Umaarufu wa chama utaendelea kwa sababu M4C imezinduliwa Arumeru ili itekelezwe. Wakati rufaa inaendelea wananchi watamchangia Lema kupitia M4C ili aendelee kuwatumikia wananchi na wakati huo huo kukiongezea chama umaarufu zaidi na kukiimarisha. Hukumu hiyo ya kosa la kutunga na lisilokuwepo itatengeliwa na mahakama ya rufaa kama wakiona umuhimu wa kulinda hadhi ya mahakama kuu na ya rufaa na muhilimili wa mahakama kwa ujumla....mahakama ya wananchi inafaa zaidi. Umaarufu wa chama unazidi kupaa. Kwenda tena mahakamani ni kupoteza muda na nafasi ambayo imetolewa kuwapiga msasa wananchi kwa vitendo. Kama ingekuwa shule, basi hoi ni "remidial class.
Ikumbukwe kuwa msingi mzima wa kesi ni kuwa Lema alimdhalilisha Batilda Burian katika mojawapo ya mikutano ya kampeni. Kwamba, kuna maneno aliyasema ambayo yalikuwa ni ya udhalilishaji. Sasa hilo ni jambo linalowezakujadiliwa. Wale ambao mmesikiliza hukumu maswali yafuatayo yamejibiwa vipi. Binafsi sijaweza kuchukua msimamo wa hukumu yenyewe bila kuisoma vizuri na kuelewa reasoning ya jaji:
a. Mahakama imejuaje kuwa Batilda alidhalilishwa? - Bila kumuuliza yeye wanajuaej kuwa alijisikia kudhalilika. Vipi kama aliona ni ujinga tu wala haikumdhalilisha? Hivi mtu mwingine anaweza kwenda kusema "x ameibiwa" wakati yule ambaye anadaiwa kuibiwa anaona kila kitu chake kipo salama?
b. Imethibitishwa nini kuhusu alichosema Lema ambacho ni cha udhalilishaji? Alisema maneno gani, lini na wapi na ni ushahidi gani kuwa aliyasema hayo? Kwa mfano watu watatu wakija na walikuwepo kwenye mkutano wakasema hawakusikia maneno hayo na watu wengine watatu ambao walikuwepo kwenye mkutano huo wakasema walimsikia mahakama inaamua vipi kuwa hao watu watatu wanaosema walisikia wanasema kweli?
c. Binafsi kwa kweli sijashtushwa sana na Lema kuvuliwa ubunge - kama kuna ushahidi wa kutosha sidhani kama mahakam ailikuwa na uchaguzi mwingine- kilichonishtua zaidi na kinachonisumbua ni kuwa inaonekana hukumu ilishajulikana mapema zaidi almost a week kabla. Hili ni geni sana kwenye mahakama zetu. What happened?
Nimekuelewa, katika suala la demokrasia, ambalo wananchi wanachagua halafu jaji anabadilisha maamuzi ya wengi, hili ni suala la kujiridhisha mahakama ya rufaa. Nakwambia kama mahakama ya rufaa haitatengua maamuzi ya huyo jaji, M4C itaishukia mahakama. Nguvu ya wananchi itaishikisha adabu mahakama. Chadema na Lema wakate rufaa ili tuimukike mahakamu ya rufaa pia na muhimili mzima wa mahakamaHadhi ya mahakama miongoni mwa watu makini Tanzania iliisha pale ilipokubali kutumiwa katika suala la kuruhusu mgombea binafsi. Tanzania hakuna mahakama huru tena (hata Jaji Mkuu kasema hilo) na heshima yake imekwenda na maji. Kila mtu anajua rushwa ilivyoota mizizi na kushamiri mahakamani na uhuru wake unavyoingiliwa na serikali. Hivyo pamoja na faida zote za kukata rufaa, kwa hili, hapana. Rufaa bora ni kwa wananchi.
Mwanakijiji umenielewa vema sana. Hukumu hii haikubaliki na kuweza kuingizwa katika vitabu vya sheria. Njia ya kuifuta ni kukata rufaa. Sidhani kama mahakama ya rufaa itakubali kutumika namna hii kwa kosa la kutunga na lisiloweza kumvua ubunge, kama huyo jaji alivyotumika.
Naheshim anayejiheshim na kuheshimu wengine. Heshima ya upande 1 ni unafiki au uwoga au vyote viwili kwa pamoja.Kukata rufaa ni kuuheshimu
Pasco nawe unaionea huruma Chadema? Mimi sioni kama kuna kupoteza muda. Nimeeleza vema namna Chadema na Lema watakavyoendelea na kazi za M4C wakati rufaa inaendelea. Kushinda rufaa kwa Lema ni ushindi wa wananchi wote maana hatuwezi kama nchi kuruhusi sheria za ovyoovyo kuingia kwenye vitabu vya sheria. Ikumbukwe kuwa hukumu za ovyo kama hizi zikiachwa bila kukatiwa rufaa zinaingizwa kwenye vitabu vya sheria.Hakuna ubishi kuwa hukumu ile ina madhaifu kisheria na Lema akikata rufaa atashinda ila hukumu hiyo itabatilishwa 2014!. Time consuming for nothing!.
Baadhi ya lugha zinazodaiwa ni za udhalilishaji are facts na zina fall kwenye sheria za madai na sio jinai!.
Mfano mtu akiwa tipwa tipwa ukamuita 'wee tipwa tipwa' ana haki ya kulalamika kuwa amedhalilishwa but its a fact!.
Its a fact kuwa Batilda ni mwanamke na hakuna Lwaigwanan wa kike!.
Its fact Batilda kama mwanamke aliyeolewa kwa ndoa na ana mahusiano yasiyo ya kawaida nje ya ndoa huitwa ma..ya!.
Labda pia its a fact ile mimba ilikuwa sio ya mumewe bali ya yule Mzee wangu!.
Tuisubirie nakala ya hukumu ili tuichambue logic ya jaji katika kufikia maamuzi ila vyovyote iwavyo rufaa wasikate unless kwa kutoka rufaa kutamfanya Lema ame kubali kosa ambalo litatumiwa kama msingi wa kumwekea pingamizi!.
Wito wangu kwa Chadema, chonde chonde msije kunfanyia Lema kile mlicho mfanyia Mwera kule Tarime mkaishia kuitoa Tarime kama sadaka kwa sadakalawe!.
Kukata rufaa kuna sababu nyingi na za msingi. Na kama mahakama itaona aibu na kurudisha hadhi yake Lema atarudishiwa ubunge wake. Soma kwa makini sababu nilizoandika za kukata rufaaMkuu Atigi. Mimi ndiyo sijakuelewa. Kwa sasa hivi wengi wetu tunafikiria namna na njia ya kulirudisha
mikononi mwa Chadema jimbo la Arusha mjini. Wewe umejikita zaidi kwenye maswala ya mahakama na integrity yake. Au una ajenda ingine isiyoonekana waziwazi?
Dogo, soma sababu nilizoeleza utaelewa vema. Hukumu hii haikubaliki bika kukatiwa rufaa.kuna watu wametumwa kupima upepo hapa.gambaz hao.uchaguzi urudiwe na hakuna kukata rufaa ili aibu yao iwe juu yao na watoto wao.