utaifakwanza
JF-Expert Member
- Feb 1, 2013
- 14,193
- 2,815
Kila uchao CHADEMA inazidi kuchekesha. Tulikuwa na chadema iliyojinasibu kupigania maslahi ya wananchi na kupiga vita rushwa na ufisadi leo hii imegeuka kituko kwa kukumbatia mafisadi na wala rushwa. Imekuwa ni chama maslahi badala ya chama cha wananchi maskini.
Hivi karibuni tulikuwa na chaguzi ndogo katika majimbo matatu nchini. CHADEMA ilisusa chaguzi hizo kwa maelezo kuwa hakuna demokrasia. kumbe ni maslahi binafsi ya baadhi ya viongozi.
Hawakujali maslahi mapana ya wananchi pamoja na demokrasia katika nchi yetu. Hawakuwa na maslahi na wananchi wa majimbo yaliyokuwa yanarudia uchaguzi.
Leo hii chama hiki kinashiriki uchaguzi wa jimbo la kinondoni na siha bila kueleza sababu za msingi zinazowaingiza kwenye ucgauzi huo na zile zilizowafanya wasishiriki songea mjini, Singida Kaskazini na Longido ambapo CCM imeshinda kwa kishindo.
Hii yote ni kwa sababu viongozi walitanguliza maslahi yao binafsi badala ya maslahi ya wananchi. inauma sana