa hawamkubali raisi vivyoivyo watutangazie kuwa wameanza kumkubali na wataendelea

Songoka,matendo yanatangaza zaidi kuliko maneno.
 
Mwenye hii hoja ni mbuz tu? Walitaka ktba mpya mchakato ukaaza, inshu ya tume ikaundwa sasa wewe unaongea nn kanye kwanza.
 
Mbona hata rais akitingwa huwa anawaita kwa mazungumzo?? Nae rais huwa anajua cdm ni babu kubwa ndio maana anawaheshim.
 
Mkuu, wewe ulitaka hayo uliyosema niyahoji wapi? mbona unahangaika kuandika kitu ambacho mantiki yake huijui. ukweli ni kuwa, kama mtoa mada alivyosema, CHADEMA wamelamba matapishi yao

Wewe si umesema ni mwanachama wa Chadema?Wewe ni mwanachama gani ambaye hujui sehemu ya kuhoji masuala ya chama chako? Kwani ofisi za Chadema ziko JF? Mapandikizi utayajua tu.
 
Wewe si umesema ni mwanachama wa Chadema?Wewe ni mwanachama gani ambaye hujui sehemu ya kuhoji masuala ya chama chako? Kwani ofisi za Chadema ziko JF? Mapandikizi utayajua tu.

sijawahi kuwa mwanachama wa CHADEMA na wala sijawahi kuota au kufikiria kuwa mwanachama wa chama hicho. Nadhani umenichanganya. hakuna mahala nimejitangazia kuwa ni mwanachama wa chama hicho
 
Baada ya uchaguzi 2010 chama cha DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) hawakukubaliana na matokeo yaliyompa ushindi ndugu KIKWETE. Wakakataa kumtambua kama RAIS wa JMT. Hawakuishia hapo tu bali hata alipotinga bungeni wote walitoka nje ili kudhihirisha kutokumkubali JK kama kiongozi na rais wa JMT.

Wakiongozwa na kauli mbiu ya PEOPLES POWER, Chadema walijipambanua kuwa maamuzi na maswala muhimu yote yataamuliwa na wananchi wenyewe na wananchi ndo watakuwa mahakama kwa kila jambo la serikali.

Mpaka sasa naandika mada hii, sijawahi sikia CHADEMA wakiutangazia uma kuwa wamemtambua Jakaya Mrisho Kikwete kama rais ya Jamuhuri hii na wanautambua ushindi wake wa mwaka 2009/2010
Kwa msingi huu najiuliza yafuatayo/ na wanajavi mnisaidie.

  • Chadema wameenda IKULU mara mbili kutafuta eti BUSARA ya raisi katika maamuzi mabovu yaliyotolewa na bunge kuhusu muswaada wa KATIBA mpya.Je walienda kuonana na nani?? na Kama ni RAIS je ni yuleyule wasiyemtambua?
  • Kama walivyotoka katika ile hotuba ya kwanza nini kiliwazuia jana kuto toka tena?? au huyu kikwete si yule wa wakati ule
  • Je CHADEMA kwa matendo yao yanayopingana na kauli walizotoa hawaoni wanatuchanganya sisi wanachama?
  • Je chadema wanapokuwa majukwaani na kusema RAIS inchi imemshinda huwa wanamaanisha RAIS yupi??
Kwa misingi hii napenda kuwashauri viongozi wa chadema kuwa ni muda muafaka sasa waitishe KIKAO na waandishi wa habari na kuutangazia uma wa watanzania kuwa wanaifuta kauli yao waliyoitoa 2010 na wanamtambua JK kama RAIS halali wa JMT, na wataendelea kumtambua mpaka muda wake utapoisha. Or else waache unafiki wa maneno wakati matendo ni kinyume.Mimi ka mwanachama nasikitishwa na misimamo isiyotekelezeka ambayo hutolewa mara kwa mara na VIONGOZI. Hii ni kama kulamba matapishi yako mwenyewe

usipoteze muda kujadili hili genge la wasaka tonge.
 
Mwenye hii hoja ni mbuz tu? Walitaka ktba mpya mchakato ukaaza, inshu ya tume ikaundwa sasa wewe unaongea nn kanye kwanza.

walisema hawamtambui rais. inakuwaje wanamfuata ikulu mara kwa mara?
 
sijawahi kuwa mwanachama wa CHADEMA na wala sijawahi kuota au kufikiria kuwa mwanachama wa chama hicho. Nadhani umenichanganya. hakuna mahala nimejitangazia kuwa ni mwanachama wa chama hicho

Kama wewe si mwanachama wa Chadema basi mambo ya Chadema yanakuhusu nini? Mbona huongelei masuala ya ufisadi na rushwa ndani ya ccm? Mbona huongelei mambo ya madawa ya kulevya yaliyojaa ndani ya ccm? Mbona huongelei majangili waliojaa ndani ya ccm? Ccm imejaa mambo ya ajabu mengi,mbona huyahoji unarukia mambo ya Chadema?
 
ZITTO ANAMTAMBUA RAISI KIKWETE...hii ni moja ya nashtaka
 
Back
Top Bottom