Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,437
- 5,235
Ila Jeshi letu la Polisi wanafanya mambo yao nje kabisa na maadali kabisa!
Mlimchukua mkasema mnampeleka Tarime, lakini mkapelekea sehemu nyingine na mkakaa kimya kama hamjui chochote. Kelele zimekuwa nyingi ndio mnakiambia chama alipo kiongozi wao!
Acheni huo ushamba wenu mnaendelea kujichafua zaidi
================
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinapenda kuutaarifu umma kuwa Makamu Mwenyekiti Taifa, Mhe. John Heche anashikiliwa kwenye mahabusu ya Jeshi la Polisi Mtumba, jijini Dodoma.
Mheshimiwa Heche leo Ijumaa, tarehe 24 Oktoba, 2025 alihofiwa na Idara ya Uhamiaji mbele ya Wakili wa Chama na Kaka yake akituhumiwa kuvunja Sheria za Uhamiaji kwa kile walichosema alivuka mpaka wa Tanzania na kuingia nchini Kenya bila kufuata taratibu.
Pamoja na kosa hilo alilotajwa ambalo lina dhamana, Jeshi la Polisi limekataa kumpa dhamana likisema kuwa kuna maelekezo kutoka juu kuwa aendelee kushikiliwa mahabusu.
Mhe. Heche alikamatwa na Jeshi la Polisi juzi Jumatano kwenye geti la Mahakama Kuu Masijala ya Dar es Salaam kabla ya kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi (Central), Dar es Salaam kisha jeshi hilo linasemekana linasafirisha kumpeleka Polisi Tarime mkoani Mara.
Soma Pia:
Tunamtaka Rais Samia aache kuvutia vibaya vyombo vya Ulinzi na Usalama kuwakamata na kuwaweka kizuizini washindani wake wa siasa.

- Mnyika: Nimedokezwa na ofisa wa Polisi kuwa John Heche yupo Dodoma
- John Heche akamatwa akiwa Mahakama Kuu akijiandaa kuhudhuria kesi ya Tundu Lissu