Ni maoni yangu tu wanaJF,
Kama ambavyo BAVICHA ilififia na kuzikwa alipotoka tu John Heche kama mwenye kiti wake, na kuchaguliwa chaguo la mwenyekiti, Protas.
Sasa tunashuhudia tena taratibu chama kikuu cha upinzani kikielekea shimoni baada ya chaguo la mwenye chama na mamvi kwa maslahi wayajuayo wao kuteuliwa katibu mkuu, aka "katibu mkuu mchina".
Inasikitisha sana chama tulichokipenda sana kikifa kwa uzembe au kwa maslahi binafsi.
CHADEMA kilikuwa chama hadi Julai mwaka jana, kabla hakijageuzwa kuwa taasisi ya kibiashara.
Lakini hata naibu katibu mkuu Salum Mwalimu alijitahidi sana kukiongoza chama katika kipindi kigumu cha mpito kuelekea uchaguzi mkuu hadi alipotolewa kwa mizengwe wanayojua Mbowe na Lowassa na kuja na chaguo lao ambalo hata hakuna anayejua walikomtoa.
Binafsi nilitegemea huyu kijana shujaa Salum Mwalimu angeteuliwa katibu mkuu.
Haidhuru, lakini tangu uteuzi wa katibu mkuu wao hadi leo tunashuhudia kifo kikikinyemelea CHADEMA.
RIP CHADEMA.
Tutamkumbuka sana Dr. Slaa na Salum mwalimu. Mungu awalinde.