Nawashauri CHADEMA
kama wanataka kushinda Uraisi,wapeleke M4C kwa Wazungu kwanza,
wakifanikiwa huko ndio waje wamalizie huku kwetu!
Natoa huo ushauri kwa maana Wazungu ndio wanaamua nani awe Raisi wetu,
na sio sisi Ngedere Wananchi, hilo la kupiga kura ni kuzuga tu lkn mara
nyingi Raisi huwa ameshaamuliwa na Wazungu!
Aaaah wapi mbona Kenya wameshindwa?? Uhuru Kenyata ameshinda licha ya ubalozi wa Uingereza kutoa vitisho.
2015 tutalinda kura zetu na ushindi tutapata, huyu mkoloni mweusi lazima tumtoe, mweupe alishatoka zamani
Kwa hiyo CCM wanaendeleza hayo maslahi ya wazungu?Ya Kenya hawajashindwa subiri kwanza uone mchezo unavyokwenda, na hapo kuna mawili, ukiwaona kimya ujue Bw. Uhuru ameshafanya nao dili na wamekubaliana au bado wanajadiliana ni jinsi gani Bw.Uhuru atakavyolinda maslahi yao, kama kuendeleza vita Somalia, Mali na kwingineko, Bw. Uhuru akikataa basi moto wake utauona siku chache zijazo!
Na hapa kwetu hivyo hivyo bila Wazungu kukubali hauwezi kuwa Raisi wa TZ, ni vizuri CHADEMA wakapeleka kwanza M4C kwa Wazungu, wao ndio wanaamua, wakiaamua hata kesho CCM itaondoka aidha kwa maandamano au kwa hiari, na wasipoamua CCM haitaondoka hata ishindwe kwa asilimia 80%, huo ndio ukweli!
Kwani Mengi ni wa chama gani cha siasa?Baada ya skendo ya mengi na ndugu yake kuzulumu shamba kwa wanzungu sidhani kama kuna mzungu anataka kudeal na jamaa wa mlimani tena.
Mkuu, kwa hiyo una maanisha kura zinapigiwa na kuhesabiwa Washington? Ni dhahiri mnahitaji tuition ili muweze kuelewa vizuri nini maana ya NGUVU YA UMMA.Mtoa mada nakusifia kwa mtazamo wa sera za nje. Cdm hawajui kuwa nguvu ya kushika nchi katika nchi maskini inatoka Washington. Ukifika hapo ndipo utagundua kuwa cdm haiwezi kushika nchi 2015. Katika matamko yao wanafanya makosa ya ki-stratejia kwa kupambana na wawekezaji, kuuona uwekezaji ni kama sehemu ya ufisadi.
Kama tukishindana na ccm kuwa please wazungu,nadhani hatutafanikiwa kwasababu ccm wameshauza kila kitu kwa bei chee.
Na ili wakubalike na wazungu inatakiwa wafanyeje?
Hakuna jinsi! Bila kuwafurahisha Wazungu, hauendi popote, watakushinda tu hata ufanye nini!
Hivyo CHADEMA wanahitaji kukubalika kwa Wazungu kwanza bila ya hivyo, safari yao hawatafika! Ndio ukweli mchungu wenyewe huo!
Halafu wawaambie wazungu serikali ya JK ni mbaya kwasababu gani?Wapeleke M4C!