SCHRUMBEGER
Member
- Jan 29, 2013
- 12
- 2
Kumeanza kutokea tabia isiyokuwa ya kuridhisha kwa baadhi ya watu hasa wale wenye nia ya kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu 2015 kupitia CHADEMA. Wamekuwa kama CCM, maana wameanza kugombania majimbo, wameanza kutengeneza fitini mara huyu ni pandikizi n.k. Ni vema tukaiacha demokrasia ichukue nafasi yake ili tuweze kujitofautisha na wale wa upande wa pili.
Niwakumbushe wenzangu kuwa kazi ya ujenzi wa chama ni kubwa, haiwezi kufanywa na mtu mmoja katika jimbo/wilaya na CHADEMA ikaweza kupata ushindi 2015. Kwa mawazo yangu naona ni vizuri wakati wa M4C mkoani Kagera tukayazungumzia haya yafuatayo:
a) Hakuna mwenye jimbo/wilaya, jimbo/wilaya ni mali ya wananchi/wapiga kura.
b) Ni vema tukajua kuwa kura ya maoni ndiyo itakayotumika kutupatia mgombea wa nafasi yoyote kwa mujibu wa taratibu za chama.
c) Tusidhani kuwa mtu kuwahi kujiunga CHADEMA ni kigezo tosha cha kuaminiwa. Aliyeingia CHADEMA leo kwa nia ya kweli ya kimabadiriko ni bora kuliko aliyeingia CHADEMA miaka kumi iliyopita lakini bado hajaamini katika mabadiliko ya kweli!.
d) Mtu kuwa karibu na viongozi wakuu wa chama na makao makuu siyo hoja ya kuhalarisha mtu kuvunja taratibu za chama kwa maslahi yake.
e) Tabia ya kuchafuana kwa meseji, fitina, majungu na mizengwe ni tabia ya CCM ambayo haiwezi kumsaidia mtu kukubalika katika jamii yake, kwani kwa mbinu hii hata CCM wameshindwa. Turudi kwenye falsafa ya chama i.e Nguvu ya Umma ndiyo pekee itakayomsaidia mtu.
f) Kurubuni viongozi wa jimbo/wilaya kwa namna yoyote ile ili wavunje taratibu za chama kwa makusudi kabisa kwa ajiri ya kumpendelea mtu ni Rushwa. Mtu huyo hawezi kupata situ ridhaa ya chama bali pia ridhaa ya wananchi kuwaongoza.
g) Kutumia uhusiano wa kimapenzi na viongozi wa chama kwa kutaka kupewa kipaumbele na upendeleo katika shughuli za chama pia ni Rushwa. Mtu huyo hawezi kupata situ ridhaa ya chama bali pia ridhaa ya wananchi kuwaongoza. Pia ni kukidharirisha chama na wewe wenyewe.
h) Watu wote wenye nia ya kugombea wajitokeze mapema ili watu wawajue waraka no.2 wa katibu mkuu wa 2011. Watu watawajua kwa kushiriki katika shughuli za kijamii, kimaendeleo n.k huku tukikijenga na kukiimarisha chama. Hili haliwezi kufanywa kwa kuitisha tu vikao vya kamati tendaji ya jimbo na kutoa posho tukadhani eti watu wametujua. Twende kwa wananchi maana wao ndo wenye maamuzi lakini pia ni wengi (nguvu ya umma) kuliko kamati tendaji!.
i) Tujitofautishe na CCM ambayo watu hasa wazee vijijini walishaichukulia ni kama dini/imani fulani katika mioyo yao. Kwa hiyo mbinu zao za kukijenga na kukiimarisha chama chao lazima zitofautiane kabisa na zile za CHADEMA.
Ikumbuke kuwa It is very difficult to exercise freedom in poverty