CHADEMA M4C Kwa Wazungu!

CHADEMA M4C Kwa Wazungu!

Wazungu..wazungu ndo nini? Jamani natambua nafasi ya mataifa yaliyoendelea katika influence za siasa za nchi zinazoendelea,lakini mwisho wa siku nguvu ya umma ndo inakuwa last say,usipende kuwakatisha tamaa watanzania kwani vijana wadogo wenye 18+ wana hamu sana ya kushiriki uchaguzi wa mwaka 2015 na hao ndo wataipa cdm ushindi,najua nguvu kubwa ya uchakachuaji itawekezwa especially vijijini lakini nasi cdm tujipange kufanya hivyo pale inapobidi kwani jino kwa jino ndo mtazamo wa vyama vingi,
Vijana wenzangu chama chetu kiko makini sana,kwani mbowe,slaa,prof safari nk si wageni wa siasa za afrika wanajua nini chakufanya ili magogoni iwekwe kibindoni,naomba tuwe na imani na viongozi wetu pia nasi tukifanya majukumu yetu kwa moyo tukitawaliwa na wazo la ukombozi wa tz 2015 kutoka mikononi mwa mkoloni mweusi.
Vijana tulieni,maboresho ya daftari la wapiga kura ndo mpango mzima,tutatumiana sms nyingi za kutuhamasisha tukajiandikishe then tuone 2015 nafasi ya nguvu ya umma Vs nguvu ya mzungu (ccm)
 
Halafu wawaambie wazungu serikali ya JK ni mbaya kwasababu gani?

Mimi sijui!
Ila kama wanataka waing'oe CCM ni lazima kwanza wakubalike na hiyo inayoitwa International Community" ambayo mpaka sasa CCM wamefanikiwa sana kuiweka upande wao ingawaje sisi ndio tunaumia lkn nani anajali Ngedele akiumia hata hivyo, sasa watawashawishi vipi Wazungu kwamba wao ni partner bora kuliko CCM hilo juu yao wenyewe CHADEMA kujua!
Kumbuka kwamba Wazungu sasa hivi wanawekeza sana nchini kwetu hasa kwenye Madini na Gesi, sasa ni muhimu sana wao kujua ni nani anayekuja 2015 na atakuwa sera gani, kama wao CHADEMA waking'ang'ania Sera za akina Chavez itakula kwao!
 
Wazungu ndo nani hao?

Maana isije kuwa wazungu unaowasema wewe tofauti na anaowajua Kiranga.

Hata Jerry Springer type trailer trash na hillbilly hicks nao wanaweza kusema ni wazungu.
 
Nawashauri CHADEMA kama wanataka kushinda Uraisi,wapeleke M4C kwa Wazungu kwanza, wakifanikiwa huko ndio waje wamalizie huku kwetu!
Natoa huo ushauri kwa maana Wazungu ndio wanaamua nani awe Raisi wetu, na sio sisi Ngedere Wananchi, hilo la kupiga kura ni kuzuga tu lkn mara nyingi Raisi huwa ameshaamuliwa na Wazungu!

wewe ndo ngedere mwenyw tena unapaswa kutuomba radhi watz wote kwa kutuita hvyo! tuige mfano kwa wenzetu wa kenya! Nch za magharibi walimtaka Odinga lakn wenye nchi wakamtaka Kenyata na wamefaulu! Acha huo ujinga, nyie ndo akina mangungo wa msovero, wasaliti na waoga kama nin....?! Kaa mbali na sis.
 
Toa majibu ya nini tufanye wana CDM, hata serbia ni wazungu kama je tufuate sera zao
 
mleta mada hakika una hoja. That's true mkuu japo umeleta tafakuri yako kwa namna ya utani vile
 
wewe ndo ngedere mwenyw tena unapaswa kutuomba radhi watz wote kwa kutuita hvyo! tuige mfano kwa wenzetu wa kenya! Nch za magharibi walimtaka Odinga lakn wenye nchi wakamtaka Kenyata na wamefaulu! Acha huo ujinga, nyie ndo akina mangungo wa msovero, wasaliti na waoga kama nin....?! Kaa mbali na sis.

Mimi sio Msaliti, kwanza kama ungenijua ni kinyume chake, ila naongea ukweli tu, unauma na unakufanya uhamaki, lkn halibadilishi chochote ukweli unabaki kuwa ukweli, kama ulifikiri
Raisi Bw. Kikwete anaongoza nchi kwa matakwa yako wewe uliyemchagau unajidanganya, anayeamua nchi iendeshwe vp ni Wazungu, hata Bungeni kwetu kulikuwa na mjadala kuhusu hilo, Wabunge walikuwa wanahoji, Bajeti yetu inapelekwa kwanza kwa Wazungu wanaipitia wakiikubali ndio Ngedele tunaletewa kuijadili Bungeni, tung'ang'ania kwenye TV kuangalia bajeti kumbe ilishapitishwa na Wazungu

Hata kwa Wakenya hakuna kitu hapo, Wazungu ndio wanaamua, wakiamua Bw.Raila awe raisi wa Kenya na itakuwa hivyo, hata kama Bw.Uhuru Kenyata ndio ameshinda kiuhalisia, na ukiona Bw.Uhuru Kenyata anakuwa Raisi basi ujue ameshawaangukia na kuwaahidi maslahi makubwa kiuchumi, wewe huwezi jua kinachooendelea sasa hivi huko utashangaa kusikia Bw.Raila naye yumo kwenye Serikali ya Bw. Kenyata tena kwa cheo kikubwa ingawaje ameshindwa Uchaguzi na hakupaswa kupewa cheo chochote!

Toa majibu ya nini tufanye wana CDM, hata serbia ni wazungu kama je tufuate sera zao

Jibu gani tena nitoe, si nimeshasema waepeleke M4C kwa Wazungu, huko hakuna kulalal mpaka kieleweke ifanyike!

Hao Waserbia, inategemea kama ni wanachama wa Umoja wa Ulaya inabidi, kwa maana kwenye Umoja wa Ulaya kila mwanachama ana kura sawa haijalishi kama ni mdogo au mkubwa!
 
mada imenipozea mood ya kuchangia Kijakazi ulipochomeka neno ngedere!
 
Last edited by a moderator:
itabidi tuongee nao tuwakabidhi gesi ya Mtwara bila mkataba wowote na wajipangie kila kitu wao. wenyewe..
 
Nawashauri CHADEMA kama wanataka kushinda Uraisi,wapeleke M4C kwa Wazungu kwanza, wakifanikiwa huko ndio waje wamalizie huku kwetu!
Natoa huo ushauri kwa maana Wazungu ndio wanaamua nani awe Raisi wetu, na sio sisi Ngedere Wananchi, hilo la kupiga kura ni kuzuga tu lkn mara nyingi Raisi huwa ameshaamuliwa na Wazungu!

mbona umejizarau hivyo?
 
Kila kitu kinaenda vizuri makamanda,Huku nje tumeshawasilisha kila kitu kipo mezani [capital hill]washington DC.Na mitaani kwenye vibanda vya habari kuna picha nyingi zimewekwa na zinaendelea kuwekwa kuhusu mauji yanayoendelea huko.Na Dr slaa alitakiwa kuongea kwenye redio ya demokrasia hapa washington dc.hii redio inasikilizwa na watu wengi wa siasa,haki za binadamu na wengine .Kwa hilo hapa Washington limepita.Tunakandamiza vibaya sana mkuu
 
Huyu aliyeleta hii topic amekosea kuipa ujumbe vizuri even though its a reality.

Mi nadhani tunachohitaji nikujitambua internationally, kama tulivyoanza sasa kujitambua nationally. Unfortunately, katika kujitambua huko nationally, we have also invented makabila na dini zetu as the way of identifying ourselves.

Hii itatuchukua muda kuaanza harakati za kujitambua internationally. Mfano wa nchi ambazo zimekuwa kufikia stage ya kuanza kujitambua internationally ni Iran with his nuclear threat!
 
Nawashauri CHADEMA kama wanataka kushinda Uraisi,wapeleke M4C kwa Wazungu kwanza, wakifanikiwa huko ndio waje wamalizie huku kwetu!
Natoa huo ushauri kwa maana Wazungu ndio wanaamua nani awe Raisi wetu, na sio sisi Ngedere Wananchi, hilo la kupiga kura ni kuzuga tu lkn mara nyingi Raisi huwa ameshaamuliwa na Wazungu!

na ndio sera zao za kutawala dunia nzima, kwasababu kwa sasaivi hawa jamaa hawana kabisa rasilimali, na mategeo ni kutoka bara la Africa, hivyo kwa mbinu yoyote lazima wahodhi rasilimali za Afrika, na mifano tunayo kwa Mugabe na Gadafi, na wenzetu kubwa zaidi uchumi unapiganiwa na kulindwa na majeshi. hivyo tuwe makini sana na hila za wazungu kutuchagulia viongozi
 
Back
Top Bottom