Boss
Barbarosa Ukiona hivyo ujue, Mh. Mbowe kawashika pabaya. Kila mnalopanga kuiua Chadema mnashindwa. Kuna mmoja alisema kabla ya Uchaguzi Chadema itakuwa ishakufa kabisa. Mkashindwa na Akashindwa. Sasa hivi mnanunua Wapinzani, Chadema bado ipo.
Ukishaona mpinzani wako anakushauri, tafakari mara mbili mbili.
Ila la kubadilisha Uongozi kwa awamu, nakuunga mkono hoja.
Ila ushauri wangu kwako na kwenu, msiue Upinzani. Upinzani ni mzuri kwa Afya na Ustawi wa Taifa, Taasisi, Kundi, Ndoa, Familia. Bila Upinzani Imara hakuna maendeleo. Na zama za Ndio Mzee zimepitwa na wakati.
Hamasisheni wananchi kufuata Katiba na Sheria za Nchi.