CHADEMA kiboko ya Magamba hata CC wanajua hivyo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA kiboko ya Magamba hata CC wanajua hivyo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Nov 24, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Nov 24, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,754
  Likes Received: 82,699
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]CC yataka JK akutane na vyama vyote, si Chadema [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Wednesday, 23 November 2011 20:35 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  Waandishi Wetu
  KAMATI Kuu (CC) ya CCM, imemwagiza Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete akutane na vyama vyote vya siasa badala Chadema peke yake.

  Kamati hiyo imesema ni muhimu hatua hiyo ya kuzungumzia muswada wa Katiba ikafanywa kwa umakini mkubwa kwa kuwa jambo hilo, linawagusa Watanzania wengi.

  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema jana Mjini Dodoma kuwa Muswada wa Marekebisho ya Katiba ni moja ya mambo yaliyojadiliwa kwa kina katika kikao hicho cha Kamati Kuu.

  Agizo la chama hicho limekuja baada ya Rais Kikwete kupokea na kukubali ombi la Chadema la kukutana naye ili kujadili suala la Katiba.

  Katika kutekeleza azma hiyo ya kuonana na Rais, Chadema iliunda timu ya watu saba chini ya Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe ambayo imepewa kazi ya kushughulikia suala hilo.

  “Chama kimempongeza mwenyekiti kwa hotuba yake nzuri kuhusu mchakato wa Katiba Mpya. Pamoja na kukubali akutane na Chadema, tumetahadharisha kuwa lazima kushirikisha na wajumbe wengine kutoka vyama vyenye uwakilishi ndani ya Bunge isiwe Chadema pekee,’’ alisema Nape.

  Alisema CCM kinaamini kuwa njia ya majadiliano waliyoitumia Chadema katika kutafuta haki ni nzuri na fursa hiyo ikitumiwa vizuri, inaweza kuleta maelewano mazuri na faida kwa jamii.

  Viongozi wa dini wampongeza JK
  viongozi wa dini, wasomi na wanasiasa, wamepongeza hatua ya Rais Jakaya Kikwete kukubali kukutana na viongozi wa Chadema ili kusikiliza madai yao juu ya Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba wa mwaka 2011.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, walisema uamuzi huo wa Rais umeonyesha kuwa amesoma alama za nyakati na wakamtaka atafute fursa ya kukutana na wadau wengine kupata maoni yao pia kuhusu suala hilo.

  Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bashiru Ally alisema ni muhimu Rais akakutana na wadau hao kwa awamu, kwa kuwa Chadema hawawezi kuwawakilisha watu wote wanaopinga muswada huo.
  “Chadema wajue wana madukuduku yao ambayo si ya watu wote, hivyo kuwe na awamu ya kukutana na Rais kwa ajili ya jambo hili,” alisema.

  Alisema ni muhimu Rais akawa msikivu na akazialika taasisi zote Ikulu na kujadiliana nazo ili kupata ufumbuzi wa suala hilo lililoonekana kuwa bado ni tata.
  “Suala la Katiba ni kubwa na hiyo aliyofanya Rais ni hatua moja hivyo ni bora taasisi zote zihusishwe na utafutwe muda wa kukutana naye pamoja,” alisema.

  Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe alisema ni muhimu kwa wadau wote wa Katiba kupewa fursa ya mazungumzo ili muafaka upatikane kwa lengo la kuwa na Katiba bora.

  Zitto alisema hatua hii ya Rais Kikwete kukubali kukutana na Chadema ni njema: “Nchi haiongozwi barabarani. Kitendo cha Chadema kuachana na maandamano na kuamua kwenda kukutana na Rais na yeye kukubali hilo, nawapongeza wote,” alisema Zitto.

  Katibu Mtendaji wa Baraza la Makanisa ya Pentekoste Tanzania (PCT), Dk David Mwasota amepongeza hatua ya Rais Kikwete kukubali kukutana na uongozi wa Chadema.

  Dk Mwasota alisema hatua hiyo ni njema na inaonyesha mwanga bora na mwelekeo wenye kuleta matumaini mapya kwa taifa. Alisema kwa muda sasa kumekuwa na matukio yanayoonyesha ishara mbaya likiwemo la mchakato wa kuandika Katiba Mpya ambao wabunge wa Chadema na NCCR-Mageuzi walisusia mjadala wake bungeni.

  “Tunampongeza Rais Kikwete, hii ni hatua inayoashiria mwanga bora kama wa asubuhi, ni imani yetu kuwa mazungumzo hayo yatazaa matunda na kurejesha amani na utulivu ambao tayari kumekuwa na ishara mbaya juu yake,” alisema Dk Mwasota.

  Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba alisema hatua ya Chadema kukutana na Rais ni jambo jema na inastahili kufanywa pia kwa vyama vingine vya siasa.

  Alisema Rais ni mkuu wa nchi na kiongozi wa wote hivyo Chadema kutaka kukutana naye kwa ajili ya kuwasilisha madai yao wako sahihi.Kuhusu mjadala wa Katiba alisema ni mchakato unaohusu wananchi wote na kwamba wanasiasa wana nafasi yao kama ilivyo kwa wananchi.

  SOURCE: Mwananchi

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #2
  Nov 24, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  CCM inaongoza nchi kwa Dira za CHADEMA
   
 3. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #3
  Nov 24, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Kukutana na vyama vyote??? - Ili CCM na CUF wakapigilie msumari kuwa mchakato ni sahihi na vyama vingine kama TLP vikapokee posho na kuunga mkono hoja ya CCM na CUF. Hivyo wakija kuhesabu kura (si hoja) itaonekana ni CHADEMA tu ndiyo inayopinga huo mchakato. Magamba kwa faulo hawajambo!!!
   
 4. P

  Panda Kapesi JF-Expert Member

  #4
  Nov 24, 2011
  Joined: Nov 22, 2011
  Messages: 284
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 60
  "Zitto alisema hatua hii ya Rais Kikwete kukubali kukutana na Chadema ni njema: “Nchi haiongozwi barabarani. Kitendo cha Chadema kuachana na maandamano na kuamua kwenda kukutana na Rais na yeye kukubali hilo, nawapongeza wote,” alisema Zitto."


  Huyu bwana Zito tumweleweje? Mbona kama anakikandya chama chake?
   
 5. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #5
  Nov 24, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Ondoa hofu, demokrasia inampa kila mtu fursa ya kutoa maoni yake.
   
 6. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #6
  Nov 24, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Mzee wa Rubisi,

  Umenena. Huo ni ukweli mtupu ambao hakuna anayeweza kuupinga.
  Kwa kifupi tu nisema kuwa hata hili swala la mchakato wa Katiba Mpya ni wazo la CHADEMA ambalo CCM walikuwa hawanalo lakini Mwenyekiti wao from nowhere alilirukia tu kama kibaka anayemrukia mtu kumpora mali zake. Ndivyo alivyofanya Kiwete na ndiyo maana hili swala sasa linatusumbua kwa sababu siyo agenda ya CCM from the very beginning.

  CC/NEC wamekutana Dodoma kuvuana Magamba lakini yakawashinda badala yake WAMERUKIA HOJA YA CHADEMA KUONANA NA RAIS KIWETE HUKU WAKISHINIKIZA NA VYAMA VINGINE VIHUSISHWE!!!Kweli ri-CCM limekufaga na kuozaga moja kwa moja!
   
 7. k

  kisimani JF-Expert Member

  #7
  Nov 24, 2011
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 553
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Kwani hivyo vyama vingine vimeomba kukutana na KJ or sorry JK?? Nyie CC ya magamba ni bora muwe mnakaa chini na kutafakari kitu kabla hamjapayuka kwa wananchi...

  Kwa mtu mwenye uelewa hiyo statement ni upuuzi, unaonyesha ni jinsi gani chuki zilivyowajaa na huku mkiogopa kuzidiwa kete za ukweli na CDM.
   
 8. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #8
  Nov 24, 2011
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Mimi naona ni vyema kila chama wakamwone kivyao kama wana hoja ya kumweleza na si kukaa chuni ya mwamvuli wa CDM
   
 9. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #9
  Nov 24, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Sijui lini tutaacha usanii hapa Tanzania? Watu wanapotoa pendekezo la rais kukutana na vyama vingine kwa mantiki ipi? Kuna mambo mengi yanayotakiwa kujibiwa kabla ya kuunga mkono wazo la rais kukutana na vyama vyote kwa sababu:
  1. Chama cha Mapinduzi ndicho chama ambacho rais anayeongoza serikali anakotokea. Ni nini ambacho CCM wamashindwa kumweleza rais katika vikao vyao kama CC na NEC kiasi kwamba wamfuate tena Ikulu? Ina maana kwamba wakienda kutana naye Ikulu atakuwa mtu tofauti?
  2. Wabunge wa CUF waliungana na wabunge wa CCM katika kuunga mkono muswada, watakapoenda Ikulu watatakuwa na wazo jipya ambalo tofauti?
  3. Vyama vingine havijaomba kuonana na rais, kwanini watengenezewe utaratibu wa kuoana na rais? je ajenda ya majadiliano itatoka kwa rais au kwao? Kama ajenda itatoka katika vyama hivyo, hiyo ajenda itakuwa ipi wakati hawakuionesha tangu mwanzo?
  4. Kimsingi Chadema ndio walioonesha msimamo wao tangu mwanzo walipopinga muswada kusomwa mara ya pili, na hawakuwa tayari kuunga mkono upitishwaji wa muswada huo. Vyama kama CCM na CUF waliunga mkono hoja bila kutoa hoja za maana za kuunga mkono muswada zaidi ya kuwajadii Chadema tena katika mambo binafsi. CCM na CUF watakwenda kuonana na rais kumweleza nini?
   
 10. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #10
  Nov 24, 2011
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Atakutana vipi na vyama ambavyo havina issue naye? Hayo ndo mambo walikwenda kuongea Dodoma? Kweli ndo maana mambo yame kuwa hivi, CC ina mawazo mgando
   
 11. h

  homeboyz Member

  #11
  Nov 24, 2011
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nape umezidi kudandia hoja za watu ulikua wapi kuvieleza vyama kukutana na Raisi leo chadema waombe kukutana nae wewe upendekeze Rais kukutana na vyama vyote ,je unaelewa ni nini Chadema wamepanga kuongea na Rais? kama ingekua hivyo chadema kama waanzilishi wa ombi wao ndo wangepanga vyama kukutana na Rais lakini kwa mtazamo wao wameomba wao kama chadema na si vyama vyote, tunaomba chadema ikutane na Rais kama ilivyokua katika ombi lao, hayo ya vyama vyote jipangeni muombe kwa muda wenu.
   
 12. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #12
  Nov 24, 2011
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  kinanani wawakilishi wa wananchi wanaopinga kama si Chadema na baadhi ya NCCR wote waliobaki wameunga mkono sasa akutane nao ili nini wakati wao hawakuwakilisha wananchi bali mawazo yao
   
 13. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #13
  Nov 24, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Aibu kubwa sana kwa wabunge wa CCM na CUF pamoja na spika wa Bunge na imeonesha jinsi gani walivyo vilaza....
   
 14. j

  jigoku JF-Expert Member

  #14
  Nov 24, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  CCM jamani mtakata roho lini maana tumewauguza mpaka sasa tumechoka,ni bora tujue mnakata roho lini bawana tumechoka kuwauguzana mmeshatuingizia hasara kubwa isiyoweza kufidiwa mmetupotezea rasilimali nyingi sana,sasa wewe mmoja tutakuuguza mpaka lini?Nasema hivyo tu kwa kuangalia tukio la jana baada ya kuibuka na KUTAKA RAIS AONANE NA VYAMA VYOTE,HILI LIMETOKA WAPI TENA,NYINYI NI WASEMAJI WA DP,TLP,NCCR,UDP,NA VINGINE,NDIO MNAWEZA KUWASEMEA CUF MAANA HUYO NI MKEO THAT IS FINE ILA HAWA WENGINE KWA NINI MNAWASEMEA?NANI ALIWAAMBIA WANATAKA KUKUTANA NA RAISI?HATA HIVYO AMBACHO HAMJAKIELEWA NI NINI?MAANA CHADEMA WANATAKA KUKUTANA NA RAIS NA NDIO WAMEWASILISHA BARUA YAO IKILEZA HIVYO,Hivyo vyama vingine vinatoka wapi tena,KUDANDIA DANDIA HUKU KUTAWAHARAKISHIA KIFO CHENU.
   
 15. Ufunuo

  Ufunuo JF-Expert Member

  #15
  Nov 24, 2011
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  reverse reaction (kikemia zaidi)
   
 16. N

  Ndole JF-Expert Member

  #16
  Nov 24, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 352
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kweli ni aibu kubwa kwa spika na ccm yake. Inakuwaje muswada umeshapitishwa na bunge na baadae ukajadiliwe tena kwa raisi sijawahi kuona hii kitu. Shame on Anna Makinda ya ndege. Wangekuwa na akili wala wasingeupitisha bali wamwachie raisi ajadiliane na watu wote halafu atoe muafaka. shame on you ccm na cuf yako pamoja na Mrema wako.
   
 17. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #17
  Nov 24, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Brilliant. Yaani umejenga hoja zote za msingi na zimeeleweka. Watu wanasahau kwamba CHADEMA waliomba kuonana na rais na wala sio kwamba wameitwa na rais kujadili suala hilo.

  Sasa CC wanajenga hoja zisizo na mashiko kabisa! Na Nape naye atulie jamani, amezidi kuropoka ropoka! Silence is sometimes golden!
   
Loading...