CHADEMA: Lowassa ni kiongozi mwenye kuthubutu

CHADEMA: Lowassa ni kiongozi mwenye kuthubutu

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
[h=2][/h]JUMATATU, MACHI 25, 2013 05:11 NA ELIYA MBONEA, KARATU


MWENYEKITI wa Halmashauri ya Karatu na Diwani wa Kata ya Ganako (CHADEMA), Lazaro Maasai, amesema Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa ni kiongozi pekee katika nchi hii mwenye uthubutu wa kuagiza.

Kauli hiyo aliitoa mjini hapa jana, katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Chuo cha Afya katika Hospitali ya Wilaya ya Karatu inayomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kwa ushirikiano na Serikali.

Alikwenda mbali zaidi na kumtaka Lowassa asikate tamaa kuwasaidia Watanzania akiamini ipo siku moja Mungu atamsaidia kutimiza ndoto zake.

“Nina amini Mungu atakupa afya zaidi ili ndoto zako ziweze kutimia, kwani ni viongozi wachache nchini wenye uthubutu wa kuagiza,” alisema Maasai.

Alisema mwaka 2007, Lowassa akiwa Waziri Mkuu aliwahi kuwaita ofisini kwake wenyeviti wote wa Halmashauri na kuwapa maagizo ya kuhakikisha hakuna mtoto wa Mtanzania atakayebaki nyumbani, kwa kushindwa kwenda shule.

“Agizo hili sisi tulilifanyia kazi hatukulala siku hiyo Dar es Salaam, tulikuja moja kwa moja hadi Karatu na kuanza kulifanyia kazi.

“Ile ndoto yako ya kielimu sisi Karatu tuliifanyia kazi na ndio maana leo unaona tunaiendeleza kwa kujenga Chuo hiki cha afya ili wale watoto wanaomaliza kidato cha nne waweze kuendelea na masomo,” alisema Maasai.

Alisema wakati wa maandalizi ya kuendesha harambee hiyo, wakiwa katika juhudi za kutafuta mgeni rasmi ndipo jina la Lowassa lilipopendekezwa.

Naye, Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini, Dk. Martine Shao, akizungumza katika Ibada hiyo alimshukuru Mungu kwa kujibu maombi yao.

Alisema siku zote Kanisa huwa halibahatishi na yeye anaamini kwamba, Mungu amempa Lowassa vipaji mbalimbali.

“Mungu amekubariki na ndio maana ukitoa kauli nchi nzima inafuata na kila unapofanya kazi yako, Watanzania wanamshukuru Mungu.

“Siku zote mtu mwenye vipaji ana ndoto nyingi na umesimamia ndoto zako vizuri, hatujui huko mbele tuendako tunamuomba Mungu akulinde na kukubariki katika wajibu wako,” alisema Askofu Shao.

Kwa upande wake, Lowassa akizungumza kabla ya kuanza kuchangisha harambee hiyo aliwaeleza waumini hao kwamba zipo sababu kadhaa ambazo zimekuwa zikimsukuma kutumika katika harambee.

Alisema sababu ya kwanza ni mapenzi yake kwa kazi ya Mungu, huku sababu ya pili ikiwa ni kumbukumbu zake mbele za Mungu.

“Sasa anayebisha namuomba akamuulize Mungu kuhusu hizo sababu zangu za kushiriki katika harambee,” alisema Lowassa.

Akizungumzia kuhusu harambee hiyo, alilipongeza Kanisa na Halmashauri ya Karatu kwa kazi nzuri ya ujenzi wa Chuo hicho.

Alisema juhudi hizo za kujenga Chuo cha Afya ni harakati za kuendeleza kupambana na bomu la ajira kwa vijana linalotarajia kulipuka.

“Niwapongeze kwa uamuzi wa ujenzi wa Chuo hiki, narudia kusema tena juhudi hizi ni mbinu sahihi za kutegua bomu la ajira kwa vijana nchini,” alisema Lowassa na kuongeza:

“Niwashukuru pia Mbunge wa Karatu Mchungaji, Israel Natse na mwenyekiti kwa kuwa walikuja nyumbani kuomba nishiriki harambee hii,” alisema Lowassa.

 

So, CHADEMA What R U trying to tell US???? Yeye sio FISADI ila anathubutu kuwa FISADI????
 
Ndo uone walivyo wanafiki? Ukweli wanaujua ila hawataki kuukiri.
 
Sitta aliwaambia mzikatae lakini Mbunge Natse ndiye aliyekwenda kumfuata nyumbani kwake.

Chezea pesa wewe!
 
Hii ni kauli ya mtu binafsi sio ya chama .............acheni wivu wa kike hii ni kauli ya ccm
 
Huyu Askofu anaongea mpaka anasahahu kama yeye ni mchunga kondoo wa bwana. Pesa kweli ni ufunguo.

Yaani hata Maaskofu Tanzania wamejaa ubinafsi na njaa tupu. Kauli kama hii huwezi kuamini kama imetolewa na Kiongozi wa kanisa achilia mbali Askofu. Akija mwingine na dau zaidi ya hili, utamsikia tena akisema kauli kama hizi.
Kauli ya Askofu anayepiga chapuo kupata pesa. Ama kweli ni rahisi ngamia kupita kwenye tundu la sindano.
Naye, Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini, Dk. Martine Shao, akizungumza katika Ibada hiyo alimshukuru Mungu kwa kujibu maombi yao.
Alisema siku zote Kanisa huwa halibahatishi na yeye anaamini kwamba, Mungu amempa Lowassa vipaji mbalimbali.
"Mungu amekubariki na ndio maana ukitoa kauli nchi nzima inafuata na kila unapofanya kazi yako, Watanzania wanamshukuru Mungu.
"Siku zote mtu mwenye vipaji ana ndoto nyingi na umesimamia ndoto zako vizuri, hatujui huko mbele tuendako tunamuomba Mungu akulinde na kukubariki katika wajibu wako," alisema Askofu Shao.
 
hujui kitu inaitwa sifa za kijinga? hapo wataalamu walikuwa wanashawishi kupata salio la kutosha tu, hakuna zaidi ya hilo
 
Daym Money
Nani aligundua pesa? Inafanya watu wale ma-puke yao wenyewe?
I hate the power of money aisee
 
kwangu sishangai kwani wote hao wa kaskazini na zimwi likujualo........
 
Sitta aliwaambia mzikatae lakini Mbunge Natse ndiye aliyekwenda kumfuata nyumbani kwake.

Chezea pesa wewe!
Sasa Sitta anaweza akatoa maagizo kwa CHADEMA wakayatekeleza? Au umesahau kuwa Sitta yupo CCM?
 
CHADEMA wajanja sana, sasa hivi wanamzuga tuu huyo jamaa. Akija kuwa mgombea watamgeuka kwa kashfa ya ufisadi.
 
Lowassa jembe ! wanaoona mbali watasema ;anao uwezo wa kuamua na kusimamia jambo.Anafaa kuwa rais ajaye aendeleze elimu yetu,afya nk.aliuzulu kuiokoa serikali na chama chake;ALIFICHA AIBU LKN WENZAKE WAMESHINDWA KUTAMBUA HILO.
 
Back
Top Bottom