Tunataka kubadili Sheria ya Tozo ya Warfage kwa manufaa ya nani?

Imalamawazo

JF-Expert Member
Jul 27, 2021
1,343
3,256
Katika mjadala wa bajeti ya wizara ya uchukuzi 2024/25 baadhi ya wabunge wanalalamika tozo ya warfage kukusanywa na TRA. Wanataka sheria ibadilike ili tozo hiyo ikusanywe na TPA.

Ikumbukwe kuwa hiyo tozo ya warfage ilikuwa inakusanywa na TPA lakini kutokana na malalamiko ya wadau juu ya bandari kuigeuza kichaka cha upigaji hasa kuchelewesha utoaji wa mizigo ili wavune storage fee, serikali ilibadilisha sheria, tozo hiyo ikaanza kukusanywa na TRA. Baadhi ya wabunge wa sasa wameigeuka serikali, wanataka warfage fee ikusanywe na TPA.

Wote tunajua TPA imeshakabidhi kila kitu hadi wafanyakazi wake wa bandari ya Dar kwa DP World, je hiyo tozo ya Warfage ikirejeshwa TPA haitaleta mgongano na mwekezaji DP World? Na iwapo ikierejeshwa TPA je, DP world hawezi kumnyang’anya TPA kupitia vifungu vya mkataba?

Niombe mwenye uelewa zaidi na hii warfage fee atueleweshe.

Hadi nitakapo pata elimu kuhusu zaidi kwa uelewa wangu mdogo nakataa pendekezo la wabunge, tozo iendelee kukusanywa TRA.

Ni nini maoni yako kuhusu ukusanywaji wa warfage fee?
 
Mbombo ngafu !!! Sheria za nchi yetu zinagezwa kulingana na matakwa ya mtu au watu na si taifa. Sabubu walizotoa ni zipi na TRA imeulizwa kushindwa kwao au ni nini jamani. Kwa nini haikuwa hivyo kabla na sasa kuna umuhimu gani .
 
Ukiona hao wabunge wanaongea basi ujue kuna mawili,
1. Serikali imekusudia kufanya hivyo kwahiyo inawatumia kuchombeza mada ionekane ni matakwa ya wawakilishi.
2. Kuna beberu (mf. DPW) amewapa mlungula na anaitolea mate hiyo tozo.
 
Back
Top Bottom