CHADEMA NI 'CHANDA CHEMA' HIVYO WANAFUNZI WA VYUO VIKUU
WAMEHIARI KUKIVISHA TU PETE WENYEWE
Katika swali lako hilo hapo juu wala usifikiri kwamba uko peke yako tu. Hata CCM, CUF na vikundi vingine wamepigwa butwaa hivo hivo usipime!!! Kwa bahati nzuri sana taarifa zinasema kwamba CHADEMA hualikwa na wanafunzi wenyewe na wala hawajipereki kwao.
Kwa mfano jana wapambanaji walivyokua Makumira Arusha, tayari humu ndani tuliona wachangiaji kibao kwenye THREAD fulani hivi wakiwaomba viongozi wa CHADEMA wawatembelee na wao kule Mkoa wa Iringa wakisema kwamba vyuo vyote mkoani humo vikiwemo Tumaini, Ruaha, Mkwawa, Klerruu, VETA na nyinginezo tayari wanafanya matayarisho ya kufanikisha jambo hilo.
Pamoja na yote mzee siku zote mtu yeyote anayependa kutambua, kuheshimu na kutetea maslahi ya taifa badala ya kutetea maslahi binafsi ya vijikundu vijikundi vidogo vidogo vya kifisadi, siku zote mtu huyo au chama hicho hupendwa sana na wananchi na mambo yake kwenda kiulaiiini kama hivyo unavyoionea gere sasa hivi CDM. Karibu kundini kabla hatujafunga milango ya mabadiliko ya kweli Tanzania!!
Wanafunzi wa vyuo vyote nchini vikiwemo UDSM, UDOM, MAKUMIRA na sasa Tumaini Iringa, Ruaha na Mkwawa, hongereni sana kwa kujitambulisha na upande wa siasa za 'Nguvu ya Umma' nchini ambayo falsafa yake ni UTAIFA MBELE KAMA TAI na kusema watetezi wa maslahi binasi ya vikundi kama CCM siku zao kupigwa chini ndio umewadia.