CHADEMA: Lowassa mshindi kwa asilimia 61

CHADEMA: Lowassa mshindi kwa asilimia 61

Lekakui

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
1,451
Reaction score
589
Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimedai mgombea wake wa urais, Edward Lowassa anayeungwa mkono na Ukawa ataibuka na ushindi wa asilimia 61 katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Jumapili ijayo.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Kampeni za chama hicho, Reginald Munisi alidai katika tathmini iliyofanyika wiki iliyopita kimebaini kuwa mgombea wake ataibuka na ushindi huo.

"Wiki iliyopita tulifanya tathimini yetu. Kama chama cha siasa ni lazima ufanye jambo hili ili kuona utashinda kwa asilimia ngapi na unakubalika kiasi gani. Tumebaini kuwa tutashinda kwa asilimia 61 na hata ikipungua haitazidi asilimia 58," alidai Munisi.

Alisema matokeo hayo yalitokana na wananchi 30,000 waliohojiwa katika mikoa yote nchini lakini alikataa kufafanua kwa kina methodolojia wanayotumia kufanya tathimini hiyo kwa sababu ya "kimkakati".

Alisema Lowassa ambaye atahitimisha kampeni za Chadema na Ukawa kesho kutwa katika viwanja wa Jangwani, Dar es Salaam, anakubalika kwa kiasi kikubwa na wananchi.

Hii ni mara ya pili kwa Ukawa inayoundwa na vyama vya Chadema, NCCR-Mageuzi, NLD na CUF kutoa matokeo ya utafiti wao. Mara ya kwanza ilikuwa Septemba 24 baada ya mwenyekiti mwenza wa umoja huo, James Mbatia kusema utafiti uliofanywa sehemu tatu tofauti ulimpa Lowassa ushindi wa asilimia 71

Vilevile, Chadema kimetaja kasoro zilizopo katika Daftari la Kudumu la Wapigakura na mfumo wa kujumlisha matokeo na kutoa saa 24 kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutoa ufafanuzi, ikishindiwa, kitatangaza msimamo wake leo.

Alisema kuna watu wanaofahamu Chadema na Ukawa unaoundwa na NCCR-Mageuzi, NDL na CUF wataibuka na ushindi na kuanza kufanya hila kuhakikisha haupatikani.

"Kuna mambo mengi yanafanyika ikiwamokuwakatisha tamaa wananchi. Tunaitaka NEC na Serikali kuwaacha wananchi wapige kura ili wapate viongozi wanaowataka, kinyume na hapo watazua tafrani kubwa," alisema.

Alipoulizwa iwapo watayakubali matokeo, alisema: "Tukishindwa kwa haki tutayakubali, lakini kinyume na hapo ni ngumu. Ila hata wao pia wajiandae kisaikolojia iwapo tutashinda na hatutakuwa na kisasi na mtu."

Munisi alidai taarifa walizonazo zinalenga kufanikisha ‘bao la mkono' kuwa ni kuvuruga kwa muda mawasiliano ya simu na mitandao siku ya uchaguzi na kuzimwa kwa umeme katika maeneo ambayo Ukawa wana nguvu.

Chanzo: Mwananchi

Na ukawa tunategemea kupata kura 17,000,000 na zaidi

Tukienda kwa haki hizo 61% ndogo mno kwa LOWASSA anastahili zaidi ya 80%
VIVA UKAWA!!!

Nadhani wamekosea ...lowassa anashinda zaidi ya 80%

Waliwahi Kusema 71, Juzijuzi Wakasema 82 Leo 61! Hii Graph Inatia Shaka

Chama cha majambazi, kwanza jifunzeni jinsi ya kufanya sample ya kutathmini matokeo ya uchaguzi. Huwezi kufanya sample ya watu 30,000. Waulizeni mabingwa wa kufanya sample za uchaguzi. Sample haizidi watu 1000, mna wakati mgumu sana na hilo Jambazi Sugu maana mwisho wa kulamba peremende ni jumapili chijui chacha mtalamba wapi wakati Jamabazi Sugu litatokomezwa kwenda kuchunga ng'ombe kule Monduli.

Ni Lowassa tu Maana hakuna Namna!!!!
I confidently and proudly insisted that KANU would win and I forgot that the willing of the decision makers can surpass my Political Professorial Position.
I am hereby therefore, calling upon my friends those who are in power as well as those with utopian point of view; They should crystal clear understand that, to every thing there is a season and a time to every purpose.

WELL SAID DANIEL ARAP MOI

715 mbatia after 1 month 81% Mrema, then siku 2 tu 61% Munishi nadhani twaweza walikuwa sahihi kupa 22%!Viva Magufuli, jembe la uhakika, hapa kazi tu

Huo sio ushindi. Ni kwamba maeneo waliyoyafikia kwenye kampeni, ni 61% ya maeneo waliyotakiwa kuyafikia, sasa linganisha na maeneo waliyoyafikia CCM kwenye kampeni, hizo ndio hesabu za kweli, haya mengine matakataka tu

Kama kura zitapigwa kwenye mitandao ya kijamii Lowassa atashinda lakini kwenye masanduku ya kupigia kura yanayosambazwa kwa sasa, Lowassa hawezi kushinda kamwe, YATUNZENI MANENO HAYA TAREHE 27/10/2015 MNISUTE HAPA.

Tufanye weighted winning % kama ifuatavyo (71+61)/2 = 66%
UKAWA WATASHINDA KWA ZAIDI YA ASILIMIA 66.

CHAGUA LOWASSA CHAGUA UKAWA.

Ni Lowassa tu Maana hakuna Namna!!!!

I confidently and proudly insisted that KANU would win and I forgot that the willing of the decision makers can surpass my Political Professorial Position.

I am hereby therefore, calling upon my friends those who are in power as well as those with utopian point of view; They should crystal clear understand that, to every thing there is a season and a time to every purpose.

WELL SAID DANIEL ARAP MOI

Back
Top Bottom