CHADEMA, Kwa hili suala la Zitto mbona hamueleweki?

CHADEMA, Kwa hili suala la Zitto mbona hamueleweki?

Status
Not open for further replies.

Ethical Ninja CEH

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2011
Posts
3,695
Reaction score
5,053
CDM kama chama cha upinzani chenye nguvu Tanzania, juu ya hili swala la Zitto mmeshindwa kuonesha msimamo wenu kama chama isipo kua mmebaki kulalamika kwenye vyombo vya habari, kuchafuana kwenye mitandao, pasipo nyie kama chama kuchukua hatua dhidi yake kutokana na tuhumu zinazo elekezwa dhidi yake.

Zitto mnamtuhumu ni msariti ndani ya chama, mnafiki kuhusu swala la posho, anapokea pesa kinyume na utatatibu yani rushwa. Na tuhuma hizi wanao zisambaza si kwamba ni watu wa nje ya CDM, bali ni viongozi ndani ya CDM wenyewe.

Kwa hizo tuhuma dhidi yake moja kwa moja zinamnyima sifa za kua kiongozi ndani ya chama, na kama anaendelea kua nae ndani ya chama, hiyo ni sawa na kukumbatia bomu linalotaka kulipuka au nyoka.

Na kwa tuhumu hizo kama mnashindwa kuchukua hatua dhidi yake basi itatufanya tuamini mna mtengenezea mizengwe ya kisiasa kwa manufaa yenu binafsi, na kumdhoofisha kisiasa.

Chukueni uamuzi sahihi katika wakati sahihi. Kama kumfukuza au nyie mjitoe kwasababu mnashindwa kumchukulia hatua ilihali mnaona ni adui ndani ya chama.

===========
Mawio: Zitto usaliti hakuanza leo

Mwaka 2010, Sebastian Kasinge aliyeteuliwa kugombea ubunge jimbo la Mpanda Mashariki, alikwama kuwania nafasi hiyo. Kisa?! Zitto.

Ilikuwa hivi, Kasinge alikwama kupata barua ya utambulisho kutoka kwa viongozi wake wa wilaya ya Mpanda kuwa ni mgombea. Akaenda makao makuu ya Chadema jijini Dar es salaam. Akakutana na Dk. Slaa, katibu mkuu wa Chama chao, Akampa barua ya uteuzi.

Lakini Zitto kwa kutumia kofia yake ya unaibu katibu mkuu tena akiwa nje ya ofisi na bila kushirikiana na wenzake wa makao makuu, alimwandikia msimamizi wa uchaguzi wilaya ya Mpanda kumjulisha Chadema kutoweka mgombea jimbo la Mpanda Mashariki. Msimamizi wa Uchaguzi mara baada ya kupata barua ya Zitto alimwondoa Kasinge kwenye kinyang'anyiro cha ubunge na kumtangaza Mgombea wa CCM, Mizengo Kayanza Peter Pinda kuwa AMEPITA BILA KUPINGWA

Michael Makenji aliyekuwa mgombea wa ubunge wa Chadema jimbo la Musoma Vijijini, alijiondoa kwenye kinyang'anyiro hicho dakika za mwisho. Nimrod Mkono wa CCM ALIPITA BILA KUPINGWA. Hii ni baada ya Zitto kumshawishi mgombea wa chama chake kujitoa. Taarifa zinazomkhusu Makenji zinasema kabla ya mgombea huyo kujiondoa kwenye kinyang'anyiro, naibu katibu mkuu wake alifanya mazungumzo ya kina na Mkono.

Katika kuthibitisha hilo, Makenji alikabidhi kwa viongozi wake wa chama ujumbe mfupi wa sms ulioonekana umetoka kwa Zitto kwenda kwake ukilenga kumshawishi kujitoa.

Miongoni mwa yale yaliyotajwa na Zitto kwenye ujumbe huo ni pamoja na kwamba Mkono yupo tayari kuongeza fedha iwapo yeye Makenji atakubali kujiondoa kwenye mbio za kuwania ubunge.

Josephat Isango, aliyejitosa kwenye mbio za ubunge jimbioni Singida kupambana na Mohamed Dewji aliwekewa pingamizi na Wazael Nakamia, mwenyekiti wa Chama chake, CHADEMA wilaya ya singida Mjini. Katika pingamizi lake, Nakamia anasema Isango hakupitishwa na Chama chake kugombea nafasi hiyo. Alipoulizwa na mkurugenzi wa sheria wa chama hicho, Tundu Lissu kilichosababisha kuwekewa pingamizi kwa ndugu Isango, Nakamia alisema ..."ni maelekezo ya Naibu katibu Mkuu..."

Zilitokea vuta nikuvute kadhaa ambapo mwishowe Dk. Slaa ambaye alikuwa amelazwa hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa matibabu alimwandikia msimamizi wa uchaguzi barua nyingine ya kuthibitisha uteuzi wa Isango.

Rais Kikwete alipofika singida kumnadi mgombea wa CCM Singida alimtangaza Dewji kuwa amepita bila kupingwa, siku chache baadae NEC ikamtangaza Isango kama mgombea.

Tamthilia hii ya Isango, Zitto, Dewji, Nakamia na Lissu imeelezwa mara nyingi na na Lissu mwenyewe kwenye vikao vya CC mbele ya Zitto wenyewe. Zitto Hakuwahi kukana. Nakamia tayari amevulia uongozi.

Mgogoro wa Madiwani Arusha haukumalizika bila ya kumhusisha Zitto. Kamati iliyoundwa na chama chake kutfuta suluhu ya mgogoro huo iligundua mkono wa Zitto katika suala hilo. Mgogoro ule uliisha kwa kufukuzwa madiwani watano.

Naibu katibu mkuu alishiriki kwa kiasi kikubwa katika mgogoro huo kwa kushiriki kuwashawishi madiwani kukiasi chama, ni sehemu ya mkakati wake wa kupambana na Lema na wanasiasa wenzake ndani ya chama chake wanaoonekana kumpiku kwa umaarufu.

Uchaguzi mdogo ulipofanyika Zitto hakushiriki hata mkutano mmoja wa kampeni,Hkwenda Arusha siku ya Maombolezo baada ya vifo vya wafuasi wanne wa Chadema.

Mengi zaidi soma MAWIO, Toleo namba 0070 Alhamis November 21-27, 2013 Uk10-11
 
Kweli mleta mada anasema. Hatua stahiki zinabidi zichukuliwe dhidi ya ZITO hilo lipo wazi,
 
Who is zzk?mbona kila kukicha ni habari za zzk?alafu mnaosema cdm ni zzk na zzk ni cdm mnatumia k.a.m.a.c badala ya medulaoblangata.kazi kwenu
 
Cuf walimtimua hamad rashid alikuwa na mwendo km wa Zito kaka yangu mbowe we ndio m.kiti heli ya lawama kuliko fedheha timua dogo Huyu anatumika na ccm kwa nini hoja zake asilete ktk vikao anakimbilia Sudan
 
Huu ndo mwanzo wa mwisho wa CHADEMA. Kumchafua mtu sio njia sahihi ya kujisafisha. Wanaomchafua Zito wanatakiwa watafute njia sahihi ya kujisafisha na si kuchafua watu safi. kwa kufanya hivyo wanachama wote wenye akili wote watawadharau.
 
Subiri uje uyavae matusi hapa muda si mrefu,

Wengine tunaitwa waislam wenye siasa kali na tujikite kupigania gesi ya mtwara,hayatuhusu,sometimes tunaitwa MAGAMBA KABISA,YAHITAJI UJASIRI KUSIMAMIA MAONO YAKO NA KUACHA UCHUMIA TUMBO NA USUKULE....
 
ccm mnachotaka ni zitto afukuzwe,maneno yawe mengi kila kona na nyie mpande mbegu huko.zzt atajikaanga mwenyewe kama kiti moto.na ccm wakiona anachelewa watamkaanga maana wanataka vurugu zake zianze mapema ila imeshindikana,kwa jina la yesu roho ya mafarakano itawarudia ninyi na mungu atachafua ndimi zenu mtahuana wenyewe kwa wenyewe,sema amina
 
Matusi hayana nguvu katika ukweli..
Ukweli unauma kuliko matusi..

Subiri uje uyavae matusi hapa muda si mrefu,

Wengine tunaitwa waislam wenye siasa kali na tujikite kupigania gesi ya mtwara,hayatuhusu,sometimes tunaitwa MAGAMBA KABISA,YAHITAJI UJASIRI KUSIMAMIA MAONO YAKO NA KUACHA UCHUMIA TUMBO NA USUKULE....
 
Chadema wakimfukuza zitto chama kinakufa mchana kweupe.

Kama unalijua hilo kwanini sasa unaropoka? Na km CDM ni Zitto kuna ubaya gani si Mwanachama wa CDM kwani ni Mwanachama wa CCM?

Hata CDM wanajua kwamba Mapenzi yenu kwa Zitto sio ya dhati isipokuwa ni ya Kinafiki.
Mtasubiria sana tumfukuze lakini hatumfukuzu ila ataendelea tu kuwepo km ambavyo yupo sasa.
 
mkuu, pamoja na u-CDM wangu lakini siungi mkono tabia ya kuhukumu mtu bila ushahidi - hatutaki mambo ya kusikia, kuelezwa, kutaarifiwa...jenga tabia ya kujiridhisha pasipo shaka.

Kwa maneno yako tayari umeshamhukumu ZZK kwa kuyaamini maneno ya lema ambaye wanajamvi walimtaka alete ushahidi wa ZZK kupokea posho lakini alishindwa na kutokomea kusikojulikana hadi leo!

narudia kuiomba kamati kuu imtake kamanda lema alete ushahidi wa tuhuma zake nzito dhidi ya ZZK hapa jf na akishindwa imwadhibu kama ambavyo wengine walikwishaadhibiwa huko nyuma - ningefurahi ikiwa atatoswa kuwa mjumbe kamati kuu ili kuondoa UROPOKAJI kamati kuu, hii pia itakuwa fundisho kwa wajumbe wengine siku za usoni.

ni mategemeo ya baadhi yetu (wana CDM waliotayari kukosolewa) kwamba moja kati ya sifa za wajumbe wa kamati kuu CDM ni pamoja na kuwa na hekima na busara - lema alishindwa nn kusubiri kikao hiki cha kamati kuu alete hoja dhidi ya ZZK sambamba na ushahidi ili wajumbe wengine wakijiridhisha basi hatua stahiki zingefuata.

Taswira niliyoipata kutoka kwa lema ni kama mtu aliyekasirishwa na kitendo cha ZZK kuwaanika wenzie kwa wananchi kwamba wanachukua posho - hivyo akakurupuka kuja na jazba, wivu, chuki kwa tuhuma za kufikirika.

chondechonde kamati kuu - sheria ni msumeno, unakata sehemu 2 bila kujali jina, rangi, kabila wala jinsia.

tunataraji sheria itakayotumika kumwadhibu mwigamba kwa kulalamika mitandaoni bila kupitia vikao ambavyo ana fursa kama mshiriki, pia itumike kwa kamanda lema vilevile.

hatutegemei kufunika kombe kupitia maneno 'hakuna mtu aliyeleta malalamiko kuhusu kuchafuliwa mitandaoni' na kusahau hata kwa mwigamba hakuna mtu tulitaarifiwa kupeleka malalamiko kamati kuu, hoja ni kwamba ukikichafua chama iwe barabarani au popote pale ili hali wewe ni kiongozi unaadhibiwa tu kwa taratibu za chama.
 
Chama utafikiri genge la wahuni, kila mtu akijisikia kulopoka analopoka analolijua pasipo kuangalia athari zake, chama mambo ya ndani wao wanayafanya ya nje..

Huu ndo mwanzo wa mwisho wa CHADEMA. Kumchafua mtu sio njia sahihi ya kujisafisha. Wanaomchafua Zito wanatakiwa watafute njia sahihi ya kujisafisha na si kuchafua watu safi. kwa kufanya hivyo wanachama wote wenye akili wote watawadharau.
 
Mkuu, mie sijahukumu isipo kua nimeeleza kwa pande zote mbili.

Pili sija mtaja Lema kwasababu waharibifu ni zaidi ya huyo lema... Lema huenda amaetumika na hao wenzake, Lema hana hadhi wala ajafikia level ya zitto kisiasa..

Lema anatakiwa kumuheshimu kiongozi wake lakini haijawa hivyo, na hata walio mletea zengwe nyingi ni vifaranga ambavyo inaonesha kuna mama yao nyuma.

Back
Top Bottom