GE2025 CHADEMA kinalaani vikali wimbi la ukamataji na utekaji wa viongozi na wanachama kanda Victoria, hususani mkoani Kagera

GE2025 CHADEMA kinalaani vikali wimbi la ukamataji na utekaji wa viongozi na wanachama kanda Victoria, hususani mkoani Kagera

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
505
Reaction score
887
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinalaani vikali wimbi la ukamataji, utekaji na vitisho vinavyoendelea dhidi ya viongozi na wanachama wake katika Kanda ya Victoria, hususani mkoani Kagera.

Tarehe 16 Oktoba 2025, viongozi na wanachama zaidi ya saba wamekamatwa na vyombo vya dola mkoani Kagera katika mazingira yenye utata bila maelezo yoyote rasmi kutoka kwenye vyombo vya ulinzi na usalama wa raia.

Matukio haya yanajiri wakati ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiendelea na kampeni zake za Urais kwenye kanda hiyo inayojumuisha mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera.

Miongoni mwa waliokamatwa ni:

  1. Chief Adronicus Kalumuna (Mwenyekiti wa Chadema jimbo la Bukoba Mjini na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kanda ya Victoria)
  2. Paulo Shijason Musisi (Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa)
  3. Daniel Damian Lwebugisa (Katibu wa Chadema Mkoa wa Kagera)
  4. Egbert Aloyce Kikulega (Mwanachama)
  5. Ramadhan Fadhiri (Mwanachama)
  6. Levocatus Willison (Mwanachama)
  7. Baziri Waziri (Katibu wa Jimbo la Kyerwa)
Pamoja na matukio haya kutokea kwenye mikoa ya kanda hii ya Victoria, tulitegemea Rais Samia kwenye kampeni zake angekemea, lakini tunasikitika kuona kwamba hiyo haionyeshi dalili zozote za kulinda misingi ya uhuru wa wananchi na haki za binadamu.

Aidha, Khalid Swarehe (Makamu Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Victoria), bado anashikiliwa gerezani baada ya kupwepeshwa kesi ya wizi wa kutumia silaha tofauti na kosa analoshitakiwa nalo.

photo_2025-10-16_22-25-50 (2).jpg
 
"Samuya" na magenge yake wajiandae kukimbia nchi tu, huu moto waliouwasha kamwe hautazimika.
 
  1. Chief Adronicus Kalumuna (Mwenyekiti wa Chadema jimbo la Bukoba Mjini na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kanda ya Victoria)
  2. Paulo Shijason Musisi (Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa)
  3. Daniel Damian Lwebugisa (Katibu wa Chadema Mkoa wa Kagera)
  4. Egbert Aloyce Kikulega (Mwanachama)
  5. Ramadhan Fadhiri (Mwanachama)
  6. Levocatus Willison (Mwanachama)
  7. Baziri Waziri (Katibu wa Jimbo la Kyerwa)
Jambo pekee linaloweza kufanywa na CHADEMA kwa hali iliyopo nchini sasa hivi ni "KUPIGA KELELE" nyingi sana hata kiziwi ikiwezekana asikie.

Taarifa isambazwe kila mahali waTanzania wajue kinacho endelea..

Msichoke, na wala msikate tamaa; haya ni mapambano. Waovu watashindwa tu; hata watumie njia gani; hawaponi.
 
"Samuya" na magenge yake wajiandae kukimbia nchi tu, huu moto waliouwasha kamwe hautazimika.
Huu ni moto utakao waunguza wao. Haya wanayofanya sasa ni ishara nzuri inayoonyesha hofu i kubwa mewaingia; na badala ya kuupoza moto ndiyo wanazidi kuuchochea zaidi.
 
Write your reply...acheni matusi la sivyo wataendelea kunyakuliwa na drones systeam na hamtawaona tena
 
Back
Top Bottom