zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 19,039
- 28,689
Tallying center ya UKAWA 2015 ilivamiwa na polisi na kuporwa PC zote. LHRC wakiwa chini ya mwavuli wa waangalizi wa chaguzi walipo tally matokeo yalionyesha Lowassa kaongoza kwa mbali. Ila tuliona walivamiwa ofisi zao PC zao zikaporwa na mpaka leo hazijarudishwa. Sasa kma mtu wao alishinda why wapore database za wengine ilihali ni majumuisho binafsi sio ya NEC? walikuwa wanaficha nini?Ushahidi wa hilo uko wapi?
Siku zote wanasiasa wa Afrika hawakubali walishindwa kihalali kwa uwezo wa mshindani.
Mfanano wa kura kwenye majimbo kadhaa, mfano 2010 majimbo zaidi ya 6 yalikuwa na tarakimu zinazofanana za kura za Urais kati ya Slaa na kikwete!! Coincidence?
2015 tuliona majimbo mfano Tunduma na Bumbuli kura za Urais ni nyingi kuliko za ubunge. Achilia mbali figisu za vituoni hasa kwenye kujumuisha matokeo. Kiukweli moja ya chanzo ni mawakala wanahongwa sana na CCM afu fomu zinachezewa, still masanduku yanaongezwa na huna la kufanya.
Mambo ni mengi ila ushahidi wa kimazingira unaprove CCM huwa wanaiba kura.