Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA leo kimeitisha mkutano na waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho jijini DSM.
Mkutano huu ni baada ya Mahakama Kuu jana kutoa hukumu kwenye kesi Na. 28 ya mwaka 2014 iliyotaka kupata tafsiri ya vifungu vya 25(1) na 25(2) vya Sheria ya Marekebisho ya Katiba Namba 83 ya mwaka 2011;
Hukumu ambayo imeweka precedence ya kisheria na kisiasa katika kile kinachoendelea kwenye Bunge Maalum la Katiba;
Akithibitisha habari hizi msemaji mkuu wa Chadema Tumaini Makene amesema chama kitakutana na waandishi wa habari leo Ijumaa, saa 6 mchana.
Ikumbukwe juzi Jumatano mbunge wa Bariadi Andrew Chenge aliwasilisha katika Bunge la Katiba kile kinachodhaniwa na wengi ni Rasimu ya Katiba ya CCM huku wakitupilia mbali maoni yote ya wananchi yaliyokusanywa na tume ya Jaji Joseph Warioba.

Last edited by a moderator: