CHADEMA kuvamia majimbo ya Maghembe, Kilango na Mwanri

CHADEMA kuvamia majimbo ya Maghembe, Kilango na Mwanri

Dingswayo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
4,019
Reaction score
2,930
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoa wa Kilimanjaro, kitatumia helikopta na magari tisa kuanzia leo kushinikiza wananchi wa majimbo ya Same na Siha yanayoongozwa na Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Aggrey Mwanri kuwakataa wabunge hao katika uchaguzi mkuu ujao kwa madai wameshindwa kuwajibika.

Mwenyekiti wa Chadema mkoani hapa ambaye pia ni Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, aliyasema jana kuhusu operesheni hiyo itakayoongozwa na makada wa kitaifa wa chama hicho akiwamo Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni,Tundu Lissu.

"Tutaweka kambi ya siku sita katika jimbo la Siha, Same, Mwanga na Moshi Vijijini, lakini nguvu kubwa ni kwa mawaziri wawili ambao tumeweka mkakati wa kuwang'oa kwa kuhakikisha hawarejei tena madarakani na halmashauri hizo zitaongozwa na Chadema.

Ushindi tulioupata Kiborilonitutaupeleka kesho(leo) kwa helkopta na magari tisa ya Operesheni Pamoja
Daima ya M4C," alisema Ndesamburo.

Operesheni hiyo itayahusu majimbo ya Same Magharibi, Same Mashariki, Mwanga, Vunjo Moshi Vijijini na Siha. Alisema lengo la operesheni hiyo ni kukiimarisha chama kuanzia ngazi ya shina pamoja na kufanya chaguzi za viongozi katika maeneo hayo.

Ndesamburo alisema lengo jingine ni kuendelea kuwafumbua wananchi kuhusu mchakato wa katiba mpya ambao kwa sasa umefikia katika hatua yakuanza kwa mjadala wa rasimu ya pili ya katiba Bungeni pamoja na umuhimu wa kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapigakura.

Chadema kimefanikiwa kutetea Kata ya Kiboriloni katika uchaguzi mdogo uliofanyka juzi baada ya kupata kura 1,019 dhidi ya kura 255 alizopata mgombea wa CCM, Willy Tulli na Adon Mzava wa UDP aliyeambulia kura mbili.

CHANZO: NIPASHE

mzee wa tindikali henry kilewo analitamani sana jimbo la maghembe, anatamani sana aingie mjengoni na yeye akapige posho kama lema
 
Wazee Wa ukanda...hay a huko kwenu bans kauwaneni wenyewe il a kigoma hatuwataki
 
Wazee Wa ukanda...hay a huko kwenu bans kauwaneni wenyewe il a kigoma hatuwataki

Unaongea kwa fact au unaongea kujionesha ni aina (type) ya m2 na akil ulivyo.nyie ndo mnaeneza mizz ya chuk,fitina,ukanda na ukabila....achen bhana Mungu hapend.
 
Chadema kwa Mwanri mtajisumbua bure hata muende na helikopta 100,Mwanri kaibadilisha Siha sana na Wananchi wanamkubali kwa kiwango cha juu sana! Ameweka maji kila kijiji na sasa anaweka umeme wa REA kila kijiji,Siha yote ina pitika sasa barabara zimejengwa,shule za kata zina vyoo vya ku-flash! Nendeni chadema siha mtajionea maendeleo makubwa sana ambapo mimi namchukulia Mwanri kama Mbunge bora kwa kuleta maendeleo Siha,BBC wamechukua documentary kuonesha namna rural areas in Africa wanaweza kuendelea! Miundo mbinu ya umwagiliaji ni mingi sana na imekamilika kwa wakati! JICA wameipongeza siha kwa kupiga hatua!
Ukiacha Hospital ya Kibong'oto wilaya ya Siha sasa wana hospital ya Wilaya ambayo ina maabara bora ambapo east africa hakuna yeye vifaa bora zaidi ya siha! Siha sasa wanauza nyanya Nairobi kwa wingi,kipato cha wananchi kipo juu. Chadema wakienda waongee sera ya jumla tu ya UFISADI kitaifa lakini kwa maendeleo Siha Chadema hawana kitu cha kusema
 
Karibu sana Mwanga na same tunahitaji sana chadema huku.
 
Waelekeze tu nguvu huko kwao. Hata wakichukua majimbo yote si mbaya. Ila huku kwetu Songea hawatathubutu kutwaa hata mwenyekiti wa serikali za mitaa
 
Karibu sana Mwanga na same tunahitaji sana chadema huku.
Huko ni nyumbani kwa CHADEMA. Nendeni Mtwara mkakione cha mtema kuni. Operesheni okoa kusini iliwatoa kamasi na mlirudi kwa aibu
 
Kata ya lizaboni diwani ametoka chama gani?
 
Huko ni nyumbani kwa CHADEMA. Nendeni Mtwara mkakione cha mtema kuni. Operesheni okoa kusini iliwatoa kamasi na mlirudi kwa aibu

Huku same na mwanga tuna wabunge wa kula posho tu ! tunataka wabunge wawajibikaji ,hapa kuna ukoo wa panya ,na moja ni wazir mzigo .
 
chadema njooni tunawaitaji snaaa na tupo tiyar kuwachagua
 
Huko ni nyumbani kwa CHADEMA. Nendeni Mtwara mkakione cha mtema kuni. Operesheni okoa kusini iliwatoa kamasi na mlirudi kwa aibu
Badala ya kujipanga jimbo la Kalenga wanaleta mbwebwe
 
Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    28 KB · Views: 167
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI Tume ya Tifa ya Uchaguzi
imepokea barua kutoka kwa
Mhe. Spika wa BUNGE la
Jamhuri ya Muungano Tanzania
ya kuiarifu uwepo wa nafasi wazi
ya Ubunge katika Jimbo la Kalenga lililopo katika
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa
Vijijini, kufuatia kifo cha Mbunge
wa Jimbo hilo Mhe. William
Mgimwa aliyefariki dunia tarehe
1/1/2014. Baada ya taarifa hiyo Tume imepanga ratiba ya
Uchaguzi mdogo katika Jimbo la
Kalenga kama ifuatafyo:- 1. Uteuzi wa Wagombea
Ubugne utafanyika tarehe 18-
Februari-2014 2. Kampeni za Uchaguzi
zitaanza tarehe 19-
Februari-2014 hadi 15-
Machi-2014 3. Siku ya kupiga kura ni
Jumapili terehe 15-
Machi-2014 Wagombea wanatakiwa
kuwasilisha Fomu za Uteuzi kwa
Msimamizi wa Uchaguzi wa
JImbo la Kalenga siku ya Uteuzi
si zaidi ya Saa 10:00 Alasiri.
Tume inawataarifu Wananchi wote pamoja na Vyama vya
Siasa kufuata ratiba iliyotolewa
pamoja na kushiriki katika
mchakato mzima wa Uchaguzi
kuanzia siku ya Uteuzi hadi siku
ya Kupiga Kura ili watimize haki yao ya Kikatiba ya Kuchagua
viongozi wanaowataka. Tume inawasisitiza wananchi
wote katika maeneo husika
kujitokeza kukagua tarifa zao
wakati wa kuweka wazi Daftari la
Kudumu la Wapiga Kura ili kuona
kama kuna marekebisho madogo yanahitajika kufanyika
kuwawezesha kupiga Kura bila
malalamiko yoyote. Ikumbukwe
kwamba hakutakuwa na
uandikishaji mpya wa Wapiga
Kura. J. Mallaba
MKURUGENZI WA UCHAGUZI UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE JIMBO LA KALENGA
 
Mm namsubir mwenyekit wangu hapa usangi aje ! nitampa ushirikiano wa asilimia miamoja .Nakumbuka mbal sana ,wazee wetu wanavyo danganywa na huyu mbunge mshirkina anaye toa kafara kule msitu wa kindoroko.Wazee wangu wamekuwa wana ambulia nyama tu.
 
Chadema kwa Mwanri mtajisumbua bure hata muende na helikopta 100,Mwanri kaibadilisha Siha sana na Wananchi wanamkubali kwa kiwango cha juu sana! Ameweka maji kila kijiji na sasa anaweka umeme wa REA kila kijiji,Siha yote ina pitika sasa barabara zimejengwa,shule za kata zina vyoo vya ku-flash! Nendeni chadema siha mtajionea maendeleo makubwa sana ambapo mimi namchukulia Mwanri kama Mbunge bora kwa kuleta maendeleo Siha,BBC wamechukua documentary kuonesha namna rural areas in Africa wanaweza kuendelea! Miundo mbinu ya umwagiliaji ni mingi sana na imekamilika kwa wakati! JICA wameipongeza siha kwa kupiga hatua!
Ukiacha Hospital ya Kibong'oto wilaya ya Siha sasa wana hospital ya Wilaya ambayo ina maabara bora ambapo east africa hakuna yeye vifaa bora zaidi ya siha! Siha sasa wanauza nyanya Nairobi kwa wingi,kipato cha wananchi kipo juu. Chadema wakienda waongee sera ya jumla tu ya UFISADI kitaifa lakini kwa maendeleo Siha Chadema hawana kitu cha kusema
Kani huyu sio CDM, anafiti kabisa kuwa CDM, ajifikirie.
 
Sisi same mashariki tuli mchagua mropokaji ana malechela sas hiv hata uropokati kaacha tangu arudi bungeni ametoa cd ya kiwanda cha tangawizi feki kwenye deki iliyodumu 1995-2000 sasa ameingiza cd ya msitu wa shengena kila akipata chans lazima ataongelea hilo huku msitu bado unavamiwa.barabara ya mkomazi same ndo barabara mbovu kupta zote mkoa wetu chadema njoni hili limama tumelichoka.
 
Back
Top Bottom