Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,033
- 144,386
Hili jambo kama sikosei leo naliongea kwa mara ya pili hapa JF.
Viongozi wa CHADEMA, mtu kukataa rushwa ya milioni 200 na hapo hapo akatoa tuhuma hizo hadharani kupitia vyomba vya habari kama huyu Meya wa Iringa, si jambo dogo ambalo linapaswa kuacha lipite hivi hivi.
Mtu kama huyu bila shaka ana ushahidi vinginevyo wamshitaki na wakishindwa kufanya hivyo, nyinyi kama chama chukueni hatua ya kumpongeza kwa kumpa ama tuzo au nishani maalumu itakayotolewa na chama na hili lifanyike kwa kila diwani atakaewza kufanya jambo kama hili la kizalendo na tuzo au nishani hiyo akabidhiwe mbele ya waandishi wa habari.
Vile vile nashauri mbunge Joshua Nassari na mwenzake Godbless Lema nao chama kiwaandalie nishani ya uzalendo na ushujaa kwa kutoa hadharani ushahidi wa tuhuma za kununua madiwani mkoani Arusha na kukabidhi ushahidi huo katika mamlaka husika (TAKUKURU).
Maadamu wameshindwa kuwashitaki kwa kuwachafua, basi huu kwetu ni ushahidi kuwa tuhuma walizotoa zilikuwa za kweli maana wazungu wanasema, "silence means yes."
Na Ili kuokoa gharama, hawa wote niliowataja na wengine ambao wamekuwa wakieleza hujuma hizi kupitia vyombo mbalimbali vya habari, wote kwa pamoja; wapewe nishani au tuzo hizo katika tukio moja kubwa la pamoja litakaloandaliwa na chama huku mkitoa mialiko kwa viongozi wa vyama vingine na wa taasisi zingine watakao kuwa tayari kushiriki katika tukio hilo wakiwemo na watu binafsi.
Ifike mahali tutambue uzalendo wa watu wa aina hii katika chama kwa kuwapa heshima wanayostahili kama ilivyofanyika kwa Lissu kukabidhiwa sera mpya za chama akiwa nje ya nchi bila shaka ikiwa ni heshima aliyopewa na chama chake.
Ni ushauri tu na hii si mara ya kwanza.
CHADEMA Makao Makuu,mpeni tuzo diwani Eliaf Michael - JamiiForums