Katika mahakama kumbukumbu za kesi hwekwa na huwa zinatumika kaika kutoa uamuzi kwa kesi zitakazotokea hata baada ya miaka mingi.Tumeshuhudia reference zikifanyika kwa kesi za miaka hata 50 iliyopita.Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema leo kitatoa kauli ya awali kwa umma kupitia vyombo vya habari juu ya uchaguzi mdogo wa Chalinze ambapo kimebaini njama very serious ambazo zimetumika kupika na kutengeneza ushindi wa CCM.
Akizungumza kwa ufupi Msemaji wa chama hicho Tumaini Makene amesema Kama mgombea wa chama hicho na chama chenyewe walikuwa wanakubalika kama wanavyosema, kwa nini zimetumika njama hizo?
Makene amesema taarifa watakayoitoa itaanika ukweli wote wa yaliyotokea Chalinze
Ni vyema kuna kuna ushahidi wa kutosha tamko na mbinu zilizotumika kuwekwa hadharani ili angalau chaguzi zinazokuja tuwe na reference.
Hapakuwa na jinsi ya CDM kushinda Chalinze (ilikuwa sawa na kuipindua serikali) na ndio maana mpaka Rais wa Zanzibar alifika.Kushindwa kwa RIdhwani lingekuwa pigo kubwa kwa CCM kwa serikali ya babake jambo ambalo hakuna mtu katika mfumo wetu huu angekubali.