CHADEMA kama bado mnazuzuka na mafuriko, nawakumbusha tu huyu ni Dkt. Slaa 2010

Katika yote uliyosema Lisu wala Membe hawajasema hata moja katika kutafuta wadhamini sasa nyomi atapataje?

Chadema ya Slaa ilikuwa na ajenda mkuu! Hii ya sasa hivi ni ya kumshambulia Magufuki zaidi.
Be serious? Ulimsikia Lissu Shinyanga na Bunda? Hivi hakusema kuhusu Kilimo? Hakusema kuhusu Ajira? Let's be real
 
Mh! Dada Mange anawajua vizuri watanzania walivyo.
Sasa maandamano ya mange hayakua na uongozi tofauti na CHADEMA ambao hata mapokezi ya Lissu yaliratibiwa ngazi ya kuanzia misingi hadi Kanda ndio maana nyomi lilipatikana licha ya vitisho vya polisi.

So ni mambo mawili tofauti
 
Radical approach haiwezi saidia Tanzania! Atarudi tu huko Ubelgiji na aibu yake. Ndiyo maana familia yake ameiacha huko.
Haiwezi? Unakumbuka vurugu za Arusha kuelekea uchaguzi wa meya? Radical approach haikusaidia? Vipi Zanzibar haikupelekea kuundwa SUK?

WaTZ wanaweza sana tu kuandamana sema chaguzi zote haijawahi tokea mpinzani aliye order maandamano baada ya matokeo kutokea sasa cjui mifano mnatoaga wapi kuwa waTZ ni waoga.
 
Naomba huu uzi ubaki ili angalau kuwakumbusha hawa ndugu zetu kwamba ushindi unapatikana kwa mikakati, mafuriko ya watu kwa hapa Tz hayasaidii kitu.

Jionee mafuriko ya Slaa mwaka 2010 na bado aligalagazwa.

Hapo bado ya Lowassa 2015.

Wewe si Chadema. Kama wanajazana mikutanoni na mshindi atakuwa Magufuli wenu, kinakuwasha nini?

Jibu jepesi ni hili: wafuasi wenye mgombea bora hawana muda na wapinzani wao "wenye mgombea mbovu." Mwenye lake zuri hana muda na baya la mwenzake..

Chadema wapo bize kumnadi mgombea wao, ninyi mpo bize kumbeza mgombea wao badala ya kumnadi mgombea wenu.
 
Sasa maandamano ya mange hayakua na uongozi tofauti na CHADEMA ambao hata mapokezi ya Lissu yaliratibiwa ngazi ya kuanzia misingi hadi Kanda ndio maana nyomi lilipatikana licha ya vitisho vya polisi.

So ni mambo mawili tofauti
Point yangu ilikuwa ni kwamba watanzania ni waoga na hili suala linajulikana wazi tu,polisi wangetaka kweli wasijikusanye watu basi pale asingekanyaga mtu.
 
2010-15; Kuna kitu huelewi kabisa, Dr Slaa alifanya operation za chama karibu kila wiki kiufupi walikuwa na M4C kila kukicha kwahiyo walikua na platform kubwa sana ya kuwafikia wananchi.
Let alone CHADEMA ilijengwa bungeni enzi hizo lipo live watu wakiona michango ya Dr Slaa,Zitto,Wangwe na Mdee waliona haja ya kuwaongezea nguvu.

2020: Situation ya sasa ni tofauti, Lissu hakua active politician Tz tokea ashambuliwe.

CHADEMA haikua active majukwaani kupitia M4C sababu mikusanyiko ya kisiasa ilifutwa ikabakia CCM pekee.

Bunge lililowapa umaarufu CHADEMA halikua live tena wachache wenye mitandao ndio waliibia clip fupi YouTube.

Hivyo ilikua anticipated CHADEMA imekufa, imekimbiwa na wabunge, sijui imekosa ushawishi. Sasa kiukweli hakuna aliyetegemea kuwa Lissu atapata platform kma hii ya maelfu ya watu. So tuwe wakweli kupata nyomi awamu ya 5 ni "dili" kuliko awamu zilizopita kutokana na sababu tajwa hapo juu.

Kuhusu Lowassa na Dk Slaa kugaragazwa. Lissu amekiri hao wote walishinda ila walipoporwa ushindi ''walimuachia Mungu''. Ikimaanisha yeye anafikiria radical approach kuliko hao wenzake. Till then ulinganisho wako hauna maana yeyote upo nje ya muktadha kabisa.
Naam, pia bado inakumbukwa vizuri tume ilifanya uhuni wa kubadili kanuni na taratibu zilizo kuwepo, baada ya Slaa kuongoza matokeo ya awali takribani mikoa mitatu. Tume ikazuia kutangaza matokeo ya urais level zote za chini isipokuwa makao kwa makao makuu ya tume!
 
Back
Top Bottom