Abby Senior
Senior Member
- Feb 14, 2015
- 154
- 60
Mleta mada, ninasubiri ushihidi wako kwa sababu umesema umeshuhudia vikao kwa macho na masikio. Saidia waTanzania waleo kujua ukweli!!
Lakini nimeona pia kuwa hujui majukumu ya serikali. Kama hujui kuwa ajira ziko "regulatated" kisheria basi una walakini mkubwa. Idadi ya masaa ya kazi, mikataba na haki za mfanyakazi, viwango vya mishahara (kuweka kima cha chini) ni MAJUKUMU ya serikali. Kusema kwa sababu vyombo ya usafiri si vya serikali, hakuondoi wajibu wa serikali kuhakikisha wasafirishaji ambao wamekata leseni za serikali, wanalipa kodi kwa serikali - wanafuata "rules and regulations" zilizoanzishwa na serikali.
Kama hujui EWURA, na wizara ya Uchukuzi, wizara ya kazi (udereva ni ajira) ni vyombo vya serikali - huna uhalali wa kuiondoa serikali katika kadhia hii. Kushindwa kwa serikali kuweka taratibu stahiki za kushughulika na jambo hili au mazoea ya kutolishughulikia - havifanya jambo hili kuwa nje ya majukumu ya serikali.
You are very right, hakuna ubishi kwa ulivyoeleza!!