CHADEMA machoni mwa jamii ya watanzania

Ritz

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2011
Posts
56,807
Reaction score
46,308
Wanaukumbi.

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambacho sasa hivi kipo chini ya Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dr. Slaa, kinazidi kupoteza dira na mwelekeo wake wa asili, na hivyo kuharibu sifa za chama hicho kama kilivyosifiwa na Mwalimu Nyerere enzi za uhai wake.

Badala ya kuwa chama cha siasa kinachotumia hoja na ustarabu kutafuta ushawishi kwa umma, Chadema ya sasa imegeuka kuwa chama cha kiharakati kisichoheshimu hata mamlaka ya nchi kwa mtindo huu Chadema hakiwezi kufika popote kama chama cha siasa, lazima Mbowe na Dr. Slaa waambiwe ukweli, kimsimamo wapo tofauti na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zitto Kabwe, ambao ni miongoni mwa makada wachache wazalendo na watiifu.

Zitto, ambaye ana kundi kubwa la vijana pamoja na baadhi ya wazee amekuwa akitengwa kushiriki kwenye kazi za chama kama vile operesheni za vuguvugu za M4C, operesheni Sangara, toka kumalizika kwa uchaguzi mwaka 2010, Zitto amekuwa akitofautina na misimamo kadhaa ya chama chake, ambayo inaonekana siyo ya kisiasa ni ya kiharakati zaidi. kama suala la kumtabua rais Kikwete kama rais halali wa Tanzania, na mwaka 2010 Dr. Slaa, hata wabunge wenzake walipoweka azimio la kususia hotuba ya rais bungeni kutoka nje, Zitto aliamua kujitenga nao, viongozi wa Chadema nao wanazidi kumtenga Zitto, hata majuzi walipopata mwaliko Ikulu kutoka kwa rais Kikwete, kujadili masuala ya katiba walienda peke yao, suala la ukaguzi wa mahesabu ya vyama vya siasa ambalo linafuatliwa na Kamati ya Bunge ya Mahesabu ya serikali PAC, Chadema wanaona kama ni suala la Zitto.

Chadema sasa imeshindwa kuwajenga vijana kuwa na moyo wa uzalendo wa nchi yao, na badala yake imekuwa ikiwahamasisha kuvuruga misingi ya uzalendo na kutotii sharia na mamlaka zilizopo, pia wengi wa wabunge wa Chadema ni watiifu kwa Mbowe na Dr. Slaa, ni wale wanaodaiwa kuingia ndani ya chama kwa lengo la kusaka ubunge tu, na maslahi huku wakiwa hawana historia yoyote ya mchango wao wa kujenga chama.

Hali hii ndiyo imefanya Chadema sasa ionekane machoni mwa jamii ya watanzania kama chama cha vurugu na ubabe, hali inawafanya pia wananchi wasite kukiamini kwa kukikabidhi madaraka makubwa ya kuongoza dola.
 
Kutofautiaana kimsimamo ni jambo la kawaida.
Kisicho cha kawaida ni mtu mmoja kutofautiana kimsimamo na walio wengi kwa kila jambo.
Hivi jumbe alivyotofautiana na wenzake ilikuaje? Walimchekea?
 
Hivi ccm wamebaki na uasili wake?
Wanamtandao
Wanamaslahi
Wanaccm asilia

Ipi mwalimu aliiacha?
 
Chadema kimeundwa kwa misingi ya kilaghai na udanganyifu,
kwa sasa chadema siyo chama ni sacos ya kukopeshana bila kulipa.
 
Naomba chadema wayakumbuke maneno haya,
chama cha ukoo kitafia kwenye ukoo husika tusubiri mtaniambia wenyewe.
 
bila shaka hata mh Zitto mwenyewe ana kushangaa kwa kuropoka.

kila chama kina mipango yake.
Kwa taarifa yako utawagombanisha wajinga tuu.
 
Last edited by a moderator:
Umenena Aunt Ritz. Nenda Lumumba wanakusubiri wanaume wako.
 
Ni kweli kabisa chadema kimefifia sana zile nguvu walizokuwa wakijilabu hazionekani tena ,mvuto umepotea ,wamebaki hapa JF tu wakijaribu kusifiana wenyewe kwa wenyewe ,mi nilijua tokea zamani kuwa hiki si chama.
 
hivi ni kundi gani kubwa la vijana na wazee linalomuunga mkono zito?labda kanda ya magharibi,kanda ya nyanda za
juu(mbeya,rukwa,iringa),kusini.mashariki.etc hakuna kitu kama zito!pole sana mtoa mada ,anzisha mada nyingine
hii haiwezi kushika maji!
 

Kwa akili yako tofauti ya mitazamo kati ya viongozi ndio chama kimekosa dira, ni wapi viongozi wa chadema wamefundisha vijana kutotii sheria za nchi ? hiv sheria za nchi unazijua kweli wewe? au umesahau kwa kuwa umebwia unga? majib please
 

View attachment 118285 View attachment 118286 View attachment 118287 View attachment 118288 View attachment 118289

Hapo tafakari kwa kina chama chenye vurugu ni kipi?
-. CCM mnaongoza kwa NGONO, UGOMVI ndani na nje ya chama
 

Pole kijana ikulu lazima muiage. Baba yako keshasoma alama za nyakati ndo maana anaacha katiba ambayo ni mwiba kwa wanamagamba.
 
....

.......Mtindo wa kutupia mapicha nimeupenda sana!!!!!
 

Mkuu naona hii ni wishfull thinking au wikiendi imeanza mapema.
 
Utumbo mtupu!!!! Bangi ni kitu kibaya sana!!!!!
 
Vijana wa Chadema kutoka mikoa mbali mbali isipokuwa maeneo ya kaskazini, wameapa na kuweka wazi kuwa hawatakubali yaliyotokea mwaka 2009 kukwata jina lake kugombea Uenyekiti.
 
Hivi mnazi wa Simba anaweza kuisifia Yanga au kuiongolea yanga kwa mazuri? Tafakari chukua hatua.
 
Kutofautiaana kimsimamo ni jambo la kawaida.
Kisicho cha kawaida ni mtu mmoja kutofautiana kimsimamo na walio wengi kwa kila jambo.
Hivi jumbe alivyotofautiana na wenzake ilikuaje? Walimchekea?
Kamanda hauwezi kupinga kuwa Chadema hakuna uhasama wa kisiasa kati ya Zitto na kundi la Mbowe na Dr.Slaa.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…