CHADEMA Kigoma wampania Zitto

CHADEMA Kigoma wampania Zitto

Status
Not open for further replies.
a naye muunga mkono uyu msaliti majority ni ccm. kwann msimpe nafas a kawa Mwenyekiti wenu badala ya jk kikwete...

Endelea kujiliwaza hivo kuwa tunaomuunga mkono zitto ni ccm, siku utakapokuta mmepata 8% uchaguzi mkuu ndo utatambua kama tulikua ccm kweli au wanachama hai wa chama. Make wengine mnapiga kelele na kushadadia mambo si ajabu hata kadi za chama hamna zaidi mapenzi yenu kwa chama ni kupiga kelele na kwenda kwenye videdea na maandamano kuanzisha fujo.
 
anahaki ya kugombea jimbo lolote wamesha mpangia Serukamba aende kwake na yeye atete jimbo kwa chama tawala CCM Nawala si ATC

Huitaji darubini kuitambua misukule ya ufipa humu jamvini... mwenyekiti wa chama ndo anahakisi kiwango cha elimu na upeo wa wanachama na mashabiki wake... hilo shirika la ndege siku hizi linafanya siasa?
 
Kigoma hawajali chama wana angalia mtu mfano kafulila akihamia ccm atapita kama kawaida hivo hivo kwa zitto kigoma yote ni mali yake
 
Mh:Zito ni kisiki cha mpingo...wananchi wa leo kipaumbele chao ni uwezo na utashi wa mtu na sio chama tena,kwani hali halisi ya figisu figisu kama TFF...imekuwa ikionekana ndani ya wanaojiita eti wapinzani...chakushangaza ndani mwao ni mwiko!!!

Hapa wala hatuitaji kupiga lamli ili kufaham mchango wa Mh:Zito kwa taifa la Tanzania,mapinduzi makubwa tumeyaona ndani ya bunge....mkweli na mungwana hili.atalisema tofauti na hapo atakuwa na mgogoro wa nafsi...
Hao wanaojiita wapinzani wake wanatakiwa wajipange miaka mia tisa....
 
Shida ya wakurupukaji wanadhani suala la Zitto kutogombea ubunge Kigoma Kaskazini limekuja juzi baada ya kutemwa Chadema. Kwa kuwakumbusha tu hao Bavicha ni kwamba Zitto alitangaza kutogombea tena ubunge tarehe 27 Sept 2012. Zitto aliyaongea hayo katika mjadala ulioandaliwa na asasi ya kiraia ya Meza ya Duara uliofanyika kwenye Soko la Mwanga, mjini Kigoma.
Sehemu ya aliyosema ilikuwa

"Nimefanya kazi kubwa ya ubunge, nimeleta mabadiliko mengi kuanzia bungeni mpaka kwenye jimbo langu. Nadhani inatosha na hata nikiongezewa miaka mingine sitaweza kufanya yale yaliyonishinda katika kipindi cha miaka kumi."
"Kama Mungu ataniweka mpaka mwaka 2015, sitagombea ubunge tena kwa sababu kazi niliyofanya inatosha. Natangaza rasmi kwamba nitagombea urais kupitia chama changu cha Chadema, bila kusababisha msuguano wowote na sitaki kuingia katika historia ya kurudisha nyuma harakati za vyama vya upinzani kushika dola,"
"Iwapo chama kikiona sistahili au sifai, nitakubaliana na uamuzi wa chama. Watu wengi wanadhani urais ni cheo, hawajui kuwa ni nafasi ambayo inakufanya ufanye vitu ambavyo ni vikubwa na vya maendeleo kwa wananchi,"
"Kwanza nataka niwahakikishie watu wa Kigoma msiwe wanyonge, mna uwezo wa kutoa rais wa nchi hii,"


Na kwa upande fulani hata haya yaliyomkuta ndani ya chama yanachangiwa sana na hili tamko lake la mwaka 2012
 
Last edited by a moderator:
Zitto sio mwanasiasa Jamii ya Mama ana Abdallah amvae ana miaka 45 bungeni.

Zitto aliahidi kuitumikia Kigoma Ks kwa 10 yrs.

Zitto ndio mwanasiasa ambae anaweza kwenda jimbo lilote Tanzania na kushinda uchaguzi.

mnajifariji tu,aje hapa rock city tuone basi? hana jipya kwa sasa.
 
CHADEMA bado ipo Kigoma? Siasa hizi bana huyo jamaa yeye amfurahishe tu Mfalme MBOWE.Zitto jimbo lolote la Kigoma anashinda.

Kama anataka kuaibika aje agombee tu tutamuonyesha kama sisi hatuli chungu kimoja na msaliti
 
inamaana Wana badilishana na Peter Serukamba (CCM).?.....
nimeamini chadema wapo right!..

Zitto ni oil chafu,
 
Tulieni sindano iwaingie, mmemfukuza wenyewe. Suala la kutokugombea jimbo ni ahadi ya muda mrefu wala sio wazo la leo. Toka kampeini za 2010 aliahidi ndo kipindi chake cha mwisho kugombea Kgm Kaskazini, sa kinachowawewesesha mapema ni nini? Kgm mjini wako ladhi jimbo waendelee kulitoa sadaka kwa ccm kuliko kutawaliwa na wachaga. kwani mmewanyanyasa sana waha na kuwatukana vya kutosha hawana haja na nyie.

hana uwezo wa kushinda jimbo lolote Huyo msaliti
 
Waha huwa hawayumbishwi na siasa nyepesi ndio maana kina Kafulila na kina Machali walipofukuzwa CDM walienda NCCR na wakashinda bila Shida.

Umesema Kweli, Kmeo Changu Hakina Option Ya Like Ningekupa. Nilikuwa Buzebazeba Uchaguz Wa S/ Mitaa Niliwashuhudia Waha Wakichagua Watu Zaidi Na Si Vyama. Binafsi Kwa Hili Nawapongeza Sana.
 
Zitto sio mwanasiasa Jamii ya Mama ana Abdallah amvae ana miaka 45 bungeni.

Zitto aliahidi kuitumikia Kigoma Ks kwa 10 yrs.

Zitto ndio mwanasiasa ambae anaweza kwenda jimbo lilote Tanzania na kushinda uchaguzi.

Agombee kule kule Kigoma Kaskazini, kwa nini anawakimbia wapiga kura wake? Au akagombee Serengeti tuone kama atapata hata kama ni kupitia CCM.
 
Kwa kawaida watu huwa hawapotezi muda kujadili mwendawazimu, ukiona Kila siku watu wanamjadili mtu Fulani wakati mwenyewe hajishughulishi nao ujue huyo jamaa ni potential
 
Zitto azidi kuitafuna Chadema
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom