CHADEMA Kanda ya Victoria imetengua uteuzi wa Mbunge wa Viti Maalum Susanne Maselle kwa kukaidi amri ya kutohudhuria Bunge

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,076
4,113
Uongozi wa juu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Viktoria umetengua uteuzi wa Mbunge wa Viti Maalumu kupitia chama hicho Susanne Maselle ikiwa ni adhabu ya kukaidi amri ya chama hicho kuzuia wabunge wake wasihudhurie vikao vya Bunge na Kamati za Bunge.

Mbunge.jpg
 
Wabunge wenyewe wanakula raha jijini Dar Es Salaam sasa sijui nani yupo yule aliyehatarisha maisha yake na yupo bungeni na yule aliyekimbia bunge na jimbo lake anakula maisha Dar Es Salaam. Pia nashangaza hii ndio demokrasia wakati hili jambo ni hiari ya mhusika akikaidi si ni ju yake mwenyewe aliyekaidi?au basi Chadema wana lengo tofauti.
 
Democracy ina vigezo!!
Sio kwa sababu mtoto ni wako unaweza muuwa!
 
Kisheria Bonny bado ni meya wa ubungo ila kisiasa....!
sasa mjomba wako mbona kamkomalia... kasema akigusa mlango wa ofisi tu anakwenda kulala segelea ili atie adabu...kosa kufanya fujo ofisi za Halmashauri..
 
Uongozi wa juu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Viktoria umetengua uteuzi wa Mbunge wa Viti Maalumu kupitia chama hicho Susanne Maselle ikiwa ni adhabu ya kukaidi amri ya chama hicho kuzuia wabunge wake wasihudhurie vikao vya Bunge na Kamati za Bunge.

Badala mtengue wale walio kaidi self isolation wakaenda kudanga Dar, mnatengua wale walio amua kuendelea kutumikia wananchi. Chama hakitadumu kwa hekaya. Mlidhani propaganda za corona zingewanufaisha sasa zitawabomoa. Mungu yu pamoja na watu wake.
 
Sasa Vagi linaanza!!!

Sijui Niko ndotoni mwenzenu!!!
Lakini wacha niseme ndoto yangu

Kuna ngumi zitarindima hivi punde ndani ya Chama, ukimtimua Mbunge mmoja ndani ya Chama, kuna aliyekuwa rafiki yake naye hatapenda huo uhuni ndani ya Chama,

Mbona naanza kuona ngumi zikitupwa Kwa M/kitu chake hapo!!!

Jumapili kwenye Ibada Mch Gwajima aliinua sauti akasema!!! Chadema wapigweeee!!!!

Labda ndo hayo maombi yameanza kuwapata!!!😂
Yetu macho
 
Back
Top Bottom